Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Kumbe ulitaka Nani afanye usafi shuleni?
Kwa akili yako iliyochoka unataka walimu wanaolipwa $200 wakadeki vyoo vya wanafunzi?
Wake up young lady .
Sijui tunawafundisha Nini watoto wetu wa kizazi Cha sasa, kudeki na kazi mbalimbali Mtoto awapo shuleni ni jambo la kawaida . Sasa wanaosema walimu wafanye usafi wa kudeki na kusafisha vyoo vya wanafunzi kweli ni sahihi? Kama wazazi wamefika mahali hawataki watoto wafanye kazi shuleni waajiri wafanyakazi wa kudeki madarasa ya watoto wao Kwa kuhakikisha wanawalipa.
 
Vizuri sana ilibidi huyo Mwalimu angepokea kipigo Cha kulazwa ICU ili liwe funzo. Hapo usikute mtoto alipigwa na makofi kabisa ndio mzazi akaamua kwenda kumtoa damu huyo mjinga.

Walimu jifunzeni busara, wazazi wamechafukwa Sasa na watoto wanapatikana Kwa shida sana, Kwa Sasa sio Kila mwanamke au mwanamme anaweza kuzaa au kuzalisha na unakuta mtoto kapatikana Kwa mitishamba na shida kibao halafu linatokea jinga linampiga ovyo aisee mtakuja kuuliwa maofisini
 
Sio tu Ni mpuuzi, huyo mwanamke Ni punguwani au ana mtindio wa ubongo.

Anataka walimu wafanye usafi wanafunzi wafanye nini? Kule kwao Mbagala huyu FaizaFoxy shule Zina watoto elfu nne walimu sabini au themanini, shule haina mfanyakazi zaidi ya mlinzi na walimu.

Kumbe kweli Kuna watu wanafikiria kutumia matako. Nimeamini leo
Huenda hazimtoshi ama huyo mzazi na mwalimu ni majirani hivyo wana bifu za kitaani kwao.
Alipaswa kufahamu kwa undani ni kwa nini mtoto wake kaadhibiwa na ni kwa kiasi gani kaadhibiwa.
 
Hali ya taharuki imetokea katika shule ya msingi Narumu, katika Kijiji cha Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya mama mmoja ajulikanae kwa jina la Valentina kweka, kuingia ofisi ya walimu na kumpiga Mwalimu.

Mwalimu huyo ambaye ni wa kike (jina limehifadhiwa) alijeruhiwa hivyo Kupelekea kutoka damu puani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi huyo wa darasa la tano fimbo moja kwa kosa la kukataa kudeki darasa.

Mtoto huyo alienda kusema kwa mamake huku akilia ndipo mzazi huyo alipochukua jukumu la kwenda hadi shuleni na kumpiga mwalimu huyo na kumjeruhi.

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ismael Urassa pamoja na diwani wa kata hiyo wamethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limefika ofisi ya kata na linashughukiwa.
Huyu mama achekiwe afya ya akili!Hilo tuu!
 
Mzazi amekosea sana! Kama Mwalimu alifuata taratibu zote za kumuadhibu mtoto, hakukosea!
Kizazi chetu tunazalisha watoto wenye kiburi wasio na heshima kwa sababu wazazi wa nyakati hizi wanalea watoto kama mayai.

Niseme tu ikithibitika kuwa Mwalimu alimpa adhabu mtoto kwa kufuata utaratibu mama afikishwe kwenye vyombo vya Sheria.
 
Inahusu nini mwanafunzi kudeki shule?

Bado tupo kijinga sana, akili za kitumwa.
Hata wewe una-support upumbavu? Hujui kama shule watoto wanapaswa wajifunze kila kitu kasoro tabia mbaya?

Hiyo ni moja wapo wa stadi za maisha,kama mtoto hakufundishwa umuhimu wa kufanya usafi eneo analoishi au analosomea basi tutegemee kesho chumba chake kuota majani.
 
Back
Top Bottom