Moshi: Amuua mama yake wakigombea mali za marehemu baba yake

Moshi: Amuua mama yake wakigombea mali za marehemu baba yake

Huko moshi jamaa wa miaka 54 amemuua mama yake wa miaka 74 kwa sababu ya ugonvi wa mali alizoacha baba ama mume wa marehemu ambae ndio baba wa mtuhumiwa.

Marehemu aliacha mashamba, hayo ndio yameleta mgogoro hadi jamaa akaamua kumuua mama yake.

Matukio ya hovyo ya watu kuua wazazi wao kisa mali yanashamiri sana Kilimanjaro.
---

Adela Mushi (74), mkazi wa Okaseni, kata ya Uru kusini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa na shoka sehemu ya usoni na mwanaye, anayedai mali zilizoachwa na marehemu baba yake.

Inadaiwa kuwa mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 54, alifanya tukio hilo usiku wa Septemba 23, 2024 na kisha kutelekeza mwili wa mama yake ndani ya chumba chake alichokuwa anaishi.

Mwili wa mama huyo ulikutwa ukiwa umelazwa kifudifudi huku shingoni kukiwa kumefungwa kipande cha kanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa jeshi hilo linamshikilia mwanaume huyo kwa mahojiano zaidi.

“Septemba 23, 2024 usiku wa saa 4, maeneo ya Uru Okaseni, mwanamke ajulikanaye kwa jina la Adela Dominick Mushi, aliuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani kisha kunyongwa kwa kutumia kipande cha kanga na mtoto wake aitwaye Nemes Dominic,” amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa , lakini wawili hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu wakigombea mashamba na mali za marehemu.

Mwananchi
Alimkosa Baba, amechagua kumkosa Mama na mali amekosa pia. Ni ugonjwa wa akili tu huo.
 
5
Unaweza kuta huyo muuaji alikuwa akiishi nyumbani kwa huyo mama na hiyo ikawa rahisi kumuuwa,wazazi watoto wenu wakishakuwa fukuza hapo nyumbani wakatafute miji yao,ama kwa kuwagawia ardhi yako,au watafute wenyewe,maana ukikaa nao kuna uwezekano wasijitafute maana wanajuwa wewe utakufa miaka michache ijayo,hivyo mali watazirithi,usipokufa mapema wanakutanguliza.
4 final hii mkuu means akishaona baba kaenda nani akae nyumban akarudi sasa maza inaonekana akawa anamwekeaa 😉 hahaha akamalizana nae sasa anakosa mama na mali huyu lazima wamnyonge

Dinia maumivu wengine tunaenda kulilia makaburin kwa mama zetu tunawamiss wengine wanaua aisee
 
KUNA MAWILI HAPA KWELI AMEKOSA

SEMA HAWA WATOTO BABA ZAO ALIACHA MALI

SASA KAMA VIPI...UNAMALI ZA WATOTO GAWA KIASI....UNASUBIRI UFE WATOTO WAANZE KUUANA
 
wachaga kwa roho mbaya ni kama samaki na maji huwezi vitenganisha
 
wachaga kwa roho mbaya ni kama samaki na maji huwezi vitenganisha
 
Ukanda huo kuna shida kubwa sana kuhusiana na suala la kugombea mali. Ni hatari Sana.
Mkuu kwani watu wa uko kwani tamaduni zao sina semaje kuhudu mirathi ikitokea Baba Kafariki na Mke kabakia? Au wenyewe hawana utaratibu wa mirathi ya kimila, Mfano watoto hamrithi mali za Mzazi angali bado yupo hai sasa huyo Mzee wa zaidi ya miaka 50 anatakaje kurithi mali za Mzazi wake kabla hajafa.
 
Inashangaza sana,

Unamuua Mama yako mzazi ili uchukue mali,

Hizo mali unaenda kutumia na nani ambaye ana thamani zaidi kuliko Mama yako mzazi aliyekuzaa?
Wachaga wana utaratibu mbovu sana wa mirathi ilitakiwa huyo Mama awagaiye maeneo watoto wake wakiume kwasababu hayo mashamba ya zao la ukoo kama ana watoto wakiume Watatu anawakatia kila mmoja eneo lake kisha yeye ana baki kwenye eneo la Mumewe.
 
Dah miaka 74 mama yake si angemlea tu na sio kumuua kwa maana angemuachia tu mama ake then after a while vingerudi kwake vyote.
Mkuu uwezi jua labda Mama yake alikua ana uza mali za ukoo hovyo hovyo kuna wazaz wengine wana akili mbovu, kuna Baba yetu mdogo yeye aliuza eneo lenye kaburi la Babs yake ambaye ni Babu yetu tukitaka kwenda kutembelea kaburi la Babu kijijin inatubidi tukaombe kwa mtu ndiyo aturuhusu
 
Kuna watu wengine wanakosa uzao/watoto wanajilaumu sana, kumbe Mungu anawaepusha mabazazi kama haya yakuwanyanyasa baadae
 
Huko moshi jamaa wa miaka 54 amemuua mama yake wa miaka 74 kwa sababu ya ugonvi wa mali alizoacha baba ama mume wa marehemu ambae ndio baba wa mtuhumiwa.

Marehemu aliacha mashamba, hayo ndio yameleta mgogoro hadi jamaa akaamua kumuua mama yake.

Matukio ya hovyo ya watu kuua wazazi wao kisa mali yanashamiri sana Kilimanjaro.
---

Adela Mushi (74), mkazi wa Okaseni, kata ya Uru kusini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa na shoka sehemu ya usoni na mwanaye, anayedai mali zilizoachwa na marehemu baba yake.

Inadaiwa kuwa mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 54, alifanya tukio hilo usiku wa Septemba 23, 2024 na kisha kutelekeza mwili wa mama yake ndani ya chumba chake alichokuwa anaishi.

Mwili wa mama huyo ulikutwa ukiwa umelazwa kifudifudi huku shingoni kukiwa kumefungwa kipande cha kanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa jeshi hilo linamshikilia mwanaume huyo kwa mahojiano zaidi.

“Septemba 23, 2024 usiku wa saa 4, maeneo ya Uru Okaseni, mwanamke ajulikanaye kwa jina la Adela Dominick Mushi, aliuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani kisha kunyongwa kwa kutumia kipande cha kanga na mtoto wake aitwaye Nemes Dominic,” amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa , lakini wawili hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu wakigombea mashamba na mali za marehemu.

Mwananchi
Harafu mnasema adhabu ya kifo ifutwe
 
Back
Top Bottom