Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Inahusu nini mwanafunzi kudeki shule?

Bado tupo kijinga sana, akili za kitumwa.

Bila shaka unaishi Ulaya sio Tanzania na pengine hujasoma hizi shule zetu.

Kazi za usafi kwenye shule za Umma hufanywa na wanafunzi, nadhani huko private schools ndo watakuwa na wafanya usafi walioajiriwa.

Inashangaza sana watu wanakomenti kumshambulia mwalimu kama vile wanaishi nje ya Nchi [emoji15][emoji15]
 
Hata Mwalimu hakuajiriwa kudeki wala ToRs zake hakuna kudeki

after all hizo kazi za usafi zinafanywa na wanafunzi kwa hizi shule zetu za kidumu na ufagio tuliosoma huko hilo sio jambo geni.

Kama mwanafunzi alichapwa hakujeruhiwa wala hapakuwa na athari yoyote kiafya basi Mama achukue mwanae akamfundishie nyumbani maana huyo sio wa kwanza kuchapwa, tumechapwa sana tu huwezi kugomea mwalimu kisa umepewa kazi ya kudeki

Mama wa mtoto ajiulize yeye angemtuma mwanae adeki na mwanae akatae yeye kama Mama angefanya nini?
Kuchapa hapana. Angechukuwa hatua nyingine ikiwa na pamoja na kuwasiliana na wazazi wake. Hii karne siyo ya kuchapa watoto. Kuna adhabu nyingi tu zinazoweza kutumika na siyo fimbo.
 
Bila shaka unaishi Ulaya sio Tanzania na pengine hujasoma hizi shule zetu.

Kazi za usafi kwenye shule za Umma hufanywa na wanafunzi, nadhani huko private schools ndo watakuwa na wafanya usafi walioajiriwa.

Inashangaza sana watu wanakomenti kumshambulia mwalimu kama vile wanaishi nje ya Nchi [emoji15][emoji15]
Ni kweli lakini inatakiwa hali ibadilike. Kuna shuleni nyingine wanafunzi wanakuwa kama wako gerezani kwa kufanyishwa kazi.
 
hamna mwalimu anachapa fimbo moja, lakini kizazi kinachokuja kitakuwa cha hatari..mimi nawashangaa walimu,mimi ningekuwa mwalimu naingia nafundisha nasepa,hizo shobo na wanafunzi nisingekuwa nazo..

huwa namwambiaga ndugu yangu mmoja bado miaka kadhaa astaafu aachane na kuchapa chapa wanafunzi hawamsaidii chochote,aachane nao ulimwengu utawafundisha maisha.
 
Hivi hawa wazazi walikuwa wapi Enzi zile tunapigwa kama mipira 🤣
Usipodeki unachapwa
Usipoleta kidumu unachapwa
Usipomwagilia maua unachapwa
Usipofanya hesabu unachapwa ukifanya ukakosa unachapwa
Ukirudi nyumbani mchafu unachapwa
Yaani kwa siku kuondoka shule na fimbo 20 ilikuwa kawaida sana...kwani siku hizi Kuna nini??
 
Lkn mwalimu kufanya kazi ya usafi wakati mwanafunzi yupo hiyo naona sio sawa! Tutakua hatujawatendea haki walimu wetu, kikubwa ninachokiona kazi ziwe na kipimo, kazi ziwe za kumfundisha/kumjenga mtoto na sio kumkomoa.

Mimi ninachokipinga ni adhabu za kiuonezi na kikatiri kwa watoto wadogo zinazotolewa na walimu wasiojua maadili ya kazi zao
Ndiyo maana tunakuwa na viongozi wasio jua kuwajibika ...kiongozi ni lazima utangulie mbele daima kuonyesha njia ...walimu wanatakiwa wao wawe kielelezo siyo kukaa nyuma kama mamwinyi
 
Mwalimu hajasomea kudeki amesomea kufundisha wanafunzi yaani transfer of knowledge. Achaga daharau kabisa . Kwa Tanzania wanafunzi ndio hudeki madarasa.
Mambo ya kudeki mwanafunzi ana fundishwa kwao sio shule pale shule anakwenda kwa kufundishwa elimu tu.

Mfano wewe unapata ajira kazi yako ofisini halafu boss wako anakwambia kasafishe vyoo utaona yupo sawa?.
 
Hivi hawa wazazi walikuwa wapi Enzi zile tunapigwa kama mipira 🤣
Usipodeki unachapwa
Usipoleta kidumu unachapwa
Usipomwagilia maua unachapwa
Usipofanya hesabu unachapwa ukifanya ukakosa unachapwa
Ukirudi nyumbani mchafu unachapwa
Yaani kwa siku kuondoka shule na fimbo 20 ilikuwa kawaida sana...kwani siku hizi Kuna nini??
Hao wazazi washakuwa ndio waliopitia huo unyanyasaji sasa hawataki kizazi chao kinyanyasike kama wao. Mbona kwa wenzetu hakuna haya na ndio wanaongoza kwa kuvumbua vitu duniani. Wakati sisi tunaokula mboko shuleni hatuna tulicho vumbua.
 
Kwani walimu ni nani mbona wazazi majumbani wanafanya kazi za usafi ...walimu wa kike wadeki wakiume wakate michongoma na kuchimba shimo za taka
Umesahau na kufagia na kudeki vyoo tena wasugue ving'ae.
 
Nadhani
Hao wazazi washakuwa ndio waliopitia huo unyanyasaji sasa hawataki kizazi chao kinyanyasike kama wao. Mbona kwa wenzetu hakuna haya na ndio wanaongoza kwa kuvumbua vitu duniani. Wakati sisi tunaokula mboko shuleni hatuna tulicho vumbua.
Kuna hatua za kufuata huyu mzazi amekuja kishari sana...what if angemkuta mwalimu naye anajiweza si angemtandika vibaya sana
 
Alaf asichokijua ni kua taaluma ni sehemu tu ya akipatacho mtoto awapo shulen

Kuna kitu kinaitwa MALEZI ni kipana xn apa ndipo kinapoandaliwa kizazi kijacho chenye maadili au laaah kwaiyo wazazi muwe wawazi mnahtaji walimu wawaandalie kizazi cha aina gan

Naamin walimu ni waelewa sana ukiachilia mbali changamoto za kika, walizonazo
 
Back
Top Bottom