Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Una uhakika ni kweli alikataa kudeki akachapwa fimbo moja tu? Kabla ya kutoa laana upande mmoja hebu jiridhishe kidogo nini kilitokea.

Nakupa mfano mmoja mdogo, mtoto wa jirani yangu alikuwa mgonjwa wa pumu na alitakiwa asifanye kazi ngumu kwa muda aliokuwa anatumia dozi fulani na taarifa mzazi alipeleka shuleni.

Akaja mwalimu fulani mgeni akaintroduce program ya kukimbia asubuhi kama mazoezi, so kwakuwa yule dogo alikuwa ana kamwili fulani yule mwalimu akajua dogo mzembe tu na akamlazimisha akimbie ili apungue, mzazi alivyoskia vile bado kidogo aje ale kichwa cha yule mwalimu ndio waalimu wengine wakaomba msamaha.

Kumbuka mtoto hawezi kujieleza vizuri ni jukumu la mwalimu kumuelewa haraka kwanini hataki kazi fulani na kuchukua hatua stahiki ila sio kukimbilia kuchapa mtoto kama punda. Rudia tena kutoa comment kistaarabu
Hii inanikumbusha wakati tunasoma primary kuna mshkaji ilikuwa siku ya jumanne ambayo ni siku ya usafi walimu walikuwa wanamuacha tu na hata akifanya makosa alikuwa anaachwa tu kisa uelewa mdogo wa wazazi wake na mwisho alikuja kufukuzwa shule ya sekondari ya kiislamu pale mtwara kwasababu kule hakukuwa na baba yake kama ilivyokawa shule ya msingi
 
Angenikuta mimi hakika angejuta huyo mama ningemung'oa taya right away, wazazi wabadilike, shule zinaendeshwa kwa utaratibu na kufuata sheria za nchi, mimi kumchapa mtoto naruhusiwa baada ya kupewa idhini na mkuu wa shule, ambapo viboko visizidi vitatu kwa kila kosa.

Pili wazazi watambue kuwa shule ni sehemu salama kwa mtoto kujifunza mitaala ya ziada,mfano kulima,kufanya usafi na kumfanya mtoto ajue mazingira ya kujitegemea,sasa chukulia mtoto nyumbani kazi zote zinafanywa na house girl ,je yeye atajua lini haya majukumu!?

Kingine naona baadhi ya member wanaraumu mtoto kufanyishwa usafi hasa huyu member FaizaFoxy na Islam005 sasa kwa akili ya kawaida mwalimu ndo afanye usafi mazingira ya shule!? Shule zetu za serikali zinajulikana ni supana mkononi,kama hutaki mtoto afanyishwe kazi peleka shule za kulipia kama feza.
 
Wanaraumu
 
Fimbo moja?
Ila watu wa Narumu wanapenda sana ugomvi.

Miaka ya 90 kuna vijana nilikuta nao nikiwa ninaenda kusaga mahindi, wakanisimamisha wakanitupia njiti ya moto puani.

Wanarumu wanatafuta ugomvi haswa.

Halafu Bushmamy kichwa cha habari kinasomeka "Moshi" ila tukio limetokea "Hai". Hizi ni Wilaya mbili fotauti.

Moshi siyo Mkoa, bali Mkoa ni Kilimanjaro.
 
Hali ya taharuki imetokea katika shule ya msingi Narumu, katika Kijiji cha Narumu wilaya ya Hai, baada ya mama mmoja ajulikanae kwa jina la Valeria, kuingia ofisi ya walimu na kumpiga Mwalimu.

Mwalimu huyo ambaye ni wa kike (jina limehifadhiwa) alijeruhiwa hivyo Kupelekea kutoka damu puani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi huyo wa darasa la tano fimbo moja kwa kosa la kukataa kudeki darasa.

Mtoto huyo alienda kusema kwa mamake huku akilia ndipo mzazi huyo alipochukua jukumu la kwenda hadi shuleni na kumpiga mwalimu huyo na kumjeruhi.

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ismael Urassa pamoja na diwani wa kata hiyo wamethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limefika ofisi ya kata na linashughukiwa.
Jinai inashughulikiwa na Kata?

Wapumbavu wengi sana nchini
 
Back
Top Bottom