Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

Chadema ni chama cha kidemokrasia sanduku la kura ndiyo linaamua.Wala hakuna haja yamalumbano.Wanaopiga kura ni wajumbe wa mkutano mkuu waache waamue juu ya hatma ya chama chao

Kudhani kwamba mmojawapo akishinda Chadema itakufa ni kujidanganya kwa kiwango kikubwa chama hiki kilishavuka level hiyo
 
Huu ni uchambuzi au umbeya wa kumsifia Mbowe na kumchafua Lissu.
Embu rudi kaandike upya, hicho ulichokiandika hakina hadhi ya kuutwa uchambuzi hapa JF.
 
Nyinyi wa "Molemo" hamna la ziada la kuwajulisha watu, kwa vile majibu tayari mnayo; kama mlivyo yaweka hapo juu.

Kwa hiyo hakuna sababu ya kuwatafuta tena nyinyi kupata majibu ambayo tayari mmekwisha yaweka bayana kwa maoni yenu.
Majibu hapana hatuna, sisi tunachoandika ni uhalisia wa yale tunayoona, kutafiti na kusikia.Tunachoamini muamuzi wa kweli ni sanduku la kura

Unaweza kuonyesha hata mstari mmoja tumeandika kwenye taarifa hii halina ukweli?
 
Uimara wa CHADEMA chini ya Mbowe baada ya uchaguzi ni ndoto isiyo kuwa na maana yoyote.
Unaweza kuweka haba utafiti wako usiotia shaka kwamba yatatokea uliyoyaandika.Kwa sasa Chadema kimekuwa kikubwa kuliko personalities.Aondoke Freeman au Tundu chama hiki hakiwezi kufa kiko mioyoni mwa watu
 
Worse enough kaibukia upande wa Mbowe ingawa katokea moja ya wilaya za Mkoa wa Singida
Uhuru wa mawazo na uhuru wa habari ni jambo muhimu sana.Katika mfumo wa kidemokrasia nyakati nyingine inabidi ukubaliane na usichotaka kusikia.Hiyo ndiyo demokrasia
 
Sahihi kabisa, kama wanategemea watu wachache ndio wataaamua mapenzi ya wengi, basi watajua kuwa hakuna kitu cha kuheshimu maishani kama mahitaji ya nyakati.
Mwenyekiti atapatikana kwa wingi wa kura kwenye mkutano mkuu kama katiba ya Chadema inavyosema.Kura itapigwa katika mazingira ya uwazi kabisa hadharani na atakayeshinda atapewa muhula wa miaka mitano.

Sijaelewa hoja yako ya watu wachache kuamulia wengi
 
Chombo huru kinachoonesha wazi kipo upande wa Mbowe!
Molemo media haina upande kama taarifa yetu inavyojieleza.Ukweli ukiandikwa haina maana uko upande fulani.Wagombea waendelee kujinadi kistaarabu ili mshindi apatikane kwa haki na amani
 
Molemo media haina upande bali iko huru kuhabarisha ukweli kulingana na utafiti uliofanyika
🚮🚮🚮🚮
Nilikuwa nakuheshimu enzi zile wakati una ripoti habari zako lakini kwa andiko lako la Leo nimekushusha thamani yote.

Umeegemea upande mmoja kwa kusifia na upande mwingine umeusiriba tope. Hivi Unaweza ukasimama mtaani na kuanza kumsifia FAM na kumtukana TAL?
Aisee Meku Nimekushusha sana thamani
 
Narudia tena, muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umeshapita, na hili ni hitaji la wakati. Ifahamike mihitaji ya wakati ni zaidi ya hiyo katiba yenye utata kwenye kipengele cha ukomo wa madaraka.
Molemo media haina upande bali iko huru kuhabarisha ukweli kulingana na utafiti uliofanyika
Kuwa na upande sio lazima ww ukiri, maandishi yako yanatosha kuonyesha hilo.
 
Wachaga wa CHADEMA mmekuwa wa hovyo sana aisee 🤣🤣🤣

Nyinyi hamna tofauti na Wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita
 
Huu ni uchambuzi au umbeya wa kumsifia Mbowe na kumchafua Lissu.
Embu rudi kaandike upya, hicho ulichokiandika hakina hadhi ya kuutwa uchambuzi hapa JF.
Tatizo lako ni kwamba unataka usikie unachotaka kusikia.Molemo Media haiko hivyo kufurahisha mtu mmoja mmoja.Molemo Media itatoa taarifa ya ukweli kuhusiana na mtu.Tatizo lako unaonekana tayari una upande.Lililo muhimu tumia njia mbalimbali kushawishi wajumbe wa mkutano mkuu wampigie kura unayemtaka.Hiyo ndiyo demokrasia
 
Molemo Media inakushauri kutumia njia mbalimbali kushawishi wajumbe wa mkutano mkuu kumpigia kura mgombea unayempenda.

Pia ni vizuri wagombea wetu wakajikita kutoa sera nzuri ili kushawushi wapiga kura na kuachana na mtindo wa kuchafuana na kutuhumiana bila hoja za msingi
 
Wachaga wa CHADEMA mmekuwa wa hovyo sana aisee 🤣🤣🤣

Nyinyi hamna tofauti na Wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita
Mtu yeyote anayeingiza ukabila ama udini katika hoja yoyote ni kufilisika kabisa kifikra.

Unaweza kuweka hoja yako kinzani bila kutukana mtu wala kuzungumzia kabila la mtu
 
Hahaha Team Lisu hamna tofauti na Team WEMA.

Kumtukana kila msiyekubaliana naye mitizamo.
Molemo inashauri tena kushawishi kura kwa wa wajumbe siyo lazima kutukana upande wowote.Sanasana hiyo inaweza kupunguza kura kwa yule unayempigania kwa sababu wajumbe wa mkutano mkuu hawatamchagua mtu kulingana na wingi wa matusi yatakayotolewa bali kulingana hoja za ushawishi kutoka kwamgombea na wapambe wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…