Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Watu wote walozunguka pale walishindwa msaidie aende hospital ,?mwenyekit anashindwa changisha watu huku mgonjwa yupo hospital mbona wanachangisha pesa za mlinzi mara sijui nin ,🙆🏼‍♂️🙆🏼‍♂️
Kibinadamu upo sahihi ila kiuharisia sio rahisi huko mtaani kila mtu yupo na shida ambayo inamtafuna na anahitaji pesa ya haraka 20, 30 n.k kusavaivu sio poa.
 
Inasikitisha sana ,huyo mume wake na yeye ameshindwa kabisa kujiongeza? Kwanini asingempeleka hospital kwanza wakapata matibabu then ndio akaanza kufany harambee kwa majirani kukusanya pesa? Muhara/Kutapika unaondoka fasta maana unapoteza maji kwa kiwangu kikubwa.
 
Nadhani ujanielewa jamaa, hio LAKI umeandika kiurahisi sana mtaani kuipata hio mtu kukupa sio rahisi Kama ulivyoandika jomba, mtaani kupata LAKI kwa watu wanaokopesha kwa riba tena unaweka asset Kama TV kubwa, LAPTOP yaani ulivyoandika sio rahisi hivyo
Mimi ninatoa mkuu tena zaidi ya hiyo kwenye uhitaji
 
Marehemu Happiness kasmiry kutoka kijiji cha Usari wilaya ya Moshi. Alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.

Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa la John alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.

Marehemu ameacha watoto watatu wadogo. Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
Wachaga wana tabia ngumu na ya ajabu sana. Ingekuwa harusi wangechanga ili mradi tu walewe. Sasa fuatilia maandalizi ya huo msiba. Hapo kuna Tshirt zitatengenezwa na kamati ya vinywaji. Huyo Mwenyekiti hana maana na.ni mjinga.
 
Watu wote walozunguka pale walishindwa msaidie aende hospital ,?mwenyekit anashindwa changisha watu huku mgonjwa yupo hospital mbona wanachangisha pesa za mlinzi mara sijui nin ,🙆🏼‍♂️🙆🏼‍♂️
Hivi nyie mmefanikiwa hata kuishi kijijini kweli, au ni story tu mnasikia? Upatikanaji wa pesa kijijini ni mdogo sana, ukisikia mtu fukara ni fukara kweli.
 
Tuanze leo basi kuwachangia waliokwama mahospitalini Kupata tiba.
Pale Muhimbili kanisa katoliki ukipeleka hata pampa's moja tu ya sh 500 inapokelewa ni sadaka tosha kwa ajili ya watoto wachanga wenye uhitaji, kuliko kuhonga malaya milioni Ili akupe UTI, na stress.
 
Inasikitisha sana ,huyo mume wake na yeye ameshindwa kabisa kujiongeza? Kwanini asingempeleka hospital kwanza wakapata matibabu then ndio akaanza kufany harambee kwa majirani kukusanya pesa? Muhara/Kutapika unaondoka fasta maana unapoteza maji kwa kiwangu kikubwa.
Kuna kauzembe
 
Watu Wana roho mbaya, majirani wote wameshindwa kumpa msaada hata wa laki akaanze matibabu, mpaka mtu anakufa
Siyo roho mbaya, kumbuka watu tungeweza kumchangia, ila kuna sherehe za ubatizo, komunio na Kipaimara na jarusi zitakuja na hela zilizopo ni kwa ajili ya sherehe hizo.

Ngoja tuangalie jinsi ya kuchangishana kwa ajili ya msiba. Hii ya ugonjwa ina kaugumu fulani, tunaomba mtusamehe.
 
Laanq zote hizi zitawarudia CCM na huyu Rais anayetesa wananchi kwa kuwasababishia unasikini na kuwaonhezea umasikini kwa tozo kupandisha bei za bidhaa juu na migao ya umeme maji n.k huku wao wakiendelea kulamba asali.One day
 
Back
Top Bottom