Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Mpaka sasa jeshi la polisi halijatoa taarifa rasmi wapi Tundu alipo. Wananchi wanahofu kubwa juu ya usalama wa kiongozi huyu mkubwa wa chama cha upinzani nchini. Hata hivyo taarifa za awali zinasema kuwa alikamatwa na jeshi la polisi.
Wananchi mbalimbali wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu sana taarifa za kukamatwa au kupotea kwa Lissu lakini haijulikani ni kituo gani cha polisi alipo. Hawajui kama kakamatwa, katekwa au yuko katika mikoni salama.
Kiongozi huyu mkubwa ambaye alikuwa mgombea uraia mwaka 2020 na ambaye alinusurika kuuawa kwa risasi 16 mwaka 2017 alikuwa mbeya kwa ajili ya kuhudhuria kongamano la siku ya vijana duniani lakini polisi wakazuia kongamano hilo bila kueleza sababu za msingi za kuzuia kongamano hilo.
Hali ya upotevu wa Makamu mwenyekiti imeleta taharuki kwa wananchi wengi wanaofuatilia suala hili hasa baada ya Chama cha wanasheria nchini kutangaza kupotea kwa wananchi zaidi ya 80 ambao asilimia kubwa ya wenye listi hiyo wamepotea katika kipindi cha utawala huu wa awamu ya sita chini ya Rais Samia.
Tunalitaka jeshi la polisi lieleze mara moja kama limemshikilia makamu mwenyekiti wa CHADEMA au kama halimshikilii litueleze kama linamtafuta ili hofu ya kutekwa na kupotezwa iondoke.
Wananchi tuendelee kufuatilia hali ya makamu mwenyekiti