Mossad wapo vizuri kwenye intelijensia

Usaliti yes; but zaidi ya usaliti IDF na agents wao wameionesha dunia kwa vitendo what intelligence means. Ule mlipuko wa pagers kwa walengwa specific uliishangaza dunia and was a highest alert to Hezbollah. Sijui walikosea wapi kuelewa what would follow next.
 
Haya mashambulizi yamepangwa kwa miaka mingi. Walihakikisha wanaingiza majasusi kwenye ngome ya adui na kujua nyendo na siri zao zote. Ishara ya kuanza vita ilikuwa ni ile milipuko ya simu.
 
Mungu kumbe anabariki mashoga!??
Hiyo ni vita kijana usiingize udini.
*2006 Israel alipigwa na huyu huyu Hizbollah akiongozwa na huyu huyu Hassan Nasrallah aliyeuawa.
*1973 Israel ilipigwa na Egypt Sinai Peninsula.Huyo Mungu wako mbariki wa mashoga alikua wapi??

*Hii ni vita kuwahiana ni jambo la lazima.
 
Mkuu kwa mara hii nimekubali mossad wana intelligence kubwa. Mimi siku zote naunga mkono Iran, Hezbollah, Hamas katika kuitetea palestina.
Ila toka hawa jamaa wapige tukio ndani ya Iran wakamuua kamanda wa hamas, wakalipua zile pagers, now wamemuua kiongozi wa Hezbollah, nimeamini hawa jamaa wamejipenyeza ndani kabisa. Nahisi wanamsubiri Iran ajichanganye naye wapige ndani kabisa ya Iran.
Hezbollah anapaswa kurudi kwenye hatua ya kwanza huenda anaokaa nao mezani ni ma-double agent.
 
Tupo wengi tuliowaunga mkono Hezbollah ila hawa Wayahudi ni Next level...Iran nae naona ni kwamba kasha kubali maana alibaki kuwa sapoti Hezbollah ila kwa hili atatuliza Mshono
 
Soma Charter yao mkuu, ingawa waliibadili kuficha hilo...Utasemaje kuhusu Hamas...? Au nikuletee Charter ya Hezbolah.....Itikadi ya dini ni driving force....Na mimi huo ndio msimamo wangu na nina evidence!
Hizbollah ni kundi lililoanzishwa na uislam ila ni multi-ideology organization.
Sio kikundi cha uislam pekee.
Hamas ni political organisation ambayo ilianzishwa na waislam.
Ila ni kwaajili ya Gaza na Palestina wote.
 
Fact.....
 
Hicho kibibi kinawaponda wamagharibi kikiwaita makafiri halafu simu na taarifa za Hezbollah kinapata kupitia vifaa vilivyotengenezwa na hao makafiri.

Ujinga uzeeni hauna dawa.
 
Hahahah mkuu hata wewe leo umekubali?

Kweli ngoma ngumu.
Unajua mkuu humu tunajadili mantiki sio mihemko na ushabiki.
Haya mambo yanaenda kwa mantiki kaka.
Kumuua kiongozi wa juu kabisa mwenye ulinzi mkali hutafsiri mambo mengi sana.
Hapa Hizbollah wamepata pigo kubwa ambalo litawazimisha huwenda kwa muda mrefu saaanaaaa.
 
Ndio masuala ya vita.
Kiukweli kupambana na Israel nchi ambayo inapata msaada wa kila aina na taifa tajiri kama US ni kazi mno...

Hata Yuda alimuuza Yesu kwa fedha..

Ni ngumu kwa Hezbollah ku sustain maisha ya kila siku kukwepa intel za IDF, kama mwanadamu kuna mahala utafanya mistake.
 
Alafu haohao Hezbollah Hapo Lebanon siô Wananchi wôte wanaiunga Mkono. Vivyohivyo Kwa Hamqs utegemee Ushindi kwèli

Mimi nahisi haqacwakubwa wadunia hizi vita NI zaidi ya tunavyoziona
 
Kabisa mkuu, Israel wana pesa, wana misaada ya kila aina kutoka US na EU wanaweza kununua agent wanayemtaka...
 
Tishio la Netanyahu kwa Iran jana kuwa hakuna mahali popote ndani ya Irani ambapo "mkono mrefu" wa Israeli hauwezi kufika. Walikuwa wanamaanisha Ayatollah Khamenei na uongozi wote wa Iran unafikika.
Israel anaenda kasi sana angepunguza speed kidogo,aishie tu kwanza hapo hapo kwa Hezbollah maana kama heshima ameshaipata angalao sasa watu wapumue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…