Dr Slaa kaahidi kushughulikia katiba mpya hivyo tumpe kura itafanyika
Dr Slaa kaahidi kushughulikia katiba mpya hivyo tumpe kura itafanyika
Mkuu hata huku bara inawezekana lakini wamekosea njia. Kitendo cha wao kuwa nyuma ya dini fulani zaidi ndo imekuwa kikwazo kwani hata mimi sitowapigia kura. Lakini kama wangekuja kiTanzania basi bila shaka kura yangu wangeipata.We unawazimu wa mchana hivi kwa fikra zako Slaa atakuwa Rais? nipe sababu zenye mshiko za Slaa na CHADEMA au chama chochote cha upinzani kushika nchi.....acheni ndoto za mchana nyie imeshindikana Zanzibar itawezekana Bara?
We unawazimu wa mchana hivi kwa fikra zako Slaa atakuwa Rais? nipe sababu zenye mshiko za Slaa na CHADEMA au chama chochote cha upinzani kushika nchi.....acheni ndoto za mchana nyie imeshindikana Zanzibar itawezekana Bara?
Tatizo lingine huku bara watu wajamii fulani fulani ni rahisi kurubunika, ni tofauti kabisa na kule zanji ambapo watu wakiamua hakuna anayerudi nyuma. Is fully tofauti na wengi wabara ambao ni wanafiki, na ni haohao waliokuwa wakiishabikia CCM miaka 5 iliyopita na sasa hivi wamebadilikia chama fulani na siajabu miaka 5 ijayo watahamia chama fulani
Huo ni unafiki ulioje! huku bara ni aibu tu na ubabaishaji uliovuka mipaka.
Leo huko Kenya (uhuru Park jijini Nairobi) Rais Kibaki anatia saini yake katika Katiba mpya ya nchi hiyo iliypitishwa na kukubaliwa na wananchi. Kuna baadhi ya vipengele -- kama vile haki za raia -- vinaanza kutumika mara moja.
Katiba hii imekuja baada ya miaka mingi ya ukandamizaji wa demokrasia ulioshia katika mauaji ya mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1500 walikufa katika vurugu.
Swali langu hapa ni: Kwa nini Wakenya wanatupita katika nyanja ya demokrasia wakati sisi ndio tulanza kupata uhuru kabla ya wao?
Jee nasi labda tunatakiwe tufe kwanza ndiyo tupate Katiba mpya -- maana kuna methali inayosema kwamba iUkiitaka pepo lazime ufe kwanza.
Au CCM inaona kwa vile inaendelea kutawala makundi ya makondoo ndiyo maana haitaki hata kusikia habari hiyo ya Katiba? Maana suala hilo hata halimo ktk Ilani yao ya uchaguzi! Wanaendelea kuinjoi tu na kuzoa mamia ya viti kwa kupitia ushindi wa meza kwani Katiba iliyopo inawa-favour sana. Lakini watambue kwamba wakiendelea kuibana hii mlipuko wake unaweza ukawa mkubwa kuliko hata wa Kenya.
Hawawezi badili katiba once wanajua kabisa ya sasa inawafavour.