Nimewaki kufika Moshi mara kadhaa, na ukweli wangu ni huu.
1. Ndio mji pekee hapa Tanzania niliowahi kuona watu wakichota maji bombani na kuyanywa moja kwa moja bila hata kuchemcha na mamlaka za maji na afya zinatoa muongozo huo kwa uhakika wa 100% kuwa maji ya moshi ni safi na salama. (Kwangu mimi hii ni ishara ya Usafi na ustaarabu wa kutunza mazingira).
2. Ni mji mdogo sana lakini uliojipanga vizuri kwa kiasi. Hakuna watu wengi sana na hakuna purukushani nyingi za kibiashara.
3. Ni mji msafi na salama zaidi huenda kuliko mji wowote hapa Tanzania. Kwa sehemu kubwa nyakati za usiku huwezi kukutana na giza, maana kuna taa nyingi za barabarani, taa kutokea kwenye nyumba za watu binafsi na taasisi. Kuna hadi CCTV camera zimefungwa maeneo ya katikati ya mji. Uwepo wa chuo cha polisi (Police Academy) huenda kumezaa tabia za waru kujari mambo ya usalama.
4. Ni mji wenye joto kali nyakati fulani fulani kupita hata joto la Dar, kuwepo karibu na mlima Kilimanjaro hakujapunguza joto kabisa. Labda ni matokeo ya uharibifu wa mazingira kuzunguka mlima Kilimanjaro.
5. Moshi ina stendi ndogo ya kizamani ya mabasi ya mikoani. Ni stendi ya kishamba mnoo. Ni stendi iliyopo katikati ya mji, haina ofisi za wakatisha tiketi, sehemu ya abiria kungojea usafiri imejazwa meza za wakatisha tiketi na kila biashara imeshindiliwa hapo hapo stendi. Na ikifika saa nne usiku inafungwa! Ni miongoni mwa stendi mbovu zaidi za mabasi ya mikoani (labda inaizidi stendi ya Arusha na Manyara (Babati) maana nazo ni stendi za ovyo ovyo mnoo)