Motra the future na Diss Track dhidi ya Kikosi Kazi awaita kikosi kazi WEUPE

Motra the future na Diss Track dhidi ya Kikosi Kazi awaita kikosi kazi WEUPE

Hao ndo wajinga kabisa, kwasababu group lilikuwa lipo kwenye process za kukamilika kitambo kabla hata ya hiyo diss

Afu hata interview wanazofanyiwa member wa kikosi kazi pale cluods zimekuwa zikiendeshwa na maswali yenye kuchochea bifu tu

Kwenye intrrview ya mawenge alipokua anaitambulisha ngoma yake ya nahamia weusi, mchomvu akampigia simu nikki mbishi yani kwa perception yake aliona kama nikki hakufurahia ile ngoma na kwa namna ambavyo nikki amekuwa mzee wa kuchana watu makavu walijua angemuaribia pale pale

Lakini nikki alijibu wisely sana na aka-tweet kuonesha kutopendezewa na namna ambavyo clouds wamekua wakuda
Clouds ni wakuda sana!

Walisababisha bifu ya Nako 2 Nako na Mapacha.
 
Kama Cholo kaununua hatari imekuwa mara 2.

Cholo naye ni msanii ambaye anawakubali sana wale wana wa Tamaduni music. Hata flow yake, upangaji wa vina, jinsi ya kuchora mashairi yaani mulemule. Ukimsikiliza tu unajua hili ni zao la Tamaduni.
Tamaduni imezaa wasanii wengi sana wa hip hop na hata kama hajatokea pale basi lazima kawa inspired

Rapcha mwenyewe ame admit
 
Pamoja na hayo yote bado hawaishi shobo

Kuna siku media moja ilikua inamfanyia interview nikki mbishi walimuuliza nikki mbishi mbona nyimbo zako hazichezwi redioni

Akawajibu mimi ndio niwaulize nyie kwanini hamchezi nyimbo zangu, wakasema "wewe hujawahi kuleta nyimbo zako studio ili tuzicheze"

Nikki akasema "mbona kwenye top ten ya nyimbo mnazozicheza kuna hadi ngoma za kina chris brown, ni lini chris brown alikuja studio kuleta ngoma zake?"
Manina!

Nikki bhana! Hahaha
 
Cholo brighter naye ni mkali mzee. Yaani flow yake imeathiriwa na flow za Tamaduni music hata upangaji wake wa vina. Moja ya mistari yake....

Haka kamchezo natamani kwa Sande,
Mi ni zaidi ya Baba Levo kwenye ukoo wa Mzee Nyange,
Na siogopi kuitwa mshamba,
Maana najua tisa na sita ni sawa ni mageuzi tu ya namba,

Ni vitasa kwa marapa wa juzi,
Msiombe mnikute Tabata si bata tu mtakula hata Mbuzi,
Na si la kipuuzi, Now wapuuzi wanaacha ukweli,
Mnasifia MC kinata wa Singeli...
Ngoja nimskize ngoma zake
 
Yaani Cholo ni zao la Tamaduni kabisa ukiskiza flow tu unajua aaah imekuwa inspired na Tamaduni.
Hahahaa huyu cholo wakumuangalia sana na haifai kabisa kum underrate hebu cheki hapa kwenye davinci code namna stamina alivyi pitiwa

Mwambie maradona nakoroma sio kinyonge, wanakoma wana homa watapona kwa vidonge.../

Niko boy ambapo awatoboi kina tina, jambazi dume siwezi kuliwa na kina star amina.../
 
Nipe mistari miwili:- Kitaa kuna wanyama njoo uone vicheche ukiweza tembeza rungu kama comrade kipepe.
S.O.N.G.A

Wapi wameandika kuvuta bangi ni dhambi, hii sio idea ya kizushi muulize mange kimambi.../

Juzi nlikua na scary schooby, akaniomba mistati nikamwambia sikupi.../

Skia mwana tusake sumu ya panya, sisi binadamu tunywe tuone itacho tufanya.../

Twende mbugani tuingie fresh na ndinga, tushuke tuanze kupiga selfie na simba.../

Hahahaha gheto na songa walitisha sana
 
Nimefatilia hiyo mistari ila sielewi kitu lkn naona wakuu mnatiririka comments na mnaelewana duh, kweli it's not my cup of tea. 🤤
Oya njoo tuongee biashara, hii sio ngumu uliyoizoea hii ni ngumu iliyo imara.../

Nasema kwa uhakika rafiki zangu ndio nyinyi, ila nacho sikitika sina rafiki ka mimi.../

Ingawa nawa amini, wote mlionizunguka nikianguka mtanidaka ila hainifanyi nisiwe makini.../
 
Sasa ulitaka nianze kufuatilia miaka ipi? Mi si zao la tisini Mzee?

Kwa kuwa nimeipenda Hip Hop nilirudi mpaka miaka ya nyuma(kusikiliza wasanii). Nimesikiliza mistari mpaka ya kwanza unit, Hasheem dogo( huyu mwamba ni mafia).

Ngoja nikuache.
Chief mnawadanganya hao kikosi kazi matokeo yake wanashindia chai na karoti.
 
Hao weusi wametengeneza pesa zipi mzee!!? Tuoneshe kwa evidence vitu walivyonavyo tuthibitishe kuwa muziki umewalipa,wale wako chini ya mawingu FM wanatengeneza wasanii wenye majina makubwa ila hawana kitu mfukoni ndo maana Maua sama ni msanii mwenye jina kubwa tz ila uliza anamiliki kipi cha maana kusema muziki umemlipa!!!!?the same to weusi wale jamaa hata shows sidhani kama zinawalipa maana nakumbuka mkesha wa Christmas 2019 Joe makini alikuja kupiga show mwanza pale the cask na kiingilio ilikuwa 5000 tu ila huwezi amini watu walioingia hawakuzidi 50.Hao wasanii wako unaowaona wakubwa ni majina tu ila ni choka mbaya because mtaa hauna habari nao

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
Ukisoma vyema sijazungumzia Weusi Mzee na pia sikumzungumzia Maua sama.Hiyo ni mifano yako

Hakuna cha Weusi wala Kikosi kazi wenye mafanikio ni kelele tu na ndio maana njaa zinawasumbua wengine wakakimbilia teuzi na wengine wanaendelea kubwabwaja ili tu wahurumiwe na jamii.

Tunawadangaya mtaa na jamaa wanavimba kuwa mitaa inawakubali..hakuna kitu kama hicho wataendelea wote kupotea.

Wakae chini wafanye kazi nzuri wataona tu mabadiliko ila wakiendelea na ujinga ujinga wataona mafanikio pia.
 
Pamoja na hayo yote bado hawaishi shobo

Kuna siku media moja ilikua inamfanyia interview nikki mbishi walimuuliza nikki mbishi mbona nyimbo zako hazichezwi redioni

Akawajibu mimi ndio niwaulize nyie kwanini hamchezi nyimbo zangu, wakasema "wewe hujawahi kuleta nyimbo zako studio ili tuzicheze"

Nikki akasema "mbona kwenye top ten ya nyimbo mnazozicheza kuna hadi ngoma za kina chris brown, ni lini chris brown alikuja studio kuleta ngoma zake?"
Watu wanamuona Niki mbishi ni mropokaji ila kiuhalisia Niki mbishi ni maana sahihi ya mwanaume , kwanini nasema hivi? Kwasababu Niki mbishi huwa hana tabia ya kufinya finya maneno.
 
Niko poa mtu wenu pamoja na mashabiki/
Pamoja kwenye mziki heshima kwangu haibanduki/
Mwanzo ni kale toka shule ya msingi mpaka kwenye ramani nlipofika sibanduki/
Kwa mmoja hata vikundi mludego nakata pindi/
Macho wanatumia zaidi wanasadiki/
Mi nungunungu uhaba wa miba hau nifiki/
Masikio yanasikia mitego nategua /
mengi nimepita machache yabakia/
Nikolabo na niko rhymes tena twafukia/
Walio zama wakiibuka hatua tunasogea/
Wakitembea wakisogea mizigo tumeshatua/
Uzembe waleta hasara na nafsi wazijutia/
Bado tupo jikoni kisha sokoni hewani tunawazingua/
Na umoja wa mashairi najua mmesikia/
Wewe ni motra au mota ni Bora uwe promota/
Wenge likizidi utaletewa medical doctor!/
Ukizidisha ukambale utapata ulichofuata/

NB:-Hahaha mleteni mc wenu mchague na venue mje mchukue maiti yenu....

cc Scars
 
Watu wanamuona Niki mbishi ni mropokaji ila kiuhalisia Niki mbishi ni maana sahihi ya mwanaume , kwanini nasema hivi? Kwasababu Niki mbishi huwa hana tabia ya kufinya finya maneno.
Ni mbabaishaji tu kazi kudiss Kila mtu Nani atamsupport sasa? Kama anafanya mziki wake kwà ajili ya mtaa Basi apunguze kulia lia ..
Media zinataka mziki ambao watu wengi wataskiza siyo mtaani kwenu tu pumbavu.
Uyo Nikk abaki na hip-hop yake ya kizamani ..siku hizzi Hadi wakina Nas na KRS One wanafanya Trap kupiga hela za mashabiki yeye abaki na mipasho yake.
 
Hao weusi wametengeneza pesa zipi mzee!!? Tuoneshe kwa evidence vitu walivyonavyo tuthibitishe kuwa muziki umewalipa,wale wako chini ya mawingu FM wanatengeneza wasanii wenye majina makubwa ila hawana kitu mfukoni ndo maana Maua sama ni msanii mwenye jina kubwa tz ila uliza anamiliki kipi cha maana kusema muziki umemlipa!!!!?the same to weusi wale jamaa hata shows sidhani kama zinawalipa maana nakumbuka mkesha wa Christmas 2019 Joe makini alikuja kupiga show mwanza pale the cask na kiingilio ilikuwa 5000 tu ila huwezi amini watu walioingia hawakuzidi 50.Hao wasanii wako unaowaona wakubwa ni majina tu ila ni choka mbaya because mtaa hauna habari nao

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
Wewe unaangalia show tu? WEUSI ni mabalozi wa makampuni kibao wanapiga pesa mule. Wake KIKOSI KAZI wana Nini Cha maana? Bila WEUSI kuwadiss wale jamaa tungeshawasahau.

BTN nenda kaskize Track Kali mpyaa kabisa ya MoTraa kuna madini utapata mule inaitwa #WEUPE
 
Back
Top Bottom