Mpaka leo kuna watu wanaishi nyumba za kupanga?

Mpaka leo kuna watu wanaishi nyumba za kupanga?

Yaani mpaka leo kuna watu wanaishi za kupanga? Poleni aisee ila niwaambie kitu huo ni uzwazwa inakuaje mpaka leo kijana mzima unaishi byumba za kupanga? Sasa kipindi wazazi wa wenzenu wanapambana kuwatafutia viwanja na mali watoto wao nyie wazazi wenu walikuwa wapi? Shame on them.

Ili kuondoa hiyo aibu ya wazazi wenu pambaneni mtoke hayo magodown mnayoishi hao.

This thread posted by someone who live in his house and use Samsung note 10 plus 5G
Mkuu,

Kuna kitu kinaitwa "Emotional Intelligence". Jaribu kukifuatilia ujiongeze.

Kama wewe mjanja sana umeweza kujenga hongera.

Kuna watu tofauti wenye uwezo tofauti, wenye vipaumbele tofauti, waliokutana na maswahibu tofauti katika maisha. Usiwanyanyapae kwa sababu hawajafanikiwa kama wewe, kama unaona kuwa na nyumba yako ni mafanikio makubwa sana maisha haya.

Wengine wameamua tu kupanga, wamepiga mahesabu ya kihasibu na kuona ujenzi una gharama kubwa kuliko kupanga, na wanaweza kufanya uchumi wao uende vizuri zaidi kwa kupanga.

Kuna siku nilikuwa naangalia documentary ya Vernon Jordan, tycoon la Kimarekani na kingmaker lililomsaidia sana Bill Clinton awe rais. Jamaa anasema hataki kujenga wala kununua nyumba, yeye kwa maisha yake kupanga ni rahisi zaidi, na anajua ku claim tax breaks na deductions vizuri zaidi akiwa anapanga. Na hapendi habari ya kufanyia maintenance nyumba yake, akiwa anapanga, mwenye nyumba ndiye anafanya maintenance, yeye kazi yake kulalamika tu.

Sasa hii habari ya kuunganisha kupanga na umasikini moja kwa moja, na kuwasimanga wanaopanga, kwanza inaonesha low emotional intelligence, ulimbukeni fulani upeo mdogo wa kujua kwamba, si kila mtu ana uwezo au ujanja kama wewe. Wengine kupanga ndiyo uwezo wao.

Lakini pia, inaonesha kutoelewa kwamba kuna watu wana uwezo wa kujenga, au kununua nyumba, lakini hawataki kufanya hivyo kwa sababu zao.

Kuna cousin wangu alipiga deal kubwa, mamia ya mamilioni ya shilingi, quite sometime ago, akawa na nyumba kubwa, nzuri, Mbezi Beach. Baadaye akawa anahitaji hela za kufanyia biashara zake, akaona ile nyumba kubwa sana na haizalishi kitu, akaiuza, akaenda kupanga sehemu ndogo, ile hela ya nyumba akairudisha kwenye mzunguko wa biashara zake ikawa inazalisha. Mtu kama huyo unaweza kuona anapanga, ukamuona mjinga, kumbe ana mahesabu kukushinda wewe.

Vernon Jordan: Make It Plain

"masikini akipata matako hulia mbwana"..ndicho kitu ninachokiona kwako...tofauti na hapo nitakuweka kwenye kundi la wavulana wa form II na sitatoa sababu kwanini!? 😛
 
Yaani mpaka leo kuna watu wanaishi za kupanga? Poleni aisee ila niwaambie kitu huo ni uzwazwa inakuaje mpaka leo kijana mzima unaishi byumba za kupanga? Sasa kipindi wazazi wa wenzenu wanapambana kuwatafutia viwanja na mali watoto wao nyie wazazi wenu walikuwa wapi? Shame on them.

Ili kuondoa hiyo aibu ya wazazi wenu pambaneni mtoke hayo magodown mnayoishi hao.

This thread posted by someone who live in his house and use Samsung note 10 plus 5G
Dunia duara..maisha hayana adabu.
 
Kwa shemeji yako sio kwako mkuu. Usifurahie kukaa kwenye kochi na rimoti hujui kaijengaje nyumba yake.
Ngoja dada yako atakapoamza kutoa vilio vya mahaba wewe upo sebuleni unaangalia movie ndio utakapojua umuhimu wa kupanga utoke kwa shemeji hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mpaka leo kuna watu wanaishi za kupanga? Poleni aisee ila niwaambie kitu huo ni uzwazwa inakuaje mpaka leo kijana mzima unaishi byumba za kupanga? Sasa kipindi wazazi wa wenzenu wanapambana kuwatafutia viwanja na mali watoto wao nyie wazazi wenu walikuwa wapi? Shame on them.

Ili kuondoa hiyo aibu ya wazazi wenu pambaneni mtoke hayo magodown mnayoishi hao.

This thread posted by someone who live in his house and use Samsung note 10 plus 5G

Mkuu,

Nikikwambia "Yani mpaka leo kuna watu bado wanatumia Samsung Note 10 Plus kama simu?" utajionaje?

Mimi natumia Samsung Galaxy S22 Ultra 5G na Wifi 6.

Hiyo Note 10 Plus tena ya 256 GB natumia kama dedicated MP3 player tu kusikilizia muziki kwenye bluetooth floorstanding speakers.

Hapo utajionaje na mashauzi yako?
 
Wewe ni miongoni mwa wale vijana aliowataja Magufuli msiokuwa na mchango katika taifa hili.
 
Utakuja uliwe kiboga mkuu oohoo mjini hapa we hashukwa tu
 
Kujenga mapema ni uwoga wa maisha na kutokua na uhakika wamakazi [emoji3] asilimia 90% ya vijana hua hatujengi nyumba za ndoto zetu , we jenga bana ukae kwako si tuta investment tutajenga uzeeni [emoji847]
 
Hujafa hujaumbika... Nani ajuaye ya kesho? Kuna watu katika umri mdogo kabisa walikuwa baba wenye nyumba lakini leo hii hata kodi ya chumba kimoja ni changamoto! HUJAFA HUJAUMBIKA..!
Angekua hayupo kwa shemeji yake Kapanga, asingeongea hayo. Labda kama anadekezwa sana na shemeji yake kwa sababu ya kudeka kwake na utiifu
 
Maisha hayana ramani fanya kila uwezalo uwekeze kwa kizazi chako.Ila yote tisa la kumi riziki na ziki za maisha humtembelea mtu mda wowote.
 
Mtani, hata kama huwa ni asili yenu kupenda sifa ila hapa zimezidi Mtani.

Pamoja na kutusimanga bado unataja na hiyo "Samsung note 10 plus 5G" ambayo huku Kijijini kwetu bado haijafika 🙌
 
Back
Top Bottom