Mpaka leo hii sijui kwanini mchezaji wa mpira nchini Tanzania analipwa sh milioni 5 halafu mwalimu wa shule ya Msingi analipwa sh. Laki 3

Wewe huna akili na kama dunia ingekua inatumia mawazo Yako isingeendelea hivi Kwa akili Yako tu ya kuvukia bara bara unadhani hamna madaktari wanaolipwa milion 5 na kuendelea taasisi binafsi ukielewa Hilo ndio utajua maana ya taasisi binafsi timu sio za serikali mzee ndio maana timu ya taifa hamna mshahara serikali hailipi sawa na taasisi binafsi mzee naona hujielewi
 
Ndio maana huko juu nimesema haya ni matokeo ya mfumo mbovu wa UBEPARI. Life has been reduced to a simple game of numbers. Yaani watu wapo interested na kiasi cha pesa kinachoingia na sio VALUE inayokuwa added kwenye maisha.

Nashukuru umesema kwamba football sio kitu cha maana sana kwenye maisha. Binadamu tumekuwa "conditioned" ku pay attention kwenye vitu visivyo vya maana ilimradi kuna watu wachache wanapiga pesa nyingi kwenye vitu hivyo.
 
Nadhani wewe wala hujajua huu uzi kinachojadiliwa ni kitu gani.
 
Mnajaribu kuhoji vitu ambavyo ni mbingu na ardhi.

Daktari ni muajiriwa wa serikali na amesomea. Mchezaji mpira ni muajiriwa pia sio wa kudumu ndio maana anasaini mkataba, kipaji na juhudi zake ndio mshahara wake.

Hawa watu tunakosea kuwafanya mifano ni bora mleta mada angetumia mifano mingine ya waajiriwa wa serikali.
 
Wewe sasa unakuja vizuri..

Mfano tukiamua kama binadamu kuwalipa watu kwa umuhimu wao au umuhimu wa kile wanachokifanya kwa jamii

Unadhani mcheza mpira atakuwa ranked juu ya daktari/mfamasia/mwanajeshi /askari?

Kama jibu lako ni hapana, je ni nani alieweka mfumo wa sasa wa kumlipa mchezaji zaidi ya makundi yote uliyotaja hapo juu na je mfumo huo uko sawa kwa akili za kawaida za kibinadamu..?
 
Wewe ndio hujajua unataka kulinganisha taasisi binafsi na za serikali naona hujitambui
The fact kwamba huwezi kuchangia mada ya kawaida kama hii bila kuita wenzio wajinga, hawajitambui, hawana akili nk inaonyesha kiwango chako cha uelewa kilivyo kikubwa.
 
Mmmh daktari gani alipwa laki 7!?
Au unamzungumzia Afisa tabibu?
Afisa tabibu ndio laki 7 ila sio MD.
 
Kwani wachezaj wanalipwa na serikaliπŸ€” acha kuandika pumba kijana ishu za mpira zinaingiinaje na serikali πŸ€”
Hajui kama kwa daktari huyohuyo akifanya kazi Hindumandal anaingiza mpaka milioni 4 kwa mwezi.
 
Tuseme walimu wa serikali kaka.
Ila mwalimu wa private mathalan Yemen English medium kima cha chini 500k kwa mwezi.
 
Hajui kama kwa daktari huyohuyo akifanya kazi Hindumandal anaingiza mpaka milioni 4 kwa mwezi.
Kitu chochote kikihitajika saaaaana na mtu akiweza kukidhi huo uhitaji kwa kiwango kikubwa saaaaana na akiwa ndo mdhibit wa hicho kipato kinachoingia ni dhahir shair huyu ataingiza hela nyingi mfano Daktar wa watoto aliyejibrand vizuri mfano Dr. Hameer wa pale fire anahudumia watoto zaidi ya 40 plus sometime mpaka 90 kwa siku sasa mtu kamq huyu hawezi pitwa na Dr wa watoto aliye hata muhimbili na hata aga khan kwa maana ya kipato!!
 
Ni kweli ila sasa kutokana na huu utandawazi, mambo yapo hadharani wanaona na kusikia jinsi wenzao wanavyougeuza na kutumia mpira kuwa ni mojawapo ya Fursa. Kwa bahati mbaya ushabiki hawajaweza kuugeuza nao kuwa ni Fursa bali kwa wajanja wachache wanavitumia vijiwe vyao kama sehemu ya kufanya biashara yao e.g. uuzaji wa chai, tangawizi, karanga na kahawa bila kusahau alkasusu na supu ya pweza.
 
Kazi za kuburudisha watu zinalipa kwa sababu zinapendwa na watu wa aina zote yaani matajiri na masikini, wenye akili na wasio na akili, vijana na wazee. Wavivu na wasio wavivu.
 
huna akili kweli. unaangalia tu wachezaji wachache wa ligi kuu. vipi kuhusu wachezaji wa ligi daraja la pili la tatu na la nne.. wanalipwa posho tu zinazotia huruma. mbona huwajali hawa au wao sio binadamu
 
Kwani wachezaji wanalipwa na serikali?.....wachezaji duniani kote wanalipwa mara dufu zaidi ya waajiriwa wa serikali
 
Mchezaji analipwa na mwekezaji na anaingiza hela nyingi ndani ya muda mfupi, kuajiriwa na serikali ili ufaidi inabidi uwe chawa ule teuzi (kama anavyohangaika mwashambwa & co.) au babako awe na historia ktk sekta za fedha, bandari etc lakini kama kwenu hakuna hata balozi wa nyumba kumi kumi hata uwe dokta md utatupwa hukoo IBOROGERO au NYAKANAZI kama siyo MWANDIGA ambako kila kumwona ZITTO inabidi umsalimie vizuri akirudi bungeni akukaribishe ili nawe uwe mgeni wa mbunge
 
Si TZ tu... duniani kote wanamichezo wanalipwa pesa ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…