Hip Hop ya Kibongobongo huwa inabadilika maana kutokana na kinachojadiliwa ni kipi na sio kipi kinamaanisha Hip Hop kwa ujumla.
Binafsi nayaona mapengo mengi kwa namna Harakati za Hip Hop zinavyotambulishwa kufanyika maana nyingi vitendo na uhalisia ni tofauti.
Matokeo yake wanatengenezwa mashabiki wa wanaojiita wana Hip Hop na sio mashabiki wa Hip Hop yenyewe na kila kilichomo.
Tukija katika hizi DISS TRACK Zinazoendelea kutoka juu ya WAFUASI WA WEUPI NA WA TAMADUNI MUZIK au WA KIKOSI KAZI. Hii yote ni zao la mashabiki wengi kutokuijua Hip Hop zaidi ya qanabaki kushabikia hao wanaHip Hop.
Kitu Kikubwa na Chakukikazia ni Namana Gani au nini maana ya nguzo ya Hip Hop ya MAHARIFA inavyoweza kuwasilishwa katika utamaduni wa Hip Hop.
Kwa upande wangu nimeweza kumuelewa ODWANG ODWA zaidi na nadhani DissHii ilikua iishie kwake, jaribuni kumsikiliza tena... Ukija kwa Motra bila kuathiri uandishi na upangaji wa maneno, ila Track yake ilihitaji majibu na ndio kinachofanyika ila je anajibiwa yeye au hoja zake.?
Hip Hop ya Bongo hata Niki Mbishi akimuandikia mashahiri dogo janja, yataonekana hayana vigezo vya Hip Hop labda mwandishi ajulikane ni nani? Ndipo tulipo.
Hip Hop sio RAP na Upangaji wa maneno pekee, MASSAGE ndio kila kitu hata ikiwasilishwa kwa maongezi... Harakati hazikua zakupigania haki za kupangilia maneno na vina katika Rap bali ni ukombozi na kila mtu kwa nafasi yake alitumia style yake iwe kwa kucheza, kuchora na kuandika kwenye kuta Madai ya haki zao na hawakuandika Hip Hop Never Die.
Hoja nyingi zinaonesha Motra hajafanya Hip Hop kutokana na kutokujua kuiandika na kuipangilia...
SWALI LANGU, KULIKUA NA ULAZIMA GANI WA KUJIBU MAKOSA?
TRACK YA MOTRA ILISHAISHA CHAJI WEEK ILEILE ILA KUENDELEA KUIJIBU NI SAWA NA KUANIKA BETRI JUANI.
KNOWLEDGE NDIO KILA KITU KATIKA HIP HOP.