Motra the future na Diss Track dhidi ya Kikosi Kazi awaita kikosi kazi WEUPE

naomba hiyo trap ya Nas na KRS one nikasikilize, inaitwaje hiyo ngoma maana kwenye kumbukumbu zangu Nas hajawah kupiga trap achilia mbali Teacher KRS one. Nasubiri
 
Motra si anakataa kataa wana hawajambeba! Mex anamwambia

Unakumbuka challenge ya Unju na Wakazi,
Walivyokwenda south ukadandia kijakazi,
Leo unasema mpo level moja we maandazi,
Huna shukrani unatapatapa tu hunyamazi,,

Utajua hujui,
Chalii unakua hukui,
Tushakuumbua futuhi,
Huwezi kusumbua uadui,
Hii inaitwa kichapo kutoka kwa mshua utaugua asubuhi..

Scars
 
Mex kaua mzee! Anamwambia

Utajua hujui,
Chalii unakua hukui,
Tushakuumbua futuhi,
Huwezi kusumbua uadui,
Hii inaitwa kichapo kutoka kwa mshua utaugua asubuhi..
Inakuuma nje ya boda wakiniongelea vizuri,
Utajuta kuwanyemelea manguli,
Hii kazi ni nzito utahemelea misuli,
We si mpenda weusi
Basi endelea kutembelea kivuli

Scars
 
Weka ushabiki pembeni ..Hiyo ngoma ya cortex aliyomjibu montra n ya kawaida mnoo .... yan haifikii hata robo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…