Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

*Asema wingi wa mawaziri umelifanya Bunge kuwa butu
*Asisitiza badala ya kuisimamia serikali sasa linasimamiwa
*Alaumu viongozi wanaoheshimu wafadhili kuliko wananchi
*Alalamikia mahakama kutegemea fadhila ya Hazina

Andrew Msechu na Aziza Nangwa

SERIKALI imetakiwa kuhakikisha kuwa inaridhia mabadiliko ya kikatiba, kwa kuwa hakuna namna ya kuyakimbia kutokana na umuhimu wake kwa jamii ya Watanzania wa sasa.

Akifungua mkutano wa wadau wa vyama vya siasa na vya kijamii jijjini Dar es Salaam jana, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Wariob,a alisema mabadiliko hayo ni lazima kutokana na maendeleo ya kijamii yaliyofikiwa, ambayo yanaisukuma jamii kuipitia upya na kuiboresha zaidi katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema moja ya mambo muhimu yanayotakiwa kuangaliwa na kufanyiwa kazi kwa haraka, ni kulitenganisha Bunge na Serikali, ili kulipa Bunge nguvu ambalo sasa linaonekana kuipoteza baada ya kuelemewa na kuzidiwa nguvu na serikali.

Warioba alisema muundo wa serikali na idadi kubwa ya mawaziri waliopo bungeni umelifanya Bunge kushindwa kusimamia vyema uwakilishi wa mawazo ya wananchi, hivyo kujikuta likisimamia zaidi maamuzi ya mawaziri na serikali iliyopo madarakani na kulifanya Bunge kuwa la kupitisha hoja bila kupingwa.

"Suala la msingi ni kuangaliwa iwapo tunaweza kuliongezea Bunge madaraka, zaidi ni kuangalia uwezekano wa kulitenganisha Bunge na Serikali, idadi ya mawaziri na manaibu waziri ni kubwa, hali hii inaipa uwezo mkubwa serikali na hivyo serikali kusimamia na kuongoza Bunge na si Bunge kuongoza serikali, ndiyo maana kauli za sasa za wabunge ni 'tunaiomba serikali' na si 'tunaiagiza serikali' kufanya mambo kadhaa," alisema na kuongeza:

"Dalili hizi zinaonyesha kuwa sasa serikali ndiyo inasimamia Bunge na si wabunge kuisimamia serikali, tunahitaji pia kutazama aina ya wabunge na tujadili namna ambavyo uteuzi unaweza kufanyika."

Alisema ili kuboresha hali hiyo, ipo haja ya kufikia hatua ya kuwa na mawaziri ambao si wabunge, ili kutoa nafasi ya kuwa na Bunge huru, ambalo litakuwa na mamlaka kamili ya kuwakilisha mawazo ya wananchi na kuiwajibisha serikali.

Warioba alisema hata utaratibu wa muundo wa wabunge wa aina tatu, wakiwamo wa kuchaguliwa moja kwa moja kutoka majimboni mwao, wanaochaguliwa kwa viti maalum (wanawake) na wanaoteliwa na Rais, unaweka matabaka miongoni mwao.

"Utaratibu huu kikatiba unawagawanya, katiba inaeleza kuwa huwezi kuwa Waziri Mkuu kama si mbunge wa kuchaguliwa kutoka jimboni, hivyo kama umeteuliwa huna hadhi ya kuwa Waziri Mkuu hata kama una uwezo mzuri kiasi gani, huwezi kusema tuko sawa kisha viongozi wako ambao ni wabunge unawaweka katika matabaka, hawa wana hadhi ya juu hawa hadhi ya chini, hili si sahihi," alisema.

Aliongeza kuwa ipo haja ya kuangalia kwa makini utaratibu wa kuwatafuta wabunge katika njia iliyo sawa ili kuondoa tofauti zilizopo kikatiba na kuwafanya wote kupewa hadhi sawa katika macho ya Watanzania.

Akizungumzia suala la mahakama, Warioba alisema mhimili wa mahakama umekuwa haupewi umuhimu wa kutosha kikatiba, pamoja na kufanyiwa mabadiliko kutoka Idara hadi kuwa Mhimili wa Dola katika nchi, hivyo kuifanya kuendelea kuwa dhaifu.

Alisema wakati Mhimili wa Bunge ukiwa unapewa umuhimu, ikiwemo majengo na mazingira mazuri ya kufanyia kazi, mahakama imekuwa ikitengewa kiasi kidogo kabisa cha fedha na kuinyima madaraka na kipaumbele katika uboreshaji wa miundombinu, ikiwamo majengo.

"Wakati Bunge limepewa mamlaka ya kutosha, lakini unaweza kuona mpaka sasa Mahakama ya Rufaa haijajengewa jengo, haipo kwenye kipaumbele, suala la fedha na uwezo wa miundombinu inategemea fadhila au hiyari ya Hazina, sasa ni lazima tufike mahali katiba itoe mamlaka kisheria katika kuhakikisha miundombinu ya mahakama inaboreshwa," alisisitiza.

Alikitaja kipengele kingine kinachotakiwa kufanyiwa marekebisho ni juu ya mamlaka ya Rais katika suala la uteuzi wa nafasi mbalimbali, ikiwamo kumteua Waziri Mkuu na kumtaka kuwa lazima athibitishwe na wabunge huku ikiacha nafasi ya uteuzi wa mawaziri wengine mikononi mwake.

"Mabadiliko ya mwaka 1984 yalipunguza kwa kiasi madaraka makubwa aliyokuwa nayo Rais katika uteuzi, lakini bado kuna haja ya kuangalia madaraka ya uteuzi wa Rais kwa upande wa kisiasa, hata ikibidi mawaziri wengine ni lazima wathibitishwe na Bunge ili kuondoa uwezekano wa kuteuana kirafiki, hii inaweza kutuletea shida iwapo tutapata kiongozi asiyezingatia misingi ya uongozi bora," alisema.

Aliongeza kuwa kipengele kinachozungumzia juu ya Ujamaa na Kujitegemea hakina maana tena katika katiba kutokana na kukubali utandawazi, ambapo kutokana na kuzidi kwa matatizo ya kiuchumi kujiunga na taasisi za fedha za kidunia ikiwemo Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuliondoa uwezo wa kujiamulia mambo ya ndani.

Alisema misaada na mikopo inayotoka katika taasisi hizo na nchi tajiri imekuwa ikitolewa kwa masharti magumu.

Hata hivyo, Warioba alisema umefika wakati wananchi washirikishwe haraka katika kufanya mabadiliko ya katiba, lakini alielezwa wasiwasi wake juu ya hilo kwa kile alichosema ni kutoshirikisha wananchi katika mambo muhimu ikiwemo kusikiliza kero zao.

Alisema viongozi wengi wamekuwa wakisikiliza na kufanya maamuzi kwa kufuata mawazo ya wafadhili ambao kutokana na ufadhili wao, wamekuwa wakiwapa kipaumbele kuliko wananchi.
 
Ninachofahamu ni kuwa mtu yoyote wa Tanzania anafahamu vizuri sana kuwa katiba yetu ina viraka vingi sana ambavyo bado vinavuja. Mbali na lile pande lililokusanywa kule Lancaster ambalo kimsingi ni katiba ya kumsaidia Gavana kutawala koloni(si kuongoza) sehemu nyingine muhimu za katiba ya bongo iliandikwa na Msekwa alipoagizwa na mwalimu(hii issue Issa Shivji anaijua vizuri zaidi), na wengine walizugwa zungwa tu kuipitisha. Sidhani kama kuna mtu yoyote ndani ya CCM hasa wasio wanasheria na waliowahi kuwa madaraka kama watakubali katiba ibadilishwe.

Kubadilishwa kwa katiba maana yake ni kuwapa wananchi nguvu, kuondoa nguvu kutoka kwa chama na serikali. Jiulize ni kwanini mpaka leo Tanzania ina adhabu ya viboko, au kwanini mpaka leo Preventive detantion act inaendelea mpaka leo, hizi kweli ni kuwafanya watu waogope watawala(sio viongozi). Na waandishi wa habari nadhani mnajua jinsi PDA ilivyowaumiza...kwa kweli kwa hilo unless unatokea msukumo mkubwa sana kutoka nje na ndani otherwise mambo yatakuwa kama yalivyo sasa.
 
Huu mjadadara angeupeleka kwenye chama chake badala ya magezeti ili aonekane wa maana. Amegundua lini hili swala la katiba????
 
tulitaka kumuomba Rais mwinyi au Mh Salim atuongoze kwenye mabadiliko ya Katiba sasa kajitokeza jaji Warioba tushaanza kipiga mbiu za lalama, jamani hapa kazi ipo.

mie nimefurahia kuona upo umuhimu huo na kutoa motisha bravo warioba
 
Ila kama CCM wangekuwa watu wa kusikiliza basi walau wangeandika ukweli juu ya itikadi ya nchi iliyopo kwenye katiba kwani uukiangalia tafsiri ya ujamaa na kujitegemea utapata kichefuchefu.

Angalia katiba ibara ya 152 kwenye tafsiri y7a maneno nimechoka kabisa kabisa .
 
Hakika mabadiliko ya Katiba hayaepukiki na siku zote jaji Warioba amekuwa mstari wa mbele kuongelea hili swala. Executive branch ina nguvu sana wakati judicial na legislative vimedumaa, matokeo yake wabunge na majaji wamekuwa mabubu. Katiba ya sasa haimuwakilishi mtanzania ambaye ni mlipa kodi; kwahiyo, kilichopo ni taxation without representation.

Mjadala wa mabadiliko ya katiba inabidi uanze, na uanze sasa.
 
Kwa jinsi Warioba alivo weka hoja zake zimekaa vyema sana, kwani zinaonyesha umuhimu wa mabadiliko hayo kwa ajili ya mstakabali wa Taifa letu, na si vyama vya siasa! Huu ni mwanzo mzuri!

Nime shangaa na Msekwa (former spika) naye kuibukia kuiunga mkono hoja hii! (angalia http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=974)

naamini congent/influential figures including mzee ruksa, Salim and others, wakitokea kulisemea kwa nguvu hili, wana JF, vyama vya ushindani na wananchi wengine tukaunga mkono, pengine CCM na serikali yake itakubali yaishe ama italazima tu kukubali mabadiliko hayo.
 
Jamani Jamani, ebu nipeni somo kidogo hapa.
Hivi katika Kamati KUU zote za CCM, ni kamati ipi kuna jina la huyu warioba! na mara ya mwisho ilikuwa lini kuwepo katika kamati hizi!- Nimekwama hapo!..
Kifupi JF hongereni sana yaani kila alichosema ni maswala ambayo yalikwisha jadiliwa hapa na kutolewa Mapendekezo kama haya!..

Warioba: Mabadiliko ya Katiba hayaepukiki
*Asema wingi wa mawaziri umelifanya Bunge kuwa butu.
*Asisitiza badala ya kuisimamia serikali sasa linasimamiwa.
*Alaumu viongozi wanaoheshimu wafadhili kuliko wananchi.
*Alalamikia mahakama kutegemea fadhila ya Hazina.

Sasa badala ya kuanza kulalamika na kunyoosha vidole vyenu inabidi mjipe pongezi kuwa mawazo yenu hayapotei bure!
 
Wasomi wamshangaa Msekwa kubadilika kuhusu katiba

Na Andrew Msechu
WASOMI na wanazuoni wa masuala ya siasa katika Chuo Kikuu cha Dar as Salaam, wameeleza kushangazwa kwao na hatua ya Spika wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa, kuzungumzia umuhimu wa kuwapo kwa katiba mpya.

Wasomi hao wameungana na baadhi ya wanasiasa waliokuwa wakishiriki kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Kituo cha Dmoktasia nchini (TCD) ambao pamoja na Msekwa kuelezea umuhimu wa kuwa na katiba mpya, wengi wao walimlaumu kwa kudai kuwa amechangia kwa kiasi kikubwa kudumaza mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Katika maoni yake wakati akiwasilisha mada katika mkutano huo uliojumuisha wanasiasa, wataalam wa masuala ya kijamii, asasi za kidini na asasi zisizo za serikali, Msekwa alieleza mtizamo wake uliokuwa ukifanana na ule wa Jaji Joseph Warioba juu ya umuhimu wa kuwapo kwa katiba mpya.

Akizungumza na Mwananchi ofisni kwake jana, mtaalam wa utawala na masuala ya umma katika kitengo cha Siasa kitivo cha Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu cha Dar as Salaama, Dk Benson Bana, alisema nafasi anayoitumia Msekwa si yake kwa kuwa alikuwa na nafasi ambayo angeweza kuitumia kwa manufaa zaidi.

Alisema hatua ya Msekwa kuibukia katika kongamano la wanasiasa na asasi za kijamii si ya maana kwake, hivyo ni vyema angetafuta nafasi nyingine kwa kuwa alishindwa kutumia nafasi yake alipokuwa Spika wa Bunge.

"Kwa mujibu wa mwenendo mzima wa masuala ya siasa na uongozi, si hulka nzuri kiongozi anaposubiri awe nje ya mfumo ndio aelezee mambo ambayo angeweza kuyarekebisha akiwa ndani, hii inatupa mashaka," alisema Dk Bana.

Akizungumzia umuhimu wa katiba mpya, Dk Bana alisema pamoja na maeneo muhimu yanayohitajii mabadiliko ikiwemo muundo wa serikali na Bunge, pia ipo haja ya kutoa fursa kwa Bunge kuhakiki uteuzi wowote unaofanywa na Rais katika nafasi nyeti serikalini.

Alizitaja nafasi hizo kuwa ni pamoja na Mkuu wa Majeshi, Mkurugenzi wa Takukuru, Mkurugenzi wa usalama wa Taifa, Gavana wa Benki Kuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Magereza hata ikiwezekana mawaziri na makatibu wakuu.

Alisema upungufu uliopo kwenye katiba unatoa mwanya wa uteuzi unaofuata misingi ya urafiki katika nafasi muhimu, hivyo ni vyema kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kuwa wote wanaoteuliwa wanapitia mikononi mwa kamati maalum ya Bunge ili kuchunguzwa na kuonekana usafi wao kama ilivyo kwa Waziri Mkuu.

"Bunge ni nguvu ya Umma, linatakiwa pia kupewa uwezo huu wa kuwathibitisha viongozi wote wa ngazi za juu wanaoteuliwa katika nafasi nyeti hata kama ni kwa kuundwa kamati maalum kufanya hivyo, kamati ambayo itapewa hata nguvu ya kuweza kusikiliza maoni ya wananchi juu ya walioteuliwa ili kuona usafi na uadilifu wao kabla ya kuthibitishwa," alisema.

Naye Dk Mohammed Bakari ambaye ni mhadhiri mwandamizi wa kitengo cha siasa na uongozi chuoni hapo, aliungana na Bana kwamba hakuna suala jipya katika kilio cha katiba mpya kwa kuwa ni suala ambalo limekuwa likijadiliwa na kutolewa mapendekezo kila wakati lakini mamlaka husika zimekuwa zikilifumbia macho.

Alisema kutokana na ubutu wa baadhi ya mihimili ya dola unaotokana na upungufu mkubwa wa kikatiba, mgawanyo wa madaraka katika mihimili mitatu imebaki kuongozwa kinadharia zaidi na kwamba katiba mpya inaweza kutoa mgawanyo sahihi zaidi wa madaraka.

"Katiba ya sasa haikidhi mahitaji ya Watanzania na mfumo unaoendeshwa chini ya katiba hii haudhibitiki, hata dhana nyingine ikiwemo suala la Rais kuteua wabunge kinadharia halina mantiki, mbunge anachaguliwa na wananchi kuwakilisha wananchi, huyu anayeteuliwa na Rais anmwakilisha nani?" alihoji.

Hata hivyo, pamoja na wengi wa washiriki wa mkutano huo kumlaumu na kumwelekezea vijembe Msekwa katika mkutano huo, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema kinachowaponza viongozi wengi ni unafiki wanapokuwa madarakani.
 
Taifa linahitaji kujadili katiba (Maoni)

MJADALA wa mabadiliko ya katika nchini umeibuka tena katika mijadala, safari hii ukiibuliwa na watu wenye uzoefu mkubwa katika siasa za Tanzania kutokana na wao kuwa sehemu ya muundo wa utawala, tena wakishikilia nafasi za juu za uongozi katika nyakati tofauti.

Ni katika mkutano wa kujadili maendeleo ya katiba nchini ulioshirikisha wadau kutika vyama vya siasa na asasi za kijamii ndiko kwa mara ya kwanza viongozi hao watendaji wa zamani katika serikali na taasisi zake walikoibuka na hoja ya kutaka kufanyike mabadiliko ya katiba ili kwenda na wakati.

Aliyeibua hoja hiyo ni Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ambaye alisema wakati umefika sasa kwa Watanzania kupewa nafasi ya kuanza kujadili mabadiliko ya katiba ili kuboresha utawala bora kutokana na matatizo ya kiutawala yanayojitokeza kutokana na changamoto mpya zinazoikabili serikali.

Jaji Warioba, ambaye aliungwa mkono na Spika wa Bunge Mstaafu, Pius Msekwa, alisema matatizo na changamoto mpya zinazojitokeza sasa ndizo hasa zinazochochea fikra za kuifanyia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mabadiliko makubwa.

Kimsingi hoja ya Warioba ililenga katika kuiwezesha mihimili mitatu ya dola kufanya kazi zake kwa uwiano kimamlaka, huku akitoa mifano ya namna mihimili miwili ya dola inavyogeuka taratibu kuwa sehemu ya utawala badala ya kufanya kazi zake kama ilivyokusudiwa.

Kwa mujibu wa Warioba, Bunge limeanza kupoteza mwelekeo wake wa kusimamia utendaji wa serikali kutokana na mazingira ya sasa na taratibu limeanza kugeuzwa kuwa chombo ambacho kinasimamiwa na serikali.

Ingawa viongozi wa mhimili wa mahakama wamekuwa wakijitahidi kujitenga na serikali ili kuupa mhimili huo mamlaka inayostahili kikatiba, bado serikali, ama utawala umekuwa ukiibana kwa kuinyima vitendea kazi na hivyo kuulazimisha kuwa kitegemezi cha busara na hiari ya viongozi serikalini.

Kwa miaka mingi sasa, wazo la kuifanyia mabadiliko makubwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limekuwa likitolewa na viongozi kutoka vyama vya upinzani kwa maelezo kuwa mabadiliko ya mfumo wa kijamii na kisiasa kutoka uchumi unaoendeshwa na serikali hadi uchumi huria na kutoka chama kimoja hadi vyama vingi, yalitakiwa kuungwa mkono na mabadiliko katika katiba.

Kwa ufupi ni kwamba madai ya kuwa na katiba mpya yalianza tangu kuanza rasmi kwa mfumo wa vyama vingi Julai 1992, huku baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakitishia kususia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 hadi pale katiba itakaporekebishwa.

Lakini katika muda wote huo, serikali imekuwa ikipuuza madai ya katiba mpya kwa maelezo kwamba katiba iliyopo ndiyo iliyoifanya Tanzania kujenga amani na utulivu.

Matokeo yake ni kuwa serikali ilifanya mabadiliko madogo, yakiitwa mabadiliko ya 12 ya Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyoruhusu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi na kuelekeza vyama vya siasa namna ya kujipanga kushiriki katika chaguzi.

Lakini tunadhani kuwa busara za wazee wetu, ambao wamefanya kazi serikalini na katika ngazi za juu kwa muda mrefu zinahitaji kuzingatiwa katika suala hili na litakuwa jambo la busara iwapo serikali itasikiliza kilio hiki na kutangaza mjadala wa kitaifa wa kujadili namna bora ya kuifanyia katiba yetu marekebisho.

Mpaka sasa Katiba imewahi kurekebishwa mara 14, hali ambayo imesababisha mikinzano ya mara kwa mara baina ya kipengele kimoja na kingine na kusababisha tafsiri ya katiba katika masuala mbalimbali kuwa ngumu zaidi.

Uzoefu ni kwamba misimamo ya serikali nyingi duniani imekuwa migumu mno kurekebishika kutokana na mifumo ya kirasimu iliyojengwa na kuingia si katika maandishi peke yake bali pia katika nyoyo na fikra za watendaji wa serikali.

Lakini tunaamini migongano ya kiutendaji aliyoifafanua Warioba katika maelezo yake ina uzito wa kutosha kuiamsha serikali katika usingizi wake wa pono wa kuona kila jambo linakwenda sawa na kwamba katiba haiwezi kubadilishwa mpaka kutokee mzozo mkubwa wa kuitikisa nchi.

Tunaamini mjadala wa kitaifa kuhusu jambo hilo litakuwa ndiyo suluhisho la maana katika kujenga katiba itakayosimamia masuala yote muhimu katika nchi na hivyo kupanua zaidi wigo wa ushirikishwaji wa wananchi katika mambo ya utawala.
 
Wasomi wamshangaa Msekwa kubadilika kuhusu katiba

Na Andrew Msechu

WASOMI na wanazuoni wa masuala ya siasa katika Chuo Kikuu cha Dar as Salaam, wameeleza kushangazwa kwao na hatua ya Spika wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa, kuzungumzia umuhimu wa kuwapo kwa katiba mpya.


Wasomi hao wameungana na baadhi ya wanasiasa waliokuwa wakishiriki kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Kituo cha Dmoktasia nchini (TCD) ambao pamoja na Msekwa kuelezea umuhimu wa kuwa na katiba mpya, wengi wao walimlaumu kwa kudai kuwa amechangia kwa kiasi kikubwa kudumaza mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.


Katika maoni yake wakati akiwasilisha mada katika mkutano huo uliojumuisha wanasiasa, wataalam wa masuala ya kijamii, asasi za kidini na asasi zisizo za serikali, Msekwa alieleza mtizamo wake uliokuwa ukifanana na ule wa Jaji Joseph Warioba juu ya umuhimu wa kuwapo kwa katiba mpya.


Akizungumza na Mwananchi ofisni kwake jana, mtaalam wa utawala na masuala ya umma katika kitengo cha Siasa kitivo cha Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu cha Dar as Salaama, Dk Benson Bana, alisema nafasi anayoitumia Msekwa si yake kwa kuwa alikuwa na nafasi ambayo angeweza kuitumia kwa manufaa zaidi.


Alisema hatua ya Msekwa kuibukia katika kongamano la wanasiasa na asasi za kijamii si ya maana kwake, hivyo ni vyema angetafuta nafasi nyingine kwa kuwa alishindwa kutumia nafasi yake alipokuwa Spika wa Bunge.


"Kwa mujibu wa mwenendo mzima wa masuala ya siasa na uongozi, si hulka nzuri kiongozi anaposubiri awe nje ya mfumo ndio aelezee mambo ambayo angeweza kuyarekebisha akiwa ndani, hii inatupa mashaka," alisema Dk Bana.


Akizungumzia umuhimu wa katiba mpya, Dk Bana alisema pamoja na maeneo muhimu yanayohitajii mabadiliko ikiwemo muundo wa serikali na Bunge, pia ipo haja ya kutoa fursa kwa Bunge kuhakiki uteuzi wowote unaofanywa na Rais katika nafasi nyeti serikalini.


Alizitaja nafasi hizo kuwa ni pamoja na Mkuu wa Majeshi, Mkurugenzi wa Takukuru, Mkurugenzi wa usalama wa Taifa, Gavana wa Benki Kuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Magereza hata ikiwezekana mawaziri na makatibu wakuu.


Alisema upungufu uliopo kwenye katiba unatoa mwanya wa uteuzi unaofuata misingi ya urafiki katika nafasi muhimu, hivyo ni vyema kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kuwa wote wanaoteuliwa wanapitia mikononi mwa kamati maalum ya Bunge ili kuchunguzwa na kuonekana usafi wao kama ilivyo kwa Waziri Mkuu.


"Bunge ni nguvu ya Umma, linatakiwa pia kupewa uwezo huu wa kuwathibitisha viongozi wote wa ngazi za juu wanaoteuliwa katika nafasi nyeti hata kama ni kwa kuundwa kamati maalum kufanya hivyo, kamati ambayo itapewa hata nguvu ya kuweza kusikiliza maoni ya wananchi juu ya walioteuliwa ili kuona usafi na uadilifu wao kabla ya kuthibitishwa," alisema.


Naye Dk Mohammed Bakari ambaye ni mhadhiri mwandamizi wa kitengo cha siasa na uongozi chuoni hapo, aliungana na Bana kwamba hakuna suala jipya katika kilio cha katiba mpya kwa kuwa ni suala ambalo limekuwa likijadiliwa na kutolewa mapendekezo kila wakati lakini mamlaka husika zimekuwa zikilifumbia macho.


Alisema kutokana na ubutu wa baadhi ya mihimili ya dola unaotokana na upungufu mkubwa wa kikatiba, mgawanyo wa madaraka katika mihimili mitatu imebaki kuongozwa kinadharia zaidi na kwamba katiba mpya inaweza kutoa mgawanyo sahihi zaidi wa madaraka.


"Katiba ya sasa haikidhi mahitaji ya Watanzania na mfumo unaoendeshwa chini ya katiba hii haudhibitiki, hata dhana nyingine ikiwemo suala la Rais kuteua wabunge kinadharia halina mantiki, mbunge anachaguliwa na wananchi kuwakilisha wananchi, huyu anayeteuliwa na Rais anmwakilisha nani?" alihoji.


Hata hivyo, pamoja na wengi wa washiriki wa mkutano huo kumlaumu na kumwelekezea vijembe Msekwa katika mkutano huo, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema kinachowaponza viongozi wengi ni unafiki wanapokuwa madarakani.
 
Tuunde Katiba mpya - Warioba
2007-08-07 10:39:23
Na Nasser Kigwangallah
Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Joseph Warioba ameishauri serikali kuangalia upya uwezekano wa kuundwa kwa Katiba mpya ili kuingiza mapendekezo ya wananchi juu ya utekelezaji wa majukumu ya serikali katika kuingoza nchi.

Bw. Warioba alitoa wito huo jana wakati akifungua mkutano wa wadau kuhusu Katiba ya nchi ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Alisema ili kukidhi haja ya uongozi bora, demokrasia na utawala wa sheria, ipo haja ya kuwa na Katiba itakayojumuisha mambo yote muhimu, hasa masuala ya umoja na usawa miongoni mwa Watanzania.

Alisema Katiba ya sasa ina mapungufu mengi ambayo yanahitaji kurekebishwa ili kuendana na mfumo wa utandawazi na soko huria.

``Katiba yetu ya sasa ya mwaka 1977, inatokana na Katiba tatu: ile ya baada ya Kikoloni ya mwaka 1962; ya baada ya Uhuru mwaka 1962 na ile ya baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana mwaka 1964.

Katiba hii, licha ya kuwa imefanyiwa marekebisho kumi na manne hadi hivi sasa, bado tu kuna mapungufu mengi, hivyo kuwa na uhalali wa kuundwa kwa Katiba mpya au kuifanyia marekebisho makubwa ili iendane na mabadiliko ya nyakati,`` alisema.

Bw. Warioba alisema Katiba mpya haina budi kuyajumuisha masuala ya msingi, ikiwemo utawala bora, umoja wa kitaifa na usawa ambayo ni muhimu kuwepo kwani katika Katiba hayamo. Mapungufu haya yanafanya haja ya kuifanyia Katiba iwe bora zaidi.

Alisema Katiba ya sasa imejengeka katika mfumo wa ujamaa na kujitegemea, mambo ambayo Tanzania kamwe haiyazingatii, hivyo hayana budi kuondolewa kabisa.

Aliongeza kuwa katika zama hizi za utandawazi, serikali inashirikiana na jumuia ya kimataifa katika masuala mbalimbali, hivyo kufanya maingiliano ya kibiashara na tamaduni zingine, Katiba inapaswa iyatambue hayo.

Aliviasa vyama vya siasa kuacha malumbano na kusigana kusikokuwa na maslahi ya kitaifa.

Vyama viwe mstari wa mbele katika kulinda utaifa wetu kwa kizazi cha baadaye na kamwe visiwe ndiyo sababu ya kuvunjika umoja wetu, alisema.

Aidha, aliwaponda wanasiasa wenye uchu wa madaraka ambao wamekuwa wakihangaika kuhama kutoka chama kimoja hadi chama kingine wakisaka maslahi.

Mimi nawaita watu hawa kuwa ni mamluki, hawafai katika jamii yetu, ni wasaliti wa dhamana waliyopewa na wananchi.

Alisema Katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa sana ya kiutendaji, hivyo Katiba mpya impunguzie madaraka hayo na badala yake Bunge na Mahakama ziwe na mamlaka makubwa zaidi ya kuidhibiti serikali.

Wakati sasa umefika ambapo Bunge linatakiwa kuwa na mamlaka makubwa ya kiutendaji kuisimamia serikali, kwani hivi sasa Bunge linadhibitiwa na serikali kwa kuwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri wengi Bungeni. Hawa viongozi wa serikali wanafanya nini Bungeni? Alihoji.

Alisema Katiba mpya iweke bayana kwamba mawaziri wote watoke nje ya Bunge ili iwe rahisi kwao kuwajibika kwa wananchi kuliko ilivyo hivi sasa.

Mapema Mwenyekiti wa TCD, Profesa Ibrahimu Lipumba alimwelezea Bw. Warioba kuwa ni miongoni mwa watu wachache sana ndani ya CCM ambao wanasema kweli kwa maslahi ya taifa.

Tumekualika ufungue kongamano hili kwa kuwa mchango wako utatuwezesha kupata mapendekezo tutakayoyapeleka serikalini ili Katiba mpya ipatikane, Lipumba alisema.

SOURCE:[/B] Nipashe
 
Nadhani naweza kusema kuwa hii ni hulka ya viongozi wa Tanzania. Apio alivurinda sasa mambo ya pension lakini alianza kulalama sana alipukuwa akihitaji hizo pension na kuziona kiduchu. Msekwa sio kama tu alikwamishwa maendeleo ya mabadiliko ya katiba, yeye alishiriki kwa kiasi kikubwa kuunda katiba mbovu ambyo imewekwa viraka na sasa haiwekeki viraka tena.

Kama ukiweza kusoma hii text yote utajua mchezo uliofanyika. Lakini nadhani hata pale Dar ambapo tunasema kuna wasomi wengi nadhani wanaofahamu ukweli huu hata elfu kumi hawafiki.
http://www.eldis.org/go/display/?id=11422&type=Document
 
Wanaokula bila kunawa mikono.....................
 
People you can not be serious pamoja na kushutumi ujinga wote unaotokea hapa kwetu siamini kuwa KIA inaweza kukodishwa kwa dola tatu kwa siku, kwa sababu hata hoteli zilizoko mashenzini huko Kilimanjaro kwa usiku mmoja ni atleast dola 8, let us be serious guys. Sifahami mkataba wa kuikodisha KIA ukoje lakini haileti mantiki hata kidogo, our Government can not be that hopeless.
 
Nilipinga, naendelea kuipinga mikataba ya siri
Edwin Mtei
Kutoka Gazeti la Tanzania Daima

KATIKA majadiliano niliyokuwa nayo na waandishi wawili wa gazeti la RAI walionitembelea nyumbani kwangu wakitokea Dar es Salaam, moja kwa moja mwanzoni wa wiki hii, nilisisitiza kwamba mikataba tuliyo saini wakati nikiwa serikalini au Beki Kuu, ilikuwa ikitangazwa na mingine kuwasilishwa bungeni pale sheria ilipotaka hivyo.

Hata ile niliyosaini nikiwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki haikuwa ya siri. Ni jambo la kusikitisha kwamba RAI katika toleo la Alhamisi la Septemba 5, linamaanisha kama vile nimebeza msimamo wa Mheshimiwa Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Chama chetu cha CHADEMA juu ya jambo hilo.

Katika mazungumzo yangu na waandishi wa RAI, nilisisitiza kwamba sasa Tanzania haitishi wawekezaji kutoka ngambo tena, kama ilivyokuwa wakati wa zama za Awamu ya Kwanza.

Kwa hiyo ni lazima katika madini tuhakikishe wazawa wanakuwa wabia wa hawa wawekezaji wageni na pale ambapo Watanzania hawajitokezi vya kutosheleza, basi serikali ichukue hisa katika makampuni hayo.

Hii si tu kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya faida ipatikanayo inabaki hapa nchini, bali hasa wazalendo ni lazima kufuatilia kwa karibu mienendo ya haya makampuni kwa kukaa kama wakurugenzi katika bodi zao.

Niliwaeleza msimamo wangu kwamba ni vizuri serikali ikawezesha wachimbaji wadogo wanaokutwa katika sehemu zenye madini kushirikishwa kama wanahisa pamoja na wawekezaji wageni.

Ikiwa ni lazima hawa wenyeji washirikishwe wakiwa katika vikundi au vyama vya ushirika.

Kuwaondoa wenyeji kwa kuwalipa fidia ni kama kuwanyanganya urithi ambao Mwenyezi Mungu aliwatunuku katika makazi yao ya asili.

Kuwajengea shule au hospitali si hoja, kwa vile mwekezaji yeyote anaponufaika ana wajibu wa kujenga shule, zahanati na barabara kwa jamii inayomzunguka.

Katika kusisitiza uwazi katika mikataba ili kuondoa uwezekano wa rushwa (na ni ukweli usiopingika kwamba sasa Tanzania inanuka rushwa!), niliwapa RAI sheria mbili nilizozinukuu katika gazeti la Serikali ya Afrika Kusini.

Hizi Sheria zinaonyesha bayana jinsi wenzetu Afrika Kusini walivyo wawazi. Nimetaarifiwa kwamba RAI sasa linamilikiwa na mwana CCM mwandamizi na kama kupuuzwa kwa ushauri wangu kunamaanisha sisi hatutafuata nyayo za hawa wenzetu, nahofia rasilimali zetu zitatokomea kwa wapita njia na umma wa Tanzania tutaendelea kudidimia katika lindi la umaskini. Ole wetu Watanzania!

Hata hivyo nafarijika kwamba kutokana na jinsi umma wa Tanzania unavyoafiki msimamo wa Zitto, kuna matumaini kwamba ujasiri, uzalendo na umakini wa kizazi kipya kikiongozwa na Mbowe na Zitto, tutavuka mapema. Iko siku! Rushwa na ufisadi vinatokomea!

Katika mazungumzo yangu na RAI nilisisitiza kwamba Zitto Kabwe ameelezea kutoridhishwa kwake na jinsi wataalamu wa wizara walivyopuuzwa na Waziri Karamagi na hasa kwamba hata Tume ya Mazingira ilitakiwa kuridhika na mipangilio ya kuendeleza mradi wa machimbo ya dhahabu wa Buzwagi kabla ya mkataba kusainiwa.

Badala ya msisitizo huo, hawa waandisi wa RAI wanakuza mfano nilioutaja kwamba mkataba wa TAZARA ulitiwa saini na serikali tatu za China, Tanzania na Zambia huko Beijing, China. Kwani mkataba wa TAZARA ulikuwa wa siri?

Mtu mwenye akili timamu anaweza kulinganisha mkataba wa TAZARA na mkataba wa Buzwagi? Utawezaje kulinganisha kitu kinachojulikana na kitu ambacho hakijulikani?

Watanzania wataendelea kumiminika maefu kwa maelfu katika mikutano ya Zitto na Mbowe, hadi kieleweke ni nini hasa Waziri Karamagi kaidhinisha, na kwa nini hakuuambia umma wa Tanzania mpaka alipohojiwa bungeni?

Cha ajabu ni kwamba hata Bunge lenyewe (pamoja na wingi wa wana CCM huko bungeni) hawakujua lolote juu ya mkataba huo kabla ya Zitto kuliibua suala hilo.

Naandika makala hii fupi kwa Mtanzania, ambalo ni gazeti dada la RAI, nikiwasihi wasahihishe mapema, na pia kwa magazeti mengine ili ikiwezekana msimamo huu binafsi wa muasisi wa CHADEMA, chama cha Mhe. Zitto na Mbowe, uweze kujulikana.

Tutaweza tu kupiga hatua za maendeleo thabiti kwa kuwa waadilifu, wakweli, wazalendo wanaopenda na kuhurumia watu wao, tukijiamini na tukiwa jasiri kama hawa viongozi wa kizazi kipya.

Edwin Mtei, amewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) na Waziri wa Fedha, pia ni mwanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Anapatikana kwa simu namba 0754 387 177.
 
tuko mstari mmoja ila njia ya mkato ili kufikisha kilio chetu ni kuanzisha personal informal education kwa watu wasiojua hilo.
 
ccm wanapenda kuwafanya watanazania madoli, ila watake wasitake mwisho wao utafika tu.Msingi wa kuiondoa ccm madarakani unawekwa leo
 
Kwako Mheshimiwa rais Jakaya Mrisho Kikwete,

Katiba ya sasa iliyotayarishwa mwaka 1977 wakati chama kimoja, ilikusudiwa kukidhi mahitaji ya mfumo huo ambao ulikuwa na dhana ya chama kushika hatamu (Party Supremacy). Mbali na hayo, katika uundwaji wake haikuwashirikisha wananchi wengi wa taifa letu, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mijadala mingi na ya kwa mara kwa mara ya madai ya katiba mpya.

Serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikidhibiti madai haya kwa kuunda Tume na Kamati mbali mbali na kuifanyia marekebisho katiba iliyopo kwa nyakati mbali mbali, ambayo sio muhimu sana kwa taifa letu. Pia ingawa Tume zote zilizoundwa na dola zilishauri kutungwa kwa katiba mpya, serikali yetu mara zote imekuwa ikikwepa sana suala hili, wakati umefika sasa wananchi walengwa tunakuomba uanze kuliangalia suala hili kwa mapana na marefu, ili kuundwa kwa katiba mpya itakayoendana na wakati tulionao kisiasa na kisheria kama taifa ambalo ni huru, na pia kuundwa kwa tume mpya ya uchaguzi.

Sababu zangu za msingi, Mheshimiwa rais ni kama zifuatavyo:-


.....Itaendelea..........!
 
Ndugu si ungeimaliza barua kabla ya kuileta maana yake kipande ulichoandika sio kirefu kabisa mimi najua wanaposema itaendelea ni kwamba nafasi inakuwa imeisha sasa ndugu umeandika nusu ukurasa halafu unasema itaendelea, lakini tunaingoja.
 
Back
Top Bottom