Moshi ndio Manispaa ya ovyo kushinda zote Afrika Mashariki

Moshi ndio Manispaa ya ovyo kushinda zote Afrika Mashariki

Nimewahi kufika Moshi mara kadhaa, na ukweli wangu ni huu.
1. Ndio mji pekee hapa Tanzania niliowahi kuona watu wakichota maji bombani na kuyanywa moja kwa moja bila hata kuchemcha na mamlaka za maji na afya zinatoa muongozo huo kwa uhakika wa 100% kuwa maji ya moshi ni safi na salama. (Kwangu mimi hii ni ishara ya Usafi na ustaarabu wa kutunza mazingira).

2. Ni mji mdogo sana lakini uliojipanga vizuri kwa kiasi. Hakuna watu wengi sana na hakuna purukushani nyingi za kibiashara. Kiujumla ni mji wa kimaendeleo kuanzia mifumo ya maji safi na maji taka, barabara, hospitali, shule,vyuo nk.

3. Ni mji msafi na salama zaidi huenda kuliko mji wowote hapa Tanzania. Kwa sehemu kubwa nyakati za usiku huwezi kukutana na giza, maana kuna taa nyingi za barabarani, taa kutokea kwenye nyumba za watu binafsi na taasisi. Kuna hadi CCTV camera zimefungwa maeneo ya katikati ya mji. Uwepo wa chuo cha polisi (Police Academy) huenda kumezaa tabia za watu wake kujari mambo ya usalama.

4. Ni mji wenye joto kali nyakati fulani fulani kupita hata joto la Dar, kuwepo karibu na mlima Kilimanjaro hakujapunguza joto kabisa. Labda ni matokeo ya uharibifu wa mazingira kuzunguka mlima Kilimanjaro.

5. Moshi ina stendi ndogo ya kizamani ya mabasi ya mikoani. Ni stendi ya kishamba mnoo. Ni stendi iliyopo katikati ya mji, haina ofisi za wakatisha tiketi, sehemu ya abiria kungojea usafiri imejazwa meza za wakatisha tiketi na kila biashara imeshindiliwa hapo hapo stendi. Na ikifika saa nne usiku inafungwa! Ni miongoni mwa stendi mbovu zaidi za mabasi ya mikoani (labda inaizidi stendi ya Arusha na Manyara (Babati) maana nazo ni stendi za ovyo ovyo mnoo)
U po sahihi sana / MAMLAKA ZISHUGHULIKIE SUALA LA STENDI MOSHI.
 
Ni Manispaa ya ajabu sana ukitembea mita 500 kutoka katikati ya mji unakutana na mashamba ya mahindi. Nyumba zimechanganyikana na mashamba

Iendelee tu kuwa Manispaa haifai kuwa jiji inapitwa mpaka na Kahama
Mkuu nini kilichokusibu huko?
 
Aliekuambia mahindi yanafanya kutokuwa jiji ni nani..?? Hii mind set ya mji kuwa jangwa ifike mahali ife mimea inafaida kushinda hata hayo majiji mnayokimbilia!.

Huu ni utetezi usio na mashiko. Acha mji uwe ni mji, yasiwe ni mashamba!
 
Nani kasema jangwa?
Ushaona jiji gani katikati ya jiji kuna mashamba ya mahindi?
Moja uchafu
Mbili makazi ya wezi
Tatu makazi ya wadudu na wanyama
Unachoongea hapa ni pumba tu na sijajua dhamira yako ni kuelimisha au ku portray uwezo wako finyu wa kufikiri.Ninyi ambao hamzalishi mazao kwetu ndio wengi ombaomba. Inasaidia nini kuwa na mji wenye magorofa halafu mna upungufu wa chakula
 
Unachoongea hapa ni pumba tu na sijajua dhamira yako ni kuelimisha au ku portray uwezo wako finyu wa kufikiri.Ninyi ambao hamzalishi mazao kwetu ndio wengi ombaomba. Inasaidia nini kuwa na mji wenye magorofa halafu mna upungufu wa chakula
Haya mangi so unataka kusema zile mita 10 ulizolima chakula ndio kinakutoshereza tembea uone watu wanavyolimq achana na uchafu wenu wa moshi
 
Nani kasema jangwa?
Ushaona jiji gani katikati ya jiji kuna mashamba ya mahindi?
Moja uchafu
Mbili makazi ya wezi
Tatu makazi ya wadudu na wanyama

Moshi ndio manispaa safi kuliko zote Tz, tuambie jiji la Dsm ambalo halina mashamba ya mahindi ni safi kuliko mji wa Moshi.??
Dsm hapa hakuna mashamba ya mahindi ambayo yanaweza kutumika kama makazi ya wezi lakini mji umejaa wezi, panya road, vibaka kila kona.
 
Nasubiri wana moshi waje kukubishia [emoji16]

Mji wa kahama una

1 Barick gold mining
2 Bulyanhulu Gold mining
3 kiwanda kikubwa cha maji kipo njiani kufunguliwa
4 kiwanda cha bati
5 vituo vya mafuta vingi na vya kisasa
6 BANK OF AFRIKA
7 DTB
8 NBC
9 CRDB
10 TPB
11 NMB
12 Elution
13 N.K

Watuwekee na MOSHI, wana nini cha kujivunia!!!
Naanza[emoji1427]
1 Watengenezaji wa Pombe aina ya Mbege
2.???
Kiwanda kikubwa cha maji kiko njiani kufunguliwa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kahama is a glorified village my friend and no body cares whether it's a town or municipal...
Human development index in kilimanjaro region is 0.631 ...this alone speaks volume
 
Niliwahi enda kilimanjaro ile njia ya kupanda mlima kilimanjaro ukipitia kibosho. Tulikuwa na watu weng katka safari hiyo ila kilamtu alikuwa anastaajabu umeme ulopita kwenyemigomba ukifuata mijengo y haja.
Ni migomban ila mijengo mizur. Umeme. Maji na barabara.
Weng tulistaajabu sana basi tukajifunza kitu kuhusu mkoa ule
Moshi vijijini[emoji1787][emoji1787]
Screenshot%20(20220323-225136).jpg
Screenshot%20(20220323-224104).jpg
Screenshot%20(20220323-224504).jpg
Screenshot%20(20220323-222358).jpg
 
Moshi ndio manispaa safi kuliko zote Tz, tuambie jiji la Dsm ambalo halina mashamba ya mahindi ni safi kuliko mji wa Moshi.??
Dsm hapa hakuna mashamba ya mahindi ambayo yanaweza kutumika kama makazi ya wezi lakini mji umejaa wezi, panya road, vibaka kila kona.

Siyo kiivyo. Dar linazidiwa pia kwa sababu ya ukubwa wake. Lakini naamini Dar ina sehemu kubwa safi kuliko Moshi. Lakini ina sehemu kubwa chafu kuliko Moshi
 
Binafsi sijawahi kufika Kahama wala Geita.. Ila Moshi nimefika.

Kwa faida ya wengi, tuanze kuweka picha za mji wa Kahama na Geita na wa Moshi waweke zao ili tuanze kuilinganisha hii miji.
Kahama ni gulio lililochangamka hakuna kitu ..

Waambie wakupe picha kama hii ya Moshi👇

FQUfLUaX0AYSAbD.jpeg
 
Nasubiri wana moshi waje kukubishia 😁

Mji wa kahama una

1 Barick gold mining
2 Bulyanhulu Gold mining
3 kiwanda kikubwa cha maji kipo njiani kufunguliwa
4 kiwanda cha bati
5 vituo vya mafuta vingi na vya kisasa
6 BANK OF AFRIKA
7 DTB
8 NBC
9 CRDB
10 TPB
11 NMB
12 Elution
13 N.K

Watuwekee na MOSHI, wana nini cha kujivunia!!!
Naanza👇🏽
1 Watengenezaji wa Pombe aina ya Mbege
2.???
Weka picha acha hadithi za kijinga.
 
Back
Top Bottom