Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Mwanafunzi amekataa kudeki mwalimu ampige kisa mwanafunzi amekataa kudeki?.
Kwanini asichague mwengine adeki tusiwe wepesi kutetea walimu haohao ndio wanao wabaka watoto kwa kutumia njia kama hizo za udhalilishaji. Sijaunga mkono mzazi kumpiga mwalimu napinga mwalimu kumpiga mwanafunzi kwa kukataa kudeki.
 
Mambo ya kudeki mwanafunzi ana fundishwa kwao sio shule pale shule anakwenda kwa kufundishwa elimu tu.

Mfano wewe unapata ajira kazi yako ofisini halafu boss wako anakwambia kasafishe vyoo utaona yupo sawa?.
We sio mtanzania? Hivi hizi shule za serikali nani huwa anafanya usafi? Manake naona mnacomment kama hamuishi Tz.
 
Nadhani

Kuna hatua za kufuata huyu mzazi amekuja kishari sana...what if angemkuta mwalimu naye anajiweza si angemtandika vibaya sana
Hapa umesema kweli mimi sijaunga mkono mzazi kumpiga mwalimu pia mwalimu simuungi mkono kumpiga mwanafunzi kwa kosa la kudeki.
 
Walimu wenzake walikuwa wapi wasimsaidie?
 
Wewe jamaa hebu fikiri kwa umakini,kwa hiyo km huyo dogo amekataa kudeki basi Mwl.angetafuta mwingine adeki,sasa nikuulize swali hivi kama Ndio ilikuwa zamu yake ya kudeki je?,unataka kutengeneza matabaka kwa Wanafunzi?,Hivi huyo mwanafunzi ambaye angechaguliwa kudeki badala ya huyo aliyegoma hivi angejisikiaje?.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
We sio mtanzania? Hivi hizi shule za serikali nani huwa anafanya usafi? Manake naona mnacomment kama hamuishi Tz.
Yaani hata me namshangaa yaani mwalimu kweli akadeki darasa kweli? Au wenzetu hawajasoma Tanzania kwahiyo shule yenye madarasa 20 walimu 5 wajigawe vipi?
Kwahiyo mwalimu afundishe na kufanya usafi wote...
 
Kwa hiyo mnawauzisha watoto wetu visheti, mihogo, vitumbua na maandazi kwa kigezo cha self reliance kweli mnastahili kupigwa.
 
What if huyo mwingine naye akikataa? Kumbuka mtoto shuleni haji kusoma elimu ya darasani tu Kuna mengi ya kujifunza
 
Nilipokuwa shule ilitokea kama hivi nilikuwa naumwa na ilikuwa siku yangu ya usafi. Mwalimu alimchagua mwanafunzi mwengine afanye usafi. Halafu siku ya yule mwanafunzi nilifanya mimi na siku yangu kufika nilifanya tena. Kwanini huyu mwalimu hakutumia njia kama ya mwalimu wangu?.
 
Yaani hata me namshangaa yaani mwalimu kweli akadeki darasa kweli? Au wenzetu hawajasoma Tanzania kwahiyo shule yenye madarasa 20 walimu 5 wajigawe vipi?
Kwahiyo mwalimu afundishe na kufanya usafi wote...
Hata kama walimu wangekua mia jukumu la mwalimu ni kusimamia mwanafunzi kufanya usafi. Naona labda hapa tunajadili na wasio watz. Manake hizo mambo kwa shule zetu za kayumba ni kawaida kabisa.
 
What if huyo mwingine naye akikataa? Kumbuka mtoto shuleni haji kusoma elimu ya darasani tu Kuna mengi ya kujifunza
Soma hii comment yangu hapa 👆🏾mwalimu wangu alitumia hikma, kuwa mwalimu sio kama mkamilifu alitakiwa achague mwengine. Kama mwengine akikataa siku inayofata kutafanyika usafi au hio classroom’s ilikuwa inanuka?.
 
Usikute Wala sio fimbo moja.Wacha wapigwe maana walimu wamezidisha.
Walimu tena. Walimu, walimu, walimu, kila kukicha mwalimu amefanya lile, kisha kule amefanya lile.

Zuchu na mauno yake, walimu wakuu wakashushwa vyeo. Ile wamerudishwa tu, huyu kamchapa mtoto na yeye katolewa ngeu.

Tusubiri tuone matokeo. Walimu acheni mitoto ya watu ifanye inavyotaka.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Soma hii comment yangu hapa 👆🏾mwalimu wangu alitumia hikma, kuwa mwalimu sio kama mkamilifu alitakiwa achague mwengine. Kama mwengine akikataa siku inayofata kutafanyika usafi au hio classroom’s ilikuwa inanuka?.
Yaani mwanafunzi amgomee mwalimu halafu mwalimu achukue mwanafunzi mwingine?? Mkuu hebu think out of the box
Mtoto akugomee kufanya kazi badala uchukue hatua unamfata mtoto mwingine
 
Unamlinda saa ngapi ? Hopi watoto wenzake wakimpiga utaenda kumvamia huyo mtoto na mzazi wake ? Vipi zile tabia mbaya kama za kulswitiana, kubakwa nk unalinda saa ngapi.
Ngoja nikwambie bro, watoto wa shule za KAYUMBA hawapo salama, hata wale wa ST...tumesikia kesi za kuuwawa kubakwa nk.
Mtoto wako akibahatika kumaliza salama na kuhitimu ngazi zote ni bahati yako tu waka si juhudi zako za kumlinda.
Wazaxi tunaweza kuwalinda watoto zetu nyumbani.
Je huwa unamsindikiza mtoto wako na kumfuata muda wa kurudi ?
Je unafuatilia matukio yote yaliomtokea mtoto wako na kuchukua hatua kila siku.
Je unatembelea shuleni mara kwa mara kipata taarifa ya mwenendo wa mtoto wako.
Kama hautekelezi hayo basi unafurahisha genge tu hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…