Mpaka sasa Umejifunza nini kuhusu Maisha?

Mpaka sasa Umejifunza nini kuhusu Maisha?

1. Simuamini mtu, najiamini mimi mwenyewe. Na Mungu tu !

2. Siku zote naangalia nilichonacho siyo nachokitaka.

3. Natarajia sifuri kutoka kwa mtu yoyote.
Namba 3 ukimanisha nini..? Yaani sifuri 0 au sifuri o 😃😃😃😃🤝🤝
 
Wakuu poleni na Majukumu, moja kwa moja kwenye mada .
Binafsi Mpaka sasa nimejifunza haya hapa👇👇
1: Kama hutapambana kufanya kazi kwa bidi kutimiza ndoto zako mwenyewe, kuna mtu atakuajiri na kukupa kusudi.

2: Maisha hayangojei uwe sawa, amka kila siku na uendelee kusonga mbele.


3: Wathamini sana Watu wanaokusema na kukufuatilia Maisha yako

Maana si kazi rahisi Mtu kuacha Matatizo yake na Kuyabeba yako.

4: Kaka jitaidi kuwa Smart, piga pasi na kaperfume kwa mbali.

Kuna wanawake Shida yao ni Mwanaume Smart tu.😀😀

5: Brother Unampenda? Mwambie Akatae yaishe, kuliko kumtumia hizo HEY,HI,Umekula??,Karibu Chai, n.k(be straight to the point)

6: Kuna mpaka ‘’Mabadiliko ya tabia ya Nchi’’ halafu wewe bado unaamini huyo mpenzi wako hawezi badilika??? really😀😀


7: Umri wa Miaka 30 ni Miaka mingi sana Kukaa Ofisini huku ukisubiri kuambiwa ni kipi chakufanya.


8: Maisha ni bora 100% wakati hakuna mtu anajua chochote kukuhusu wewe.

Binafsi nimechelewa sana kujua ukweli kuhusu Maisha, hasa ukitokea kwenye familia inayoamini kwamba ''education is better than Money''
Yaani hata kama kuna fursa ya Kuuza mchicha mtaani basi ukiifanya dharau na kejeli utakazokutana nazo sio za nchi hii.
Je? wewe mpaka sasa umejifunza nini kuhusu maisha????
Nilikua nashangaa sana mshua akiamka saa 11, siku moja akanambia "itafika kipindi matatizo yako yatakuamsha". Sasa nayaona
 
Maisha yako ni jukumu lako mwenyewe 100%..

Watu hawabadiliki bali wanaamua kujidhihirisha jinsi walivyo.

Usitarajie lolote kwa mtu yeyote maana matarajio mengi yanaumiza.

Namna nzuri ya kushinda ni kuacha kushindana, kama mtu anakushinda kwa mdomo wewe mshinde kwa kunyamaza.
Asante kwa maarifa
 
Back
Top Bottom