Motra the future na Diss Track dhidi ya Kikosi Kazi awaita kikosi kazi WEUPE

Motra the future na Diss Track dhidi ya Kikosi Kazi awaita kikosi kazi WEUPE

pmawenge-20211210-0001.jpg
 
Ni mbabaishaji tu kazi kudiss Kila mtu Nani atamsupport sasa? Kama anafanya mziki wake kwà ajili ya mtaa Basi apunguze kulia lia ..
Media zinataka mziki ambao watu wengi wataskiza siyo mtaani kwenu tu pumbavu.
Uyo Nikk abaki na hip-hop yake ya kizamani ..siku hizzi Hadi wakina Nas na KRS One wanafanya Trap kupiga hela za mashabiki yeye abaki na mipasho yake.
naomba hiyo trap ya Nas na KRS one nikasikilize, inaitwaje hiyo ngoma maana kwenye kumbukumbu zangu Nas hajawah kupiga trap achilia mbali Teacher KRS one. Nasubiri
 
Motra si anakataa kataa wana hawajambeba! Mex anamwambia

Unakumbuka challenge ya Unju na Wakazi,
Walivyokwenda south ukadandia kijakazi,
Leo unasema mpo level moja we maandazi,
Huna shukrani unatapatapa tu hunyamazi,,

Utajua hujui,
Chalii unakua hukui,
Tushakuumbua futuhi,
Huwezi kusumbua uadui,
Hii inaitwa kichapo kutoka kwa mshua utaugua asubuhi..

Scars
 
Mex kaua mzee! Anamwambia

Utajua hujui,
Chalii unakua hukui,
Tushakuumbua futuhi,
Huwezi kusumbua uadui,
Hii inaitwa kichapo kutoka kwa mshua utaugua asubuhi..
Inakuuma nje ya boda wakiniongelea vizuri,
Utajuta kuwanyemelea manguli,
Hii kazi ni nzito utahemelea misuli,
We si mpenda weusi
Basi endelea kutembelea kivuli

Scars
 
Alichokifanya Cortex ni uwezo binafsi ambao sio kila Mc naweza, kwa muda mfupi tu tangu motra kaachia diss jamaa katoa bars kali za kumjibu ambazo mimi naweza kusema ni freestyle

Pengine hata yeye motra amepata uoga kujibu kutokana na kwamba huwenda ilimchukua muda mrefu kuandika hiyo diss, sasa anapokuja ku battle na metrix anaingiwa na uoga maana jamaa ni kama ana waiter wa mistari anafanya kuagiza tu
Weka ushabiki pembeni ..Hiyo ngoma ya cortex aliyomjibu montra n ya kawaida mnoo .... yan haifikii hata robo
 
Back
Top Bottom