Kwangu mimi, stendi ya kisasa iwe na sifa hizi.
1. Uwezo wa kumudu idadi kubwa ya mabasi ya mikoani kwa mara moja (Kwa stendi ya moshi hapana, upande wa kulia wameweka stendi ya coaster za Arusha, noah za Rombo na upande wa kushoto ndio rasmi kwa mabasi ya mikoani(masafa) lakini bado utakutana na coaster na Hiace za kwenda Kibosho, Mwanga. Ni fujo tupu.
2. Sehemu ya abiria pumzika kwa nafasi, uhuru na usalama. (Kwa stendi ya moshi hakuna)
3. Ofisi rasmi za makampuni ya mabasi (kwa stendi ya moshi hakuna)
4. Huduma za vyoo vya kisasa na mabafu (huduma ya vyoo ipo lakini sio vya kisasa au unadhifu)
Kuhusu Moshi kujenga stendi mpya ya kisasa (sijui maeneo ya majengo? Nami najua majengo ni maeneo ya karibu na katikati ya mji) hilo nalo ni hadithi ya miaka mingi mnoo, huenda ni jambo lisiloweza kutekelezeka, nilipofika 2010 niliambiwa hivyo, 2014 nikaambiwa hivyo, 2018 hadithi ni hiyo hiyo, November 2021 hadithi ni hiyo hiyo. Nilipochunguza nikagundua kuwa, kumbe ile stendi ya sasa ni kitega uchumi cha wajanja wa manispaa na madiwani wa CCM, wanavuta pesa nzuri kila mwezi kwa watu waliopangisha, siku stendi mpya ikijengwa tu na ulaji wao utakuwa umekwisha, na hawako tayari kwa hilo.