Maswali hayo ya Pesa utauliza wewe tu lakini Viongozi wa Yanga wanashukuru kurudishiwa Pesa zao bila ya kuuliza swali lolote kwasababu wanaijua TAKUKURU balaa lake.
Kama hujui na ulikuwa hufuatilii hili sakata basi hizo USD 30K alipewa Morrison kama Advance kwa ajili ya kusaini Mkataba mpya ambao baada ya Simba kumpa zaidi akagoma kuongeza Mkataba mpya na Yanga wakaona isiwe Shida bora wamsainie tu ili mambo yaishe.
Kiufupi hizo hela ni Hongo/Rushwa ndiyomana Viongozi wa Yanga hawatozihoji bali watazipokea tu wakirudishiwa.
Kuhusu Kupelekwa Kamati ya Maadili TFF walishafafanua nadhani hujafatilia. Sababu ni Kwamba 'Amesaini Mkataba na Simba huku akijua Kuwa Shauri lake lipo Mezani na kuzusha taharuki kinyume na Kanuni za TFF'.
Lakini Utopolo hamufuatilii mambo hatimae munaishia kuishi kwa Mabishano tu.