Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Marehemu Happiness Kasmiry kutoka kijiji cha Usari, Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.
Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa jina la John Kasmiry alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.
Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.
Marehemu ameacha watoto watatu wadogo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ismail Urassa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake.