Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
πππππWalimu ni walezi wacha wawafundishe watoto malezi ikiwemo kazi za mikono,nyie wenzetu wawapi ambako hamfanyi kazi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
πππππWalimu ni walezi wacha wawafundishe watoto malezi ikiwemo kazi za mikono,nyie wenzetu wawapi ambako hamfanyi kazi.
ππππππNa katika hili unaweza kujifunza na kubaini mtu mwenye shule kiasi kichwani na asie na shule kichwani.
Moja anachochewa na mihemko, ghadhabu na hasira bila kutathmini wala kujua hatari na madhara mbeleni....
Mwingine anaamua kuchukua hatua kwa hekima na utulivu sana tena baada ya kutathmini kwa kina, madhara ya yanayoweza tokea huko mbeleni ikiwa ataamua vinginevyo...
Nadhani mzazi angemwendea kwa upole Mwalimu,yeye pamoja na mwanae wangesaidika vizuri zaidi kwenye suala la malezi.
Hata kama kijana alichapwa na kuumizwa bado ingekua faida kwake kwa siku za usoni, kuliko kumjengea mwanae ujasiri na kiburi dhidi ya anayoelekezwa na walimu na pengine jamii baadae..
Haitamsaidia...
Mjengee mwanao malezi na ujasiri wa kumsadia, sio kumbomoa na kupambana na wanaomzunguka, huo sio upendo katika malezi.
Unaona mialimu mlivyo miSiku moja nilitoa kichapo kwa mwanafunzi mmoja wa kike wa darasa la kike baada ya kukataa kunipikia chai asubuhi. Baada ya kumchapa viboko kadhaa kwa ubishi wake alikimbia nyumbani kwao kumleta baba yake. Mzazi alikuja amefura hasira mpaka nyumbani kwa walimu eneo la shule akakosa mwalimu yupi amshambulie kwa kuwa walimu tulichanganyikana huku wengine wakiwa ni watu wazima na wenye miili mikubwa iliyojazia. Mzazi alirudi nyumbani kwake huku akitoa ole wake huyo mwalimu aliyemchapa mtoto wake angepigana naye. Tangu siku hiyo niliona isiwe taabu kuwatumia wanafunzi kwenye shughuli zangu binafsi. Kuna mkuu mmoja wa shule ni wa kike alikuwa ni mbabe, mzazi akijitia kiherehere kwenda shuleni kuleta fujo alikuwa anamkwida na kumzabatua makofi na ngumi huku akimuambia anampeleka polisi. Wazazi wengine shuleni hawaji ila watatengeneza manuever kumkomoa mwalimu aliyechapa watoto wao. Mwalimu anaweza kujikuta katundikwa juu ya mti kalala huko usiku wote kimazingara. Wengine hufanyiwa vitendo vya kishirikina usiku
Na kuna Maweni pale TangaKarma is a bitch. Huyo mtoto Hana muda mrefu atakua mgeni wa serikali Kama sio kisongo Basi Ni karanga. Huko ndio kwa wenzake wanaoendana naye.
Wazazi wa aina hii wangekuwepo shule kama Loleza na nyinginezoHali ya taharuki imetokea katika shule ya msingi Narumu, katika Kijiji cha Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya mama mmoja ajulikanae kwa jina la Valentina kweka, kuingia ofisi ya walimu na kumpiga Mwalimu.
Mwalimu huyo ambaye ni wa kike (jina limehifadhiwa) alijeruhiwa hivyo Kupelekea kutoka damu puani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi huyo wa darasa la tano fimbo moja kwa kosa la kukataa kudeki darasa.
Mtoto huyo alienda kusema kwa mamake huku akilia ndipo mzazi huyo alipochukua jukumu la kwenda hadi shuleni na kumpiga mwalimu huyo na kumjeruhi.
Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ismael Urassa pamoja na diwani wa kata hiyo wamethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limefika ofisi ya kata na linashughukiwa.
Walimu wanaweza kukuulia mtoto hivihivi yaani fimbo moja wanatuona sisi mafala niniiHali ya taharuki imetokea katika shule ya msingi Narumu, katika Kijiji cha Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya mama mmoja ajulikanae kwa jina la Valentina kweka, kuingia ofisi ya walimu na kumpiga Mwalimu.
Mwalimu huyo ambaye ni wa kike (jina limehifadhiwa) alijeruhiwa hivyo Kupelekea kutoka damu puani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi huyo wa darasa la tano fimbo moja kwa kosa la kukataa kudeki darasa.
Mtoto huyo alienda kusema kwa mamake huku akilia ndipo mzazi huyo alipochukua jukumu la kwenda hadi shuleni na kumpiga mwalimu huyo na kumjeruhi.
Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ismael Urassa pamoja na diwani wa kata hiyo wamethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limefika ofisi ya kata na linashughukiwa.
Wazazi wa kileo hao kwenye moja na mbili.Usikute Wala sio fimbo moja.Wacha wapigwe maana walimu wamezidishaw
Tunakoelekea ni kubaya sanaAngenikuta mimi hakika angejuta huyo mama ningemung'oa taya right away, wazazi wabadilike, shule zinaendeshwa kwa utaratibu na kufuata sheria za nchi, mimi kumchapa mtoto naruhusiwa baada ya kupewa idhini na mkuu wa shule, ambapo viboko visizidi vitatu kwa kila kosa.
Pili wazazi watambue kuwa shule ni sehemu salama kwa mtoto kujifunza mitaala ya ziada,mfano kulima,kufanya usafi na kumfanya mtoto ajue mazingira ya kujitegemea,sasa chukulia mtoto nyumbani kazi zote zinafanywa na house girl ,je yeye atajua lini haya majukumu!?
Kingine naona baadhi ya member wanaraumu mtoto kufanyishwa usafi hasa huyu member FaizaFoxy na Islam005 sasa kwa akili ya kawaida mwalimu ndo afanye usafi mazingira ya shule!? Shule zetu za serikali zinajulikana ni supana mkononi,kama hutaki mtoto afanyishwe kazi peleka shule za kulipia kama feza.
Mtoto wa darasa la 5 asiweze kujieleza vizuri huyo kzazi alikurupuka angefika shuleni aulize kilichotokea.Una uhakika ni kweli alikataa kudeki akachapwa fimbo moja tu? Kabla ya kutoa laana upande mmoja hebu jiridhishe kidogo nini kilitokea.
Nakupa mfano mmoja mdogo, mtoto wa jirani yangu alikuwa mgonjwa wa pumu na alitakiwa asifanye kazi ngumu kwa muda aliokuwa anatumia dozi fulani na taarifa mzazi alipeleka shuleni.
Akaja mwalimu fulani mgeni akaintroduce program ya kukimbia asubuhi kama mazoezi, so kwakuwa yule dogo alikuwa ana kamwili fulani yule mwalimu akajua dogo mzembe tu na akamlazimisha akimbie ili apungue, mzazi alivyoskia vile bado kidogo aje ale kichwa cha yule mwalimu ndio waalimu wengine wakaomba msamaha.
Kumbuka mtoto hawezi kujieleza vizuri ni jukumu la mwalimu kumuelewa haraka kwanini hataki kazi fulani na kuchukua hatua stahiki ila sio kukimbilia kuchapa mtoto kama punda. Rudia tena kutoa comment kistaarabu
Wewe ndo una akili ya kitumwa.Inahusu nini mwanafunzi kudeki shule?
Bado tupo kijinga sana, akili za kitumwa.