Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Kunipa maarifa ya kujenga nyumba yaani uashi.Haiwezekani ndege nofi anaeweza kujenga kiota kizuri lkn binadamu tunashindwa.
 
Up and down zangu zote na still nipo hai naendelea na arakati za kidunia bila kukata tamaa hilo tu namshukuru
 
Kwani hao wasio na kitu hawaku paswa kuwa na kila kitu?

Je huyo Mungu hakujua na hajui kwamba anapaswa kugawa kila kitu equally kwa kila mtu?

Huyo Mungu ni mbaguzi na mwenye upendeleo wa kuwapa watu wachache kila kitu huku akiacha maelfu ya maskini wasio na kitu wakimlilia na kumuomba awape angalau chochote kitu.

Huyo Mungu ni mwenye upendeleo sana na hastahili kuwa Mungu.

Na kama Mungu huyo yupo basi ni mkatili sana.

Mungu huyo, Alishindwaje kutoa kila kitu kwa usawa kwa kila mtu pasipo kuzidishia wengine na kunyima wengine?

Huoni kwamba huyo Mungu anafanya upendeleo?

Huyo Mungu kama ndio yupo namna hii, Hajielewi kabisa na ni mjinga sana.
Iko hivyo mkuu,
Kama kweli yupo, basi yuko biased sana. Kwa nini asigawe keki ya dunia kwa wote equally, wengine wanataabika na matatizo ya dunia wakati wapo wanaoishi mbingu ya duniani.

He's not fair, ndio maana wengi tunakuwa na mashaka sana mkuu.
 
Haya mambo huwezi kuyajua we endelea Ku hustle in vain
Kujua nini zaidi ya uongo uongo tu mnajifanya mnajua kumbe mnajua uongo tu.

Kama hicho unachojifanya unakijua huwezi kuthibitisha uwepo wake automatically ni uongo.
 
Iko hivyo mkuu,
Kama kweli yupo, basi yuko biased sana. Kwa nini asigawe keki ya dunia kwa wote equally, wengine wanataabika na matatizo ya dunia wakati wapo wanaoishi mbingu ya duniani.

He's not fair, ndio maana wengi tunakuwa na mashaka sana mkuu.
Afu hawa Theists waamini huyo Mungu ndio maskini choka mbaya kutwa kukesha kumuomba huyo Mungu huku wakiambulia patupu.

Halafu bado wanakaza mafuvu kuendelea kuwa na matumaini uchwara kwamba huyo Mungu wao atatenda..😆

Wanashindwa kukubali uhalisia kwamba huyo Mungu wao wanayedai yupo ni mchoyo sana na mwenye upendeleo au hayupo.
 
Achilia mbali zawadi ya uhai, afya na maisha aliyokujalia na bado anakukirimia wewe na mimi bure bila malipo wala gharama yoyote....

Nafahamu, Mungu amekutendea mambo mengi mno maishani mwako, na huenda ukiulizwa kuyasema, kwasababu ya muda na ufinyu wa platforms, usimalize kuyaorodhesha yote...

Hebu mbele ya hadhara hii ya familia ya wanaJF,
Shuhudia matendo mema na makuu ya Mungu kwa uchache, alioyokutendea maishani mwako, ili kwa pamoja kama watoto wa Mungu, tushuhudie sifa na utukufu wake kwa watoto wake katika ulimwengu huu....

Neema na Baraka za Mungu, ziandamane na kuambatana nawe daima, katika familia yako, kazi na majukumu yako ya kila siku daima na milele....

Amen..
Kunipa afya "NJEMA"🙏🙏🙏
 
Namshkuru mungu muumba nilinusurika kukumbwa na ugonjwa hatari sana wa stroke mnamo mwaka 2020, nikazidisha uchamungu maradufu. (ingawa sometimes najisahau) kwa neema, upendo, rehma na uwezo wake mkubwa mpaka leo hii nadunda... (Kama ni binadamu walifanya yale, nimewasamehe, kama ni jaribio lake mungu kwangu namshkuru.) Ingawa ni mtu mwenye mikosi sana na bahati mbaya... Ila mungu wangu ananiokoa mara kwa mara dhidi ya mitihani ya maisha.

Sina kinyongo na mtu, ila sitasahau. Najitahidi kuweka sawa nilipokosea maishani na nilipochelewa aidha kukanirudisha nyuma kwa namna moja au ingine.

Sina cha kumlalamikia, ila naamini kila kukicha amenijaalia nafasi ya kuendelea kupambana na kuandaa kesho bora binafsi.

Sina mtoto wala mke, pia sina mpango kutokana na upweke ninaouhisi kutokana na niliyopitia mengi maishani. Binafsi furaha yangu haipo huko, Na inawezekana kuwa happy bila mwenza... Napenda siku moja nikipata mapesa mengi zaidi niwe mtu wa kuhudumia jamii hasa makundi maalum yenye uhitaji. Nizeekee milimani, kwenye kajumba kadogo tu ka kawaida, niwe msafiri, niizunguke dunia, mvuvi na mfugaji.
 
Kujua nini zaidi ya uongo uongo tu mnajifanya mnajua kumbe mnajua uongo tu.

Kama hicho unachojifanya unakijua huwezi kuthibitisha uwepo wake automatically ni uongo.

Sawa upo sahihi mkuu but to me I'm believer and in GOD nothing impossible
 
kuna huyu mwanaume aliletwa na Mungu
Always thanksful kwa ajili yako Baba P😍
 
Kuweza kukaa kwenye mood Bila kutoka kwenye reli..... wapumbavu nyote mnaotaka nitoke kwenye mood
 
Hili swali wataliruka kama vipofu vile.

Wote hawa wanao comment mara ohh! Namshukuru Mungu kwa uhai, uzima, pumzi sijui afya n.k

Wanadhani kwamba kushukuru kwao hivyo, kutawaepusha na kifo, ajali, au kuumwa.

Kumbe ni uongo mtupu, muda wowote watakufa, wanaweza kuumwa au kupata ajali.

Lakini kwa vile watu hawa wamesha pumbazwa na dini zao wana comment urojo hapa mara uhai, uzima, pumzi n.k wala hawafikirii sawa sawa.
Una hoja usikilizwe
 
Kwani hao wasio na kitu hawaku paswa kuwa na kila kitu?

Je huyo Mungu hakujua na hajui kwamba anapaswa kugawa kila kitu equally kwa kila mtu?

Huyo Mungu ni mbaguzi na mwenye upendeleo wa kuwapa watu wachache kila kitu huku akiacha maelfu ya maskini wasio na kitu wakimlilia na kumuomba awape angalau chochote kitu.

Huyo Mungu ni mwenye upendeleo sana na hastahili kuwa Mungu.

Na kama Mungu huyo yupo basi ni mkatili sana.

Mungu huyo, Alishindwaje kutoa kila kitu kwa usawa kwa kila mtu pasipo kuzidishia wengine na kunyima wengine?

Huoni kwamba huyo Mungu anafanya upendeleo?

Huyo Mungu kama ndio yupo namna hii, Hajielewi kabisa na ni mjinga sana.
Hahahahahaha 😂😂😂😂😂😂
 
Kuniweka hai.mpaka sasa nikiwa na afya njema, akili, busara na hekima.

Aendelee kunipa uhai, hekima, busara, utajiri wa pesa na mali hadi uzee nikiwa na nguvu zangu.
 
Back
Top Bottom