Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 478
- 1,025
Bologonja ni mpaka au geti linalounganisha hifadhi ya taifa ya Serengeti na Maasai Mara Kenya. Geti hili linawezesha mgeni kutoka Kenya Maasai Mara kuingia Serengeti kufanya game drive na kurudi Kenya kupitia mpaka huu.
Mwalimu Nyerere kwa kutumia akili kubwa na busara ya kizalendo kwa maslahi ya taifa alifunga huu mpaka na kufanya mgeni yoyote kutoka Kenya ni lazima afike Tanzania, alale kwenye hotel zetu, alipe viingilio na aingie hifadhini kufanya game drive. Hili jambo limepelekea Tanzania kulinda rasilimali zetu na kuzifaidi kwa kutengeneza ajira kwa vijana, na sekta nzima ya utalii.
Hivi majuzi mkutano wa EAC umeisha kukiwa na agenda ya kutaka kufungua mpaka huu, na agenda hii ilisukumwa na Kenya kwa kuzingatia madai ya kupunguza vikwazo visivyokuwa vya kikodi (NTB), Kenya wanatazama huu mpaka kama (NTB) huku sisi tukiutazama kama hatma ya sekta ya utalii, chanzo cha mapato kwa serikali na nyenzo muhimu katika kulinda maslahi ya taifa.
Swali je Wana diplomasia wetu wanatambua yanayoendelea? Je wamejipanga kupinga hoja iyo na kuimaliza moja kwa moja au tutegemee Samia akisaini makubaliano hayo bila kujua yana hatma gani kwa vizazi vijavyo? EAC ni muhimu ila isizidi maslahi ya taifa letu.