Moscow, Urusi: Shambulio la kigaidi laua Watu zaidi ya 130
Miafrika minafiki sana hii ya JF tukio la Oct 7 ilikuwa inakesha JF kusema Magaidi wa Hamas lazima wamalizwe mabwana zao hapo Urusi yamejificha kwenye mashimo kama nguchiro hayajui hata yaandike nini[emoji1787]
Umeshajua ni watu gani wamehusika na huo ugaidi??
 
Kwa sababu ugaidi ni tofauti sana na matatizo ya akili au ugomvi binafsi wa watu mitaani. Ugaidi huwa unapangwa, visa vya ufyatulianaji risasi Marekani watu hawakai chini wakafanya mipango.
Hayo mauaji kwann yasitokee kwenye nchi zingine lakini yatokee Marekani tu ,au Marekani ni nchi yenye wendawazimu wengi kuliko nchi yeyote duniani?
Kama ni suala la umiliki wa silaha mbona zipo nchi nyingi ambazo udhibiti wake wa silaha sio mkali kama Marekani lakini hatusikii mauaji ya kiholela ndani ya nchi hiyo?
Kitendo cha vyombo vya usalama vya nchi yeyote kushindwa kulinda maisha ya maelfu ya watu wake bila kujali yanatishiwa na nani ni ishara ya udhaifu tena mkubwa.
 
Gaidi si angerusha bomu tu?

Itakuwa ni waharifu tu
Tatizo mnajua ugaidi lazima mtu awe muislamu kavaa kanzu na kujilipua.

Gaidi hata wewe ukienda kulipua watu pale kariakoo kisa serikali imewafunga wachungaji flani jela huo ni ugaidi pia.

Ugaidi ni matumizi ya vurugu zisizo halali au tishio la vurugu kinyume cha sheria ili kuleta hofu;
 
Hayo mauaji kwann yasitokee kwenye nchi zingine lakini yatokee Marekani tu ,au Marekani ni nchi yenye wendawazimu wengi kuliko nchi yeyote duniani?
Kama ni suala la umiliki wa silaha mbona zipo nchi nyingi ambazo udhibiti wake wa silaha sio mkali kama Marekani lakini hatusikii mauaji ya kiholela ndani ya nchi hiyo?
Kitendo cha vyombo vya usalama vya nchi yeyote kushindwa kulinda maisha ya maelfu ya watu wake bila kujali yanatishiwa na nani ni ishara ya udhaifu tena mkubwa.
Usichanganye mambo jikite kwenye mada husika, CIA hata hawahusiki sana na mambo ya ndani ya Marekani.
Pia suala la silaha kwa raia Marekani ni kubwa mno juu ya uwezo wako kulielewa. Pia hakuna nchi yenye bunduki nyingi mikononi mwa raia zaidi ya Marekani na hakuna nchi ambayo sheria za kununua na kumiliki bunduki ni rahisi kuliko Marekani.
 
Picha za kwanza za wanaohisiwa ni magaidi zimechapishwa na media za Urusi.
 
Attachments

  • 20240322_235624.png
    20240322_235624.png
    806.3 KB · Views: 2
CIA walipata taarifa mapema miezi kadhaa kabla ya tukio ila kulitokea mkanganyiko kati yao na FBI pamoja wanasiasia kutotilia maanani baadhi ya taarifa za tahadhari hali iliyopelekea taarifa muhimu kutofanyiwa kazi na maafa baadaye.
Unamaamisha hawakujali lolote kuhusu uhai wa watu wao
 
America katoa tahadhari na kweli imetiki, cha ajabu katoa tahadhari kwa nchi pinzani, ila kwake matukio kama haya huwa yanatokea na wala hashituki.
Uchawi upo duniani 😂
Ughaidi wa kupangwa haujatokea marekani tangu 9/11; kinachotokea ni mass shootings za kiholela ambazo siyo planned bali ni matukio ya mtu mmoja mmoja kuchukua mabunduki yake na kwenda kuua watu hovyo.

CIA hawafanyi kazi ndani ya Marekani, na vile vile huwa hawafanyi kazi na mtu mmoja mmoja bali hufuatilia mtililiko wa information zinazuhusu makundi ya watu nje ya nchi.

Urusi ilipoachagua kuwa taifa la kighaidi kwa kuvamia nchi jirani, ikajikosesha nafasi ya kuwa inapewa tips kutoka nje
 
Hapa naona kuna nadharia kama 2.

1. Inawezekana wakawa ni magaidi kutoka middle east ambao ipo wazi Russia ilikwisha wahi kushiriki kwenye vita kuwashambulia ISIS pale Syria kulinda serikali ya Assad. Inawezekana ISIS wakawa wameona ni muda sahihi kufanya mashambulizi kulipa kisasi kwa sababu Russia kwa asilimia kubwa katika intelligence, ulinzi na nguvu za kijeshi zimeelemea zaidi Ukraine sasa ISIS wameona nafasi ya wazi kulipiza kisasi, tufahamu kwamba Russia inapigana na NATO.

2. Inawezekana ni magaidi kutoka Ukraine au middle east ambao wameamua kulipiza kisasi kwa shinikizo la nchi za magharibi(NATO).

Lakini yote na yote Russia sio Zimbabwe wala Libya, kwa intelligence waliyonayo watachinja hao magaidi mmoja mmoja hata wakienda sayarini kujificha, FSB former KGB sio watu poa.
 
Tatizo mnajua ugaidi lazima mtu awe muislamu kavaa kanzu na kujilipua.

Gaidi hata wewe ukienda kulipua watu pale kariakoo kisa serikali imewafunga wachungaji flani jela huo ni ugaidi pia.

Ugaidi ni matumizi ya vurugu zisizo halali au tishio la vurugu kinyume cha sheria ili kuleta hofu;
Kama zile vurugu zinazotokeaga wakati wa Uchaguzi ni Ugaidi sio Ugaidi?
 
Back
Top Bottom