Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Soon Ngangamfumuni itaanza Kazi mkuu.Nimewahi kufika Moshi mara kadhaa, na ukweli wangu ni huu.
1. Ndio mji pekee hapa Tanzania niliowahi kuona watu wakichota maji bombani na kuyanywa moja kwa moja bila hata kuchemcha na mamlaka za maji na afya zinatoa muongozo huo kwa uhakika wa 100% kuwa maji ya moshi ni safi na salama. (Kwangu mimi hii ni ishara ya Usafi na ustaarabu wa kutunza mazingira).
2. Ni mji mdogo sana lakini uliojipanga vizuri kwa kiasi. Hakuna watu wengi sana na hakuna purukushani nyingi za kibiashara. Kiujumla ni mji wa kimaendeleo kuanzia mifumo ya maji safi na maji taka, barabara, hospitali, shule,vyuo nk.
3. Ni mji msafi na salama zaidi huenda kuliko mji wowote hapa Tanzania. Kwa sehemu kubwa nyakati za usiku huwezi kukutana na giza, maana kuna taa nyingi za barabarani, taa kutokea kwenye nyumba za watu binafsi na taasisi. Kuna hadi CCTV camera zimefungwa maeneo ya katikati ya mji. Uwepo wa chuo cha polisi (Police Academy) huenda kumezaa tabia za watu wake kujari mambo ya usalama.
4. Ni mji wenye joto kali nyakati fulani fulani kupita hata joto la Dar, kuwepo karibu na mlima Kilimanjaro hakujapunguza joto kabisa. Labda ni matokeo ya uharibifu wa mazingira kuzunguka mlima Kilimanjaro.
5. Moshi ina stendi ndogo ya kizamani ya mabasi ya mikoani. Ni stendi ya kishamba mnoo. Ni stendi iliyopo katikati ya mji, haina ofisi za wakatisha tiketi, sehemu ya abiria kungojea usafiri imejazwa meza za wakatisha tiketi na kila biashara imeshindiliwa hapo hapo stendi. Na ikifika saa nne usiku inafungwa! Ni miongoni mwa stendi mbovu zaidi za mabasi ya mikoani (labda inaizidi stendi ya Arusha na Manyara (Babati) maana nazo ni stendi za ovyo ovyo mnoo)
Moshi imetoka wap hapa?Bukoba imetoka wap hapa[emoji848]
Nakuuliza CBD ya kahama iko wapi? Niwekee picha
Nasubiri mwanza na dar wazilinganishe na kijiji cha moshiBukoba imetoka wap hapa[emoji848]
Unapolinganisha maeneo ni muhimu kuweka vigezo na sio kuja na hitimisho la kiujumla.Nasubiri mwanza na dar wazilinganishe na kijiji cha moshi
Yan december ndo mgeni akienda kule ataona utofauti.Watu wanafikiri Moshi vijijini ni porini kwa sababu ya migomba na miti mingi, bila kujua kwamba maeneo mengi ya Kilimanjaro vijijini ni RUR-URBS, yaani rural-urban au semi-urban.
Binafsi halmashauri ya manispaa ya Kahama ipo juu kimaendelea kuliko moshi.Unapolinganisha maeneo ni muhimu kuweka vigezo na sio kuja na hitimisho la kiujumla.
Kwangu mimi mpaka kesho, kwa hapa Tz, Moshi is best town linakuja suala la Usafi, Ustaarabu na Usalama.
Embu ulizie robo heka ni shilingi ngapi?Ni Manispaa ya ajabu sana ukitembea mita 500 kutoka katikati ya mji unakutana na mashamba ya mahindi. Nyumba zimechanganyikana na mashamba
Iendelee tu kuwa Manispaa haifai kuwa jiji inapitwa mpaka na Kahama
Sawa. Niwekee picha yake ya hapo Kahama. IdiotCbd kirefu chake Cannabidiol,,,Cannabidiol unajua ni nini?
Sema unatafuta tu kick huna loloteMoshi ni mji wa ovyo over
Hiyo picha hapo ni jiji kuu la nchi ya Nepal [emoji1178], ambayo inapakana na India... Linaitwa Kathmandu.. Unaona hayo mashamba ya mpunga?? Na pembeni mwake kuna magorofa, acha kukariri jombaa.Ni Manispaa ya ajabu sana ukitembea mita 500 kutoka katikati ya mji unakutana na mashamba ya mahindi. Nyumba zimechanganyikana na mashamba
Iendelee tu kuwa Manispaa haifai kuwa jiji inapitwa mpaka na Kahama
Sawa. Niwekee picha yake ya hapo Kahama. Idiot
Alisikika Msukuma mmoja akitema Nyongo[emoji23]Aliekuambia mahindi yanafanya kutokuwa jiji ni nani..?? Hii mind set ya mji kuwa jangwa ifike mahali ife mimea inafaida kushinda hata hayo majiji mnayokimbilia!.
Kwa vigezo gani?Tanzania hii Dar es Salaam, Mwanza na Arusha ndio kunafaa kuwa majiji.
Hiyo picha hapo ni jiji kuu la nchi ya Nepal [emoji1178], ambayo inapakana na India... Linaitwa Kathmandu.. Unaona hayo mashamba ya mpunga?? Na pembeni mwake kuna magorofa, acha kukariri jombaa. View attachment 2218381
ngoja waje watakushukia kama mwewe.Ni Manispaa ya ajabu sana ukitembea mita 500 kutoka katikati ya mji unakutana na mashamba ya mahindi. Nyumba zimechanganyikana na mashamba
Iendelee tu kuwa Manispaa haifai kuwa jiji inapitwa mpaka na Kahama