Mchezaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania analipwa sh milioni 5 hadi kumi kwa mwezi na bado hizo zinaonekana eti ni ndogo.
Ila mwalimu wa shule ya Msingi analipwa sh laki 3 kwa.mwezi ( hiyo inawezekana ikawa kubwa zaidi)
Daktari analipwa sh laki 7 kwa mwezi .
So katika taifa letu hili la Tanzania, mchezaji wa mpira wa miguu ni muhimu kuliko mwalimu?
Kuliko Daktari?
ili kazi iwe na mshahara hutegemea mambo mengi
1. Unazalisha au huzalishi
Ukiwa mzalishaji automatic malipo huwa makubwa
2. Umeajiriwa na nani?
Mwalimu anaajiriwa na serikali ambayo yenyewe pia ina njaa ila mchezaji anaajiriwa na matajiri
3. Unafanya kazi na nani?
Mwalimu anafanya kazi na wanafunzi ila mchezaji mpira unaangaliwa na watu wengi ikiwemo matajiri , wenye vyeo nk
4. Law of demand and supply
Wachezaji wote wa Tanzania hawazidi idadi ya walimu wa mkoa wa Dar es salaam, hadi inafikia mchezaji anawindwa na timu zaidi ya 5 kwa mara moja.
_ Kama mchezaji anagombaniwa , mwenye kulipa vizuri ndio atampata
5. ( KWA UMUHIMU)
_ Kipaji hulipa hulipa kuliko Elimu
Unaweza ukawa na fundi pikipikki au magari , unakuta kwa siku anakuingizia 100,000+ wakati huo mwalimu hana uwezo wa kuingiza hata 20,000
Hapo fundi bodaboda unaweza kumlipa 30,000 ila mwalimu utamlipa 10 tu