KERO Moyo Medicare, Arusha hawajawasilisha michango yangu ya NSSF kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa

KERO Moyo Medicare, Arusha hawajawasilisha michango yangu ya NSSF kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimewahi kufanya kazi katika Taasisi ya Moyo Medicare, Arusha, na niliacha kazi zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Hata hivyo, hadi sasa Taasisi hiyo haijawasilisha michango yangu ya NSSF, licha ya kuwa makato yalifanyika wakati nilipokuwa kazini.

Nimejitahidi mara kadhaa kuwasiliana na uongozi wa Taasisi ili kupata ufafanuzi na msaada kuhusu suala hili, lakini sijapata msaada wowote. Pia nimefika katika ofisi za NSSF mara kadhaa kufuatilia suala hili, lakini bado sijapata ufumbuzi.

Niliacha kazi kwa utaratibu na kwa amani, baada ya kutoa notisi ya mwezi mmoja kama ilivyotakiwa. Pia nilikabidhi mali na vifaa vyote vya Taasisi vilivyokuwa chini ya uangalizi wangu na kukamilisha taratibu za kuondoka kazini (departure clearance).

Kwa sasa sina deni lolote kwa Taasisi hiyo, lakini cha kushangaza ni kwamba michango yangu ya NSSF haijawasilishwa. Hali hii inaninyima haki yangu ya kupata huduma na stahiki zinazotokana na michango hiyo.

Naomba mamlaka husika ichunguze suala hili na kuhakikisha michango yangu yote inayodaiwa inawasilishwa NSSF kwa mujibu wa sheria.

Screenshot_20260823_204058_Facebook.png
 
Back
Top Bottom