Mossad wapo vizuri kwenye intelijensia

Mossad wapo vizuri kwenye intelijensia

Nikiri tu kwamba baada ya Hezbollah kukiri kifo cha Sayyed Hassan Nasrallah baada ya shambulizi la ijumaa, naona Mossad wamejipenyeza ndani kabisa ya uongozi wa Hezbollah.

Kiukweli sidhani kama Hezbollah inaweza kupambana tena na Israel.

Hezbollah itulie tu, hii vita wamekwisha shindwa vibaya.

Mimi kama mdau niliyekuwa mchangiaji mkubwa wa nyuzi za kuikubali Hezbollah hapa jamiiforums, nakiri kwamba Mossad ni next level, wametisha kwa hili....

Hezbollah watulie tu, hii vita hawaiwezi.
Unaambiwa walimtrack Kwa miezi miiingi sana.

Na sababu kubwa ya kumuua Jana, ni baada ya kupata Taarifa kua muda wowote Jamaa atahamia sehem nyingine wasoijua.
 
Unajua mkuu humu tunajadili mantiki sio mihemko na ushabiki.
Haya mambo yanaenda kwa mantiki kaka.
Kumuua kiongozi wa juu kabisa mwenye ulinzi mkali hutafsiri mambo mengi sana.
Hapa Hizbollah wamepata pigo kubwa ambalo litawazimisha huwenda kwa muda mrefu saaanaaaa.
Kuja tena kujipanga itawachukua muda na wakati huo wanajipanga haijulikani Mzayuni atakuwa amejichanganya ndani yao kwa kiasi gani na kiteknolojia atakuwa amefikia hatua gani.

Hata huko Hamas hapako salama Yahya Sinwar atakuwa amepoza sana kwa sasa.
 
Mkuu kwa mara hii nimekubali mossad wana intelligence kubwa. Mimi siku zote naunga mkono Iran, Hezbollah, Hamas katika kuitetea palestina.
Ila toka hawa jamaa wapige tukio ndani ya Iran wakamuua kamanda wa hamas, wakalipua zile pagers, now wamemuua kiongozi wa Hezbollah, nimeamini hawa jamaa wamejipenyeza ndani kabisa. Nahisi wanamsubiri Iran ajichanganye naye wapige ndani kabisa ya Iran.
Hezbollah anapaswa kurudi kwenye hatua ya kwanza huenda anaokaa nao mezani ni ma-double agent.
Una raia wengi takriban laki nane asili ya uyahudi unategemea nini!?
 
Kuja tena kujipanga itawachukua muda na wakati huo wanajipanga haijulikani Mzayuni atakuwa amejichanganya ndani yao kwa kiasi gani na kiteknolojia atakuwa amefikia hatua gani.

Hata huko Hamas hapako salama Yahya Sinwar atakuwa amepoza sana kwa sasa.
Hili ni pigo kubwa sana.
Naskia jamaa anasema wametangaza vita.
Japo mimi sishauri,huu uwanja umeshainama aisee tena pakubwa saaanaaa.
 
Imani hizi 😂😂

Unajua Imani NI kama Madawa h kulevya unaweza kujiona Bill gates kumbe Maskini WA kutupa
Huyo bibi anawaponda wayahudi na waamerica halafu yeye kasomea Canada na kaishi huko muda mrefu.

Nikamuuliza swali kwanini asingeenda kusoma Somalia au Palestina , hana majibu zaidi ya kusema "allah ndio anamchagulia mtu pa kuishi".

Very naive old woman.

Binafsi mimi sipendi vita naamini katika meza ya mazungumzo maana mwisho wa siku wanaoumia vitani ni wanawake na watoto ukifuatilia vita zote.

Hasara ya kupoteza miundombinu, kuja kuijenga nchi iliyoharibiwa na vita sio jambo dogo , sote tunaona Uganda na Tanzania licha ya kushinda vita ila uchumi ulianza kudorora kuanzia pale .
 
Huyo bibi anawaponda wayahudi na waamerica halafu yeye kasomea Canada na kaishi huko muda mrefu.

Nikamuuliza swali kwanini asingeenda kusoma Somalia au Palestina , hana majibu zaidi ya kusema "allah ndio anamchagulia mtu pa kuishi".

Very naive old woman.
Unajua we jamaa umeongea trivial point aisee!?
Unawez kwenda kusoma na kuishi Ukraine!?
Yani unataja mataifa ambayo yana vita na masikini!?
Angalau ungemtajia Brunei, Indonesia na Malaysia ningekuelewa.
 
Hicho kibibi kinawaponda wamagharibi kikiwaita makafiri halafu simu na taarifa za Hezbollah kinapata kupitia vifaa vilivyotengenezwa na hao makafiri.

Ujinga uzeeni hauna dawa.
Wapi kawaita makafiri?
Magufuli alipowaita mbona haijakuwa noma kiasi hiki ,au ni uchungu wa bandari kupewa muarabu sio dini yako? 😀 😀 😀
 
Tazama TV series hizi mbili, Tehran na Fauda uone namna Wayahudi walivyojipenyeza huko Iran, Palestina na Lebanon...

Fauda ni balaa. Hua najiuliza directors wa zile movies wanamakusudio gani?

Israel amejipenyeza kwenye maeneo mengi sana, inakua ngumu kupambana nao kirahisi. Inabidi kichwa kitulie sana.

Uko salama Mzee mwenzangu?
 
Wapi kawaita makafiri?
Magufuli alipowaita mbona haijakuwa noma kiasi hiki ,au ni uchungu wa bandari kupewa muarabu sio dini yako? 😀 😀 😀
Wewe ni timu ile ile mimi huwa sina muda siku hizi kufanya majadiliano na watu wa aina yenu .

Huwezi kuukubali ukweli awamu ya Magufuli huyo bibi alipotea jukwaani humu mpaka akawa anauliziwa hadi Magufuli alipokufa ndio akaibuka tena anazijua sababu za kupotea jukwaani humu.

Mimi sijawahi kuukubali utawala wa dikteta uchwara Magufuli na kwa mtindo huu wa kubadili mada husika siwezi kufanya majadiliano na walevi wa dini yoyote.
 
Naona na juzi bwana Netanyau kwenye Baraza la UN ameongea wazi kabisa kwamba safari hii hakuna adui yao yoyote watakaemuacha salama, yaani Kila mtu wanayemjua kwamba ni adui yao lazima watamfikia popote pale alipo na watamfanya kile kinanchomstahili.

Aisee Hawa jamaa wanajiona wao ni ma prince wa hii dunia
 
Mkuu Kosugi, nini kitafuata unafikiri......Iran haitaki kabisa vita, haiwezi kufanya lolote.....Umesikia hotuba ya Ayatollah lakini? Kaloa na baada ya hotuba kapelekwa mafichoni....
Ndio alie fadhili mauwaji ya 7 Oct 2023. Israel wamempimia kwa Rais wakala kichwa kumjulisha wameshajuwa kile walikipanga na vile walifadhili ule ugaidi. Kiufupi Pia Ayatollah wanakihitaji kichwa chake na wamedhamiria wanataka kifo chake kiwe cha kuonekana dunia nzima iwaogope wanataka sio tu kumu eliminate but seems wanataka baada ya kumalizana naye wanaivuruga Iran yaani isisimame tena. USA anajuwa yote haya na ana taarifa zote hizi ila sasa kila kitu kinafanyika kwa umakini mkubwa sana hasa ukizingatia Russian wanaipa support Iran hasa kwenye maswala ya kiusalama sasa basi vita ya Ukraine ipo kwenye shingo kwa mrusi hivyo lazima kuna mahali Putin lazima aiuze iran ili kupata kitu kwa Israel trust me. Kiufupi Iran wapo uchi maana Mossad wamesha juwa kila siri za Iran kupitia majasusi wao ndani ya idara nyeti za Urusi usiniulize kivipi.
Iran wanaenda kumalizana nayo Baada ya uchaguz wa Marekan. Ambao Trump atalamba shavu na ikumbukwe Trump ataipeleka marekani Vitani kumuondoa Ayatollah time will tell na ndio maana Iran na magaidi wanatamani kumla kichwa Trump ila kama unavyojuwa Israel wanamkubali sana Trump na wanajuwa akiwa Rais wamemaliza kazi.
 
Back
Top Bottom