Mpaka sasa Baada ya hizi nauli mpya na Tozo tunasemaje kuhusu Mama?

Mpaka sasa Baada ya hizi nauli mpya na Tozo tunasemaje kuhusu Mama?

Status
Not open for further replies.
Kosa lake kubwa ni kumteua Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha na Mipango! Atajutia sana kwa haya maamuzi yake.

Bora hata angemtafutia Wizara ya kipuuzi tu kama ile ya Muungano na Mazingira, nk.
 
... Rais Samia anaweza kuwa na madhaifu yake lakini haina maana kwamba hana mazuri yake. Uhuru wa habari na watu kujieleza bila vitisho vya dola, haki za binadamu, kutodhulumu wengine kwa ghilba (matajiri), kujiepusha na uongo uliopitiliza (sijui hakuna Corona, mabeberu wanatuonea wivu, dona kantri, etc.) kwa faida za kisiasa, n.k. ni kati ya mazuri aliyoanza nayo japo anahitaji kuboresha zaidi na naamini atafanya hivyo. Kubwa zaidi linalomsubiri ni Katiba Mpya/Bora.

Kuhusu kodi na nauli; kuliko kuwadhulumu wachache kila mtu alipe kodi japo sio rafiki. Ikumbukwe Mh. Rais hakwenda Bungeni kusoma, kujadili, na kupitisha bajeti. Tatizo ni Bunge; limeshindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo. Kama Bunge (wawakilishi wa wananchi) wamepitisha bajeti kama ilivyo, Rais alaumiwe kwa lipi? Hebu mpeni nafasi jamani!
Acha ujinga, mbunge hawezi kupinga matakwa ya raisi ndio maana uliona ndugai aliwaambia wasipopitisha bajeti raisi anaweza kulivunja bunge
 
Mama apige miaka yake 10.
tunaenda vizuri sana.
lawama ni jambo la kawaida ukiwa kiongozi.
 
Bunge si sehemu ya serikali, bajeti ilipelekwa bungeni na serikali, unadhani ni nani anapaswa kujua ugumu wa maisha kati ya bunge na serikali?
... Bunge ndio chombo cha uwakilishi wa wananchi ndugu; Bunge linatakiwa litetee wananchi. Kama linapitisha kodi kandamizi ni tatizo la Bunge. Bunge lingegomea hiyo bajeti ingepita? Lilaumiwe Bunge sio Rais.
 
Acha ujinga, mbunge hawezi kupinga matakwa ya raisi ndio maana uliona ndugai aliwaambia wasipopitisha bajeti raisi anaweza kulivunja bunge
... kama waliona bora kodi kandamizi zipite kuliko Bunge lao kuvunjwa bado ni udhaifu wa Bunge.
 
Tunaaasema anaupiga mwingi, mpaka 2030 atake asitake naaaa pia hatutakubali mamaetu atukanweeeee...
 
Mkuu nakubaliana na idea ya tozo kwa ajili ya kuboost maendeleo kwa nchi ila approach waliyotumia kina mwingulu ni mbovu ,mara nyingi tozo zinaweka kwenye huduma zile ambazo mpaka utumie maana umejipanga kwa hiyo ukinunua ni kama unachangia kwa hiyari.....Kuweka tozo kwenye huduma ambazo walalahoi ndio wanatumia sana au zina multiplier effect kubwa kwa walalahoi ndipo walipokosea!

Ila bado kuna option kwenye hiyo miamala kama unayemtumia yupo karibu ni bora umpelekee wakati ukiwa na muda wa kutosha ,utatuma tu endapo labda umebanwa au hautaki kupoteza muda....Kama unayemtumia mpo mkoa mmoja au jirani na unatuma hela kubwa ni bora kumpelekea manually.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom