Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Achilia mbali zawadi ya uhai, afya na maisha aliyokujalia na bado anakukirimia wewe na mimi bure bila malipo wala gharama yoyote....

Nafahamu, Mungu amekutendea mambo mengi mno maishani mwako, na huenda ukiulizwa kuyasema, kwasababu ya muda na ufinyu wa platforms, usimalize kuyaorodhesha yote...

Hebu mbele ya hadhara hii ya familia ya wanaJF,
Shuhudia matendo mema na makuu ya Mungu kwa uchache, alioyokutendea maishani mwako, ili kwa pamoja kama watoto wa Mungu, tushuhudie sifa na utukufu wake kwa watoto wake katika ulimwengu huu....

Neema na Baraka za Mungu, ziandamane na kuambatana nawe daima, katika familia yako, kazi na majukumu yako ya kila siku daima na milele....

Amen..
Mungu aliyonitendea ni mengi sana.....Sina pa kuanzia kusimulia.....
 
Uhai na afya njema ndiyo kila kitu kwangu.. MUNGU ni mkuu..
 
Wagonjwa wanaokufa ndugu zao hawamuombi huyo Mungu awaponye?

Mama yako ana u special upi wa kusema Mungu kamponya?

Au huyo Mungu ni mbaguzi anaponya watu kwa ubaguzi na upendeleo kwa kuruhusu wengine wapone halafu wengine wafe ilhali wote mnamuomba awaponye?
Ubaguzi wa mungu umejidhihirisha waziwazi Kwenye Quran ya waislamu pale ambapo mungu aliamua kumpa mtu mmoja Mohammed maelekezo ya kufanya hapa duniani na yanayomuhusu mungu mwenyewe ili atusambazie na sisi! Huu ni Ubaguzi wa wazi kabisa kwa mungu muweza wa yote, mwenye upendo wote, 😭ni sawa na wewe uwe na watoto Sita Kisha unamchagua mmoja kumsomesha na kumjali ilhali unao uwezo wa kumsomesha wote! 😂😂😂
 
Kunipa Uhai mpaka leo, walikuwepo niliozaliwa nao, nikasoma nao level mbalimbali lkn leo hawapo mm 40s yrs bado nadunda, regardless Mapito magumu.
 
nilitamani prado 120 nzuri mungu kanipa.. ni jambo kubwa kanifanyia.. alhamdulillah!
 
Back
Top Bottom