Ngoja niwakumbushie
1. Jaan dushman
Kibopa kilikuwa kinaitolea pikipiki tumboni.
Katika wote Akshay ndio alifanya kazi kubwa.
Sonu Nigam kwenye nyimbo alitisha
2. Karan Arjun
Watoto walizaliwa mapacha wakauliwa halafu wakaja kuzaliwa tena coincidence na wazazi tofauti tofauti
3. Qahar
Hii kuna ile scene ya mama alipewa silaha na jambazi katika watoto wake wawili amchague mmoja asiyempenda amuue.
Mama akaielekeza silaha kwa jambazi aliyempa silaha na kufyatua trigger lakini hakukua na risasi.
4. Ajay.
Humu ni visasi na mwendo wa kukomoana kati ya Sun Deol na mwamba Dan Denzopa na kuna risasi ilipigwa ikakata hadi kona
5. Loha. Ile scene ya ku climb mlima na lile jaribio la kumnusuru mtoto asinyongwe liliniteka sana.
Kingine zile fujo za wale wafungwa zilikuwa zinafanya niwacgukie, walivyopagawa na uyoga baada ya njaa kali nilijifunza kitu kuhusu njaa
6. Chandaal (Samurai wa kihindi) Mnamkumbuka huyu mara ya mwisho alikuwepo hapa bongo juzi kati kwa boss wetu wa Simba?
7. Dilwale (1997) hii inasikitisha mwishoni Ajay alipopigwa risasi akitoa toy la gari mfukoni huku Sunil akijua anatoa silaha.
8. Mohra. Nasdinlshaa kikwetu tulikuwa tumempa jina la Jalwa.
9. Tridev. Nani anaikumbuka ile ngoma ya "oye oye"
Sun Deol alipigwa kiberiti akatoka ameiva
10. Jeet (1993)
Scene ambazo zilikuwa zinaniboa ni zile za Salman Khan kupigwa marungu ya kichwa kila time
11. Koyla
Hii sikutaka hata kuiandika kwasababu ilienda viral kila mtu aliijua.
12. Ajay
Zipo nyingi sana zingine nimeziacha kwasababu zilienda viral sana