Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Hata Mwalimu hakuajiriwa kudeki wala ToRs zake hakuna kudeki

after all hizo kazi za usafi zinafanywa na wanafunzi kwa hizi shule zetu za kidumu na ufagio tuliosoma huko hilo sio jambo geni.

Kama mwanafunzi alichapwa hakujeruhiwa wala hapakuwa na athari yoyote kiafya basi Mama achukue mwanae akamfundishie nyumbani maana huyo sio wa kwanza kuchapwa, tumechapwa sana tu huwezi kugomea mwalimu kisa umepewa kazi ya kudeki

Mama wa mtoto ajiulize yeye angemtuma mwanae adeki na mwanae akatae yeye kama Mama angefanya nini?
Mwanafunzi amekataa kudeki mwalimu ampige kisa mwanafunzi amekataa kudeki?.
Kwanini asichague mwengine adeki tusiwe wepesi kutetea walimu haohao ndio wanao wabaka watoto kwa kutumia njia kama hizo za udhalilishaji. Sijaunga mkono mzazi kumpiga mwalimu napinga mwalimu kumpiga mwanafunzi kwa kukataa kudeki.
 
Mambo ya kudeki mwanafunzi ana fundishwa kwao sio shule pale shule anakwenda kwa kufundishwa elimu tu.

Mfano wewe unapata ajira kazi yako ofisini halafu boss wako anakwambia kasafishe vyoo utaona yupo sawa?.
We sio mtanzania? Hivi hizi shule za serikali nani huwa anafanya usafi? Manake naona mnacomment kama hamuishi Tz.
 
Nadhani

Kuna hatua za kufuata huyu mzazi amekuja kishari sana...what if angemkuta mwalimu naye anajiweza si angemtandika vibaya sana
Hapa umesema kweli mimi sijaunga mkono mzazi kumpiga mwalimu pia mwalimu simuungi mkono kumpiga mwanafunzi kwa kosa la kudeki.
 
Hali ya taharuki imetokea katika shule ya msingi Narumu, katika Kijiji cha Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya mama mmoja ajulikanae kwa jina la Valentina kweka, kuingia ofisi ya walimu na kumpiga Mwalimu.

Mwalimu huyo ambaye ni wa kike (jina limehifadhiwa) alijeruhiwa hivyo Kupelekea kutoka damu puani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi huyo wa darasa la tano fimbo moja kwa kosa la kukataa kudeki darasa.

Mtoto huyo alienda kusema kwa mamake huku akilia ndipo mzazi huyo alipochukua jukumu la kwenda hadi shuleni na kumpiga mwalimu huyo na kumjeruhi.

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ismael Urassa pamoja na diwani wa kata hiyo wamethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limefika ofisi ya kata na linashughukiwa.
Walimu wenzake walikuwa wapi wasimsaidie?
 
Mwanafunzi amekataa kudeki mwalimu ampige kisa mwanafunzi amekataa kudeki?.
Kwanini asichague mwengine adeki tusiwe wepesi kutetea walimu haohao ndio wanao wabaka watoto kwa kutumia njia kama hizo za udhalilishaji. Sijaunga mkono mzazi kumpiga mwalimu napinga mwalimu kumpiga mwanafunzi kwa kukataa kudeki.
Wewe jamaa hebu fikiri kwa umakini,kwa hiyo km huyo dogo amekataa kudeki basi Mwl.angetafuta mwingine adeki,sasa nikuulize swali hivi kama Ndio ilikuwa zamu yake ya kudeki je?,unataka kutengeneza matabaka kwa Wanafunzi?,Hivi huyo mwanafunzi ambaye angechaguliwa kudeki badala ya huyo aliyegoma hivi angejisikiaje?.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
We sio mtanzania? Hivi hizi shule za serikali nani huwa anafanya usafi? Manake naona mnacomment kama hamuishi Tz.
Yaani hata me namshangaa yaani mwalimu kweli akadeki darasa kweli? Au wenzetu hawajasoma Tanzania kwahiyo shule yenye madarasa 20 walimu 5 wajigawe vipi?
Kwahiyo mwalimu afundishe na kufanya usafi wote...
 
It was all about self reliance lesson. Lini huyo mtoto atajua kufanya usafi wa mazingira anayo ishi Kama hamtaki afunzwe shuleni au nyumbani?
Fikiri kabla ya kuandikia.
Kama huyo mtoto haitaji kujua kujihudumia anataka kuhudumia basi aende private school wanakoweka janitor wa kuwafanyia usafi.

Serikali haina uwezo wa kuajiri wafanya usafi shule zote za umma. Siyo ajabu hiyo mzazi angeambiwa achangie gharama ya kumlipa janitor angalalamika elimu bure kwanini wanachangishwa michango.
Kwa hiyo mnawauzisha watoto wetu visheti, mihogo, vitumbua na maandazi kwa kigezo cha self reliance kweli mnastahili kupigwa.
 
Mwanafunzi amekataa kudeki mwalimu ampige kisa mwanafunzi amekataa kudeki?.
Kwanini asichague mwengine adeki tusiwe wepesi kutetea walimu haohao ndio wanao wabaka watoto kwa kutumia njia kama hizo za udhalilishaji. Sijaunga mkono mzazi kumpiga mwalimu napinga mwalimu kumpiga mwanafunzi kwa kukataa kudeki.
What if huyo mwingine naye akikataa? Kumbuka mtoto shuleni haji kusoma elimu ya darasani tu Kuna mengi ya kujifunza
 
Wewe jamaa hebu fikiri kwa umakini,kwa hiyo km huyo dogo amekataa kudeki basi Mwl.angetafuta mwingine adeki,sasa nikuulize swali hivi kama Ndio ilikuwa zamu yake ya kudeki je?,unataka kutengeneza matabaka kwa Wanafunzi?,Hivi huyo mwanafunzi ambaye angechaguliwa kudeki badala ya huyo aliyegoma hivi angejisikiaje?.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
Nilipokuwa shule ilitokea kama hivi nilikuwa naumwa na ilikuwa siku yangu ya usafi. Mwalimu alimchagua mwanafunzi mwengine afanye usafi. Halafu siku ya yule mwanafunzi nilifanya mimi na siku yangu kufika nilifanya tena. Kwanini huyu mwalimu hakutumia njia kama ya mwalimu wangu?.
 
Yaani hata me namshangaa yaani mwalimu kweli akadeki darasa kweli? Au wenzetu hawajasoma Tanzania kwahiyo shule yenye madarasa 20 walimu 5 wajigawe vipi?
Kwahiyo mwalimu afundishe na kufanya usafi wote...
Hata kama walimu wangekua mia jukumu la mwalimu ni kusimamia mwanafunzi kufanya usafi. Naona labda hapa tunajadili na wasio watz. Manake hizo mambo kwa shule zetu za kayumba ni kawaida kabisa.
 
What if huyo mwingine naye akikataa? Kumbuka mtoto shuleni haji kusoma elimu ya darasani tu Kuna mengi ya kujifunza
Nilipokuwa shule ilitokea kama hivi nilikuwa naumwa na ilikuwa siku yangu ya usafi. Mwalimu alimchagua mwanafunzi mwengine afanye usafi. Halafu siku ya yule mwanafunzi nilifanya mimi na siku yangu kufika nilifanya tena. Kwanini huyu mwalimu hakutumia njia kama ya mwalimu wangu?.
Soma hii comment yangu hapa 👆🏾mwalimu wangu alitumia hikma, kuwa mwalimu sio kama mkamilifu alitakiwa achague mwengine. Kama mwengine akikataa siku inayofata kutafanyika usafi au hio classroom’s ilikuwa inanuka?.
 
Usikute Wala sio fimbo moja.Wacha wapigwe maana walimu wamezidisha.
Walimu tena. Walimu, walimu, walimu, kila kukicha mwalimu amefanya lile, kisha kule amefanya lile.

Zuchu na mauno yake, walimu wakuu wakashushwa vyeo. Ile wamerudishwa tu, huyu kamchapa mtoto na yeye katolewa ngeu.

Tusubiri tuone matokeo. Walimu acheni mitoto ya watu ifanye inavyotaka.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Soma hii comment yangu hapa 👆🏾mwalimu wangu alitumia hikma, kuwa mwalimu sio kama mkamilifu alitakiwa achague mwengine. Kama mwengine akikataa siku inayofata kutafanyika usafi au hio classroom’s ilikuwa inanuka?.
Yaani mwanafunzi amgomee mwalimu halafu mwalimu achukue mwanafunzi mwingine?? Mkuu hebu think out of the box
Mtoto akugomee kufanya kazi badala uchukue hatua unamfata mtoto mwingine
 
Mwalimu mbona unamkingia sana kifuabmwalimu mwenzio? Yani kamchapa fimbo? Kweli mwalimu huu ndio ukweli?

Hata hivyo acha wazazi tulinde watoto wetu maana tunaona namna mnawashambulia wanetu huku mkiwarekodi na kutuonyesha mtandaoni.

Popote ulipo mzazi mlinde mwanao kwa gharama yoyote walimu wa leo vijanavijana hawa sio watu sahihi kwa usalama wa watoto wetu mambo yamebadilika sana.
Unamlinda saa ngapi ? Hopi watoto wenzake wakimpiga utaenda kumvamia huyo mtoto na mzazi wake ? Vipi zile tabia mbaya kama za kulswitiana, kubakwa nk unalinda saa ngapi.
Ngoja nikwambie bro, watoto wa shule za KAYUMBA hawapo salama, hata wale wa ST...tumesikia kesi za kuuwawa kubakwa nk.
Mtoto wako akibahatika kumaliza salama na kuhitimu ngazi zote ni bahati yako tu waka si juhudi zako za kumlinda.
Wazaxi tunaweza kuwalinda watoto zetu nyumbani.
Je huwa unamsindikiza mtoto wako na kumfuata muda wa kurudi ?
Je unafuatilia matukio yote yaliomtokea mtoto wako na kuchukua hatua kila siku.
Je unatembelea shuleni mara kwa mara kipata taarifa ya mwenendo wa mtoto wako.
Kama hautekelezi hayo basi unafurahisha genge tu hapa.
 
Back
Top Bottom