Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Angenikuta mimi hakika angejuta huyo mama ningemung'oa taya right away, wazazi wabadilike, shule zinaendeshwa kwa utaratibu na kufuata sheria za nchi, mimi kumchapa mtoto naruhusiwa baada ya kupewa idhini na mkuu wa shule, ambapo viboko visizidi vitatu kwa kila kosa.


Pili wazazi watambue kuwa shule ni sehemu salama kwa mtoto kujifunza mitaala ya ziada,mfano kulima,kufanya usafi na kumfanya mtoto ajue mazingira ya kujitegemea,sasa chukulia mtoto nyumbani kazi zote zinafanywa na house girl ,je yeye atajua lini haya majukumu!?

Kingine naona baadhi ya member wanaraumu mtoto kufanyishwa usafi hasa huyu member FaizaFoxy na Islam005 sasa kwa akili ya kawaida mwalimu ndo afanye usafi mazingira ya shule!? Shule zetu za serikali zinajulikana ni supana mkononi,kama hutaki mtoto afanyishwe kazi peleka shule za kulipia kama feza.
Ni vizr hili la walimu wafanye usafi lifanyike Ni Kweli wanalipwa na serekali
 
Ni vizr hili la walimu wafanye usafi lifanyike Ni Kweli wanalipwa na serekali
Mkuu mwalimu ameajiliwa kufundisha na kusimamia,sio kufanya kazi za shuleni ,yaani mwalimu adeki madarasa na asafishe vyoo vya wanafunzi!? Mbona Tanzania ni pana sana ukiona mwanao hawezi fanya haya peleka shule za kulipia,ambako mtoto wako atafuliwa hadi chupi
 
Mwalimu mbona unamkingia sana kifuabmwalimu mwenzio? Yani kamchapa fimbo? Kweli mwalimu huu ndio ukweli?

Hata hivyo acha wazazi tulinde watoto wetu maana tunaona namna mnawashambulia wanetu huku mkiwarekodi na kutuonyesha mtandaoni.

Popote ulipo mzazi mlinde mwanao kwa gharama yoyote walimu wa leo vijanavijana hawa sio watu sahihi kwa usalama wa watoto wetu mambo yamebadilika sana.
Mimi nimesoma msingi 80s mwishoni na 90s mwanzoni kipindi changu watoto tulikuwa watukutu kweli kweli(mara zote watoto ni watukutu hata wa sasa) lakini tulinyooshwa kwa ushirikiano wa wazazi na walimu.

Leo wazazi hatutaki wanetu wafunzwe adabu kwa viboko mashuleni tukitegemea tutawaadabisha wenyewe so wanakuwa na nidhamu ya kinafiki nyumbani huku mtaani hawafai kwa tabia chafu zisizoelezeka,watoto walindwe kwa matukio kama ubakaji na ulawiti mengine yote walimu wapo sahihi hakuna mtoto anayejifunza bila kuelekezwa kwa msisitizo wa viboko
 
Kayumba ni sawa
hata huko private sideki aisee! Eti nimeajiriwa private nafundisha wanafunzi na kudeki nideki! Bora nikakifungie cheti changu cha ualimu sandukuni niingie mtaani kusaka mafanikio kwa nguvu na akili zangu za asili kuliko fedheha ya kulipwa mshahara dhalili, ujinga huo niliukataa
 
Hali ya taharuki imetokea katika shule ya msingi Narumu, katika Kijiji cha Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya mama mmoja ajulikanae kwa jina la Valentina kweka, kuingia ofisi ya walimu na kumpiga Mwalimu.

Mwalimu huyo ambaye ni wa kike (jina limehifadhiwa) alijeruhiwa hivyo Kupelekea kutoka damu puani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi huyo wa darasa la tano fimbo moja kwa kosa la kukataa kudeki darasa.

Mtoto huyo alienda kusema kwa mamake huku akilia ndipo mzazi huyo alipochukua jukumu la kwenda hadi shuleni na kumpiga mwalimu huyo na kumjeruhi.

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ismael Urassa pamoja na diwani wa kata hiyo wamethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limefika ofisi ya kata na linashughukiwa.
Acheni kupiga watoto wa watu la sivyo mtapigwa sana

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Vizuri sana ilibidi huyo Mwalimu angepokea kipigo Cha kulazwa ICU ili liwe funzo. Hapo usikute mtoto alipigwa na makofi kabisa ndio mzazi akaamua kwenda kumtoa damu huyo mjinga.

Walimu jifunzeni busara, wazazi wamechafukwa Sasa na watoto wanapatikana Kwa shida sana, Kwa Sasa sio Kila mwanamke au mwanamme anaweza kuzaa au kuzalisha na unakuta mtoto kapatikana Kwa mitishamba na shida kibao halafu linatokea jinga linampiga ovyo aisee mtakuja kuuliwa maofisini
Mie siwatetei watoto watovu wa nizamu, lkn adhabu za walimu lzm ziendane na umri wa mtoto na ziwe na kipimo. Kuna walimu wengine ni washenzi sana! Unamtandika mtoto mpaka anashindwa kutembea. Hasira za maisha Yao magumu wanamalizia kwa watoto. Adhabu ni muhimu lkn ziwe na kipimo
 
Unaona mialimu mlivyo mi
jinga!!! Unamlazimisha mtoto akupikie chai amekua mke wako huyo??? Shenzi kabisa!
Alafu unajisifu eti nilitia kichapo!
Walimu kama nyie Mimi ndo nawataka sasa
nilikuta kuna utaratibu wa kupikiwa chai na msosi wa mchana na wanafunzi wa kike wale wakubwawakubwa. Mbona ni kawaida sana wanafunzi kupikia chai walimu staff? Ila chai yangu ilikuwa ya nyumbani sio ya ofisini. We usingeniweza ningekubamiza mbali. Fahamu kuwa sie walimu wengine tunajua dhahma na tafrani zinazoweza kutokea shuleni muda wowote ikiwemo sisi kwa sisi kunyukana. Kwa hiyo muda wote tuko on alert ku deal na kitu chochote cha shari kitakochotokea
 
Wazazi wa aina hii wangekuwepo shule kama Loleza na nyinginezo
Walimu wangekuwa wamenyooka maana wanatesa mno watoto wa watu kwa fimbo kali mno na adhabu zinazokiuka haki za binadamu.
Walimu wengi Wana ujinga ujinga sana! Bahati nzuri mie nimewahi kuishi kwenye kota za shule hivyo nawajua vzr walivyo wakatiri na waonezi. kosa ambalo angeweza kumuelekeza mtoto bila bakora lkn yeye atampiga mifimbo ya hovyo hovyo bila kuzingatia umri ama afya ya mtoto
 
Kumbe ulitaka Nani afanye usafi shuleni?
Kwa akili yako iliyochoka unataka walimu wanaolipwa $200 wakadeki vyoo vya wanafunzi?
Wake up young lady .
Fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali kila mwezi ndizo zinatakiwa zifanye shughuli kama hizo za usafi kwa kuajiri watu hata wawili tu kusafisha vyoo vya shule.

Hivi mtoto ana umakini gani wa kudeki choo cha shule kama sio kumtafutia magonjwa ya kuambukiza?
 
Mzazi amekosea sana! Kama Mwalimu alifuata taratibu zote za kumuadhibu mtoto, hakukosea!
Kizazi chetu tunazalisha watoto wenye kiburi wasio na heshima kwa sababu wazazi wa nyakati hizi wanalea watoto kama mayai.
Niseme tu ikithibitika kuwa Mwalimu alimpa adhabu mtoto kwa kufuata utaratibu mama afikishwe kwenye vyombo vya Sheria.
Hii ni 2023 mkuu na sio 1993

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Alimkuta mzembemzembe....tungegawana majengo au tungeenda jengo moja
Huwa unafuata utaratibu wa utoaji adhabu kwa mujibu wa wataka wa elimu na adhabu mashuleni?

Au na wewe ni miongoni mwa walimu vilaza wasiojua hata job description zao bali kutumia mabavu tu kuonea vitoto visivyoweza kujitetea?

Mimi nilishatoa onyo kwa mwalimu mkuu endapo mwanangu ataadhibiwa adhabu za kipumbavu zisizofuata utaratibu kamili basi hicho kibarua chake kitaishia siku hiyo.
 
Huyo mzazi bila shaka amezaliwa 94 kuendelea mbona sisi tulikua tunachapwa sana tukienda kusema nyumbani tunachapwa tena
We huoni Kuna shida upo nayo mahara?? Hapo ulipo mtu mzima lkn huna confidence ya kusimama mbele za watu kueleza jambo lolote ukaeleweka, unafiki imekujaa huna uwezo wa kupinga jambo lolote la mkubwa wako, unaogopa hata kukosoa, Kila kitu kwako ni ndio hata kama moyoni unajua hiki sio sahihi.

Kizazi chako ndicho hichi Cha viongozi wetu wa ndioooooooo!!!!
 
Fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali kila mwezi ndizo zinatakiwa zifanye shughuli kama hizo za usafi kwa kuajiri watu hata wawili tu kusafisha vyoo vya shule.

Hivi mtoto ana umakini gani wa kudeki choo cha shule kama sio kumtafutia magonjwa ya kuambukiza?
Pale Sangu secondary,wameajiri watu wa usafi na wanafanya usafi Mazingira yote ya nje pamoja na vyoo.

Usafi darasani wanafanya wanafunzi...
Watu wa hostel walikuwa wanadeki weekend...katikati ya wiki watu wa day mnafanya..na sanasana ilikuwa kuokota karatasi tu kama zipo.


Njoo sasa shule zetu za serikali..
Mtoto anafanya usafi kuanzia hostel anakolala,,mazingira ya nje ya hostel,vyooni hostel,jikoni hostel,dining za hostel na upande wa madarasani mtoto adeki darasa,adeki ofisi za walimu,adeki chooni,bado ana eneo la kufagia kuuubwaa na kila siku lifagiliwe,
Kuna kazi za kufyeka vichaka,
Hapo bado ana tuta la mboga linamsubiri akamwagilie.


Binafsi simuungi mkono mwanafunzi kumgomea Mwalimu lakini kazi za usafi ziwe na kiasi.
Watoto wasifanyishwe kama punda.

Pia walimu wapunguze vipigo...
Sidhani kama mzazi anaweza kumvamia Mwalimu na kumpa kipigo kama ingekuwa mtoto ameadhibiwa kistaarabu kwa fimbo moja.
Walimu wanapiga mno watoto na adhabu kali mno.
 
Mimi nimesoma msingi 80s mwishoni na 90s mwanzoni kipindi changu watoto tulikuwa watukutu kweli kweli(mara zote watoto ni watukutu hata wa sasa) lakini tulinyooshwa kwa ushirikiano wa wazazi na walimu.

Leo wazazi hatutaki wanetu wafunzwe adabu kwa viboko mashuleni tukitegemea tutawaadabisha wenyewe so wanakuwa na nidhamu ya kinafiki nyumbani huku mtaani hawafai kwa tabia chafu zisizoelezeka,watoto walindwe kwa matukio kama ubakaji na ulawiti mengine yote walimu wapo sahihi hakuna mtoto anayejifunza bili kuelekezwa kwa msisitizo wa viboko
Chief hii ni 2023 na sio 1990 mambo yamebadilika!

Zamani mtoto akikosea anaadhibiwa na mtu yoyote mtaani leo hebu jaribu kumchapa mtoto wa watu uone balaa lake!



Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom