Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

Kuna watu wenye busara na heshima katika jamii Molemo media ilizungumza nao na wakashauri mdahalo huo usifanyike

Sababu wanayotoa ni kwamba mdahalo huo uaweza kutumika kupakana matope na kusingiziana uongo usiomithilika.

Pia kuna hofu mdahalo huo unaweza kutumika kuanika siri za chama na kukitia doa chama hicho
Busara na heshima au hekima si chochote mahali ambapo uhalifu unatendeka. Watu wanazungumzia rushwa, mamlaka ziko kimya na zinashughulikia tu wezi wa mbuzi, kuku na bata, kama si uonevu nini? Wabadhilifu wa mali za umma, inabidi waende lupango- period- si haya ya busara na heshima.
 
"Freeman Mbowe ni kiongozi anayesimamia na kuliamini jambo lililopitishwa na vikao hata kama baadhi ya watu watalipinga na mfano mzuri ni maridhiano kati ya chama chake na serikali ya CCM."

Hayo maridhiano yalipitishwa na kamati kuu lini?

Alichosema Lissu hamna mahali kamati kuu imepitisha Maridhiano.

Mbowe ametoka gerezani akaibukia Ikulu na ndio akaja na hilo la maridhiano

Wao kama wajumbe wa kamati kuu wakaamua kukaa kimya kumlinda Mwenyekiti wao na kwa kufanya hivyo Lissu alikiri majuzi kwamba walikosea.
 
Wapi Molemo Media imetukana mgombea? Unaweza kuripoti kwa Moderators wakaondoa hayo matusi?
Mmekuwa wajinga sana aisee, ina maana mnatufanya watu hatuoni au kushuhudia uhalisia wa mambo?

Umempamba Mbowe na ku paka tope Lissu, yote hiyo ni njaa tu mmepewa hela kuja kumpamba na kumtetea Mbowe na kumsema vibaya Lissu hivi mna akili timamu?
Yaani vijana wa Mbowe mmekuwa na utahira mwingi sana. Halafu mnajifanya mpo huru kimawazo kumbe ni machawa tu wa Mbowe.

Jifunze kwa Uncle Pascal Mayalla anavyoandika maandiko yake.
 
It's the right time for mbowe to keep his balls on the highest place of the shelf so nobody can reach them
 
Njia mbalimbali kushawishi wajumbe wa mkutano mkuu kumpigia kura mgombea ni pamoja na kutoa rushwa na vitisho!!?

Mimi nasubiria clips za watu wanavyoshawishi wajumbe kwa rushwa zianze kutolewa ndio watu mtaumbuka.
Kwanini unapanga uhalifu wa kutoa rushwa? Kiongozi halali wa Chadema hatapatikana kwa kutoa rushwa bali kwa sera nzuri za mgombea.Nimushauri kama ulipanga hivyo uachane kabisa na mpango huo haramu
 
Sera za Mbowe ni zipi enyi madalali wake?
Tulivyokuwa na nyinyi wakati wote isiwafanye mtudharau. Sisi sio wajinga tuna akili za kujua kweli na utapeli.
Safari hii hamuwezi kutapeliwa
Kutukana mtu yeyote mwenye mtizamo tofauti na wewe ni kujionyesha jinsi ulivyo duni kifikra.

Wajumbe wa mkutano mkuu hawatamchagua mgombea kwa matusi yake wala ya wapambe wake
 
Busara na heshima au hekima si chochote mahali ambapo uhalifu unatendeka. Watu wanazungumzia rushwa, mamlaka ziko kimya na zinashughulikia tu wezi wa mbuzi, kuku na bata, kama si uonevu nini? Wabadhilifu wa mali za umma, inabidi waende lupango- period- si haya ya busara na heshima.
Mbona hujaeleweka unachotaka kukieleza.Ubadhirifu wa kitu gani?
 
Kutukana mtu yeyote mwenye mtizamo tofauti na wewe ni kujionyesha jinsi ulivyo duni kifikra.

Wajumbe wa mkutano mkuu hawatamchagua mgombea kwa matusi yake wala ya wapambe wake
Tapeli ni sifa sio tusi! Ila habari mnaipata wezi wakubwa nyinyi. Weka sera za Mbowe hapa badala ya brah brah
 
"Freeman Mbowe ni kiongozi anayesimamia na kuliamini jambo lililopitishwa na vikao hata kama baadhi ya watu watalipinga na mfano mzuri ni maridhiano kati ya chama chake na serikali ya CCM."

Hayo maridhiano yalipitishwa na kamati kuu lini?

Alichosema Lissu hamna mahali kamati kuu imepitisha Maridhiano.

Mbowe ametoka gerezani akaibukia Ikulu na ndio akaja na hilo la maridhiano

Wao kama wajumbe wa kamati kuu wakaamua kukaa kimya kumlinda Mwenyekiti wao na kwa kufanya hivyo Lissu alikiri majuzi kwamba walikosea.
Kwanini umechagua kumuamini mgombea mmoja usichague kumuamini mwingine?

Walau sisi wa habari tumekuwa tukifanya mahojiano mara kadhaa na Katibu Mkuu ambaye alikuwa anatupa magizo na maelekezo ya Kamati Kuu kuhusu maridhiano

Sasa leo hii hatuwezi kuchagua kumuamini mgombea kwa sababu inaweza ikawa ni lengo la kujitafutia kura
 
Hopeless kweli nakueleza alichosema mjumbe wa kamati kuu unaniletea habari za kumwamini mtu mmoja

Lisu ana sababu gani ya kudanganya jambo kama hilo na angedanganya si lingekuwa limekanushwa na hao wengine unaowasema wewe

Hii media yako ni ya kitu gani?? naona huku unaitwa nini media

Ndio kwa akili hizi unategemea hiyo media yako iwe credible?

Nchi ina matapeli hii
 
Mbona hujaeleweka unachotaka kukieleza.Ubadhirifu wa kitu gani?
wanasema kwamba kuna fedha za michango zinaingia kwenye account za mtu binafsi, hii ni kweli au ni matango? kama ni kweli ndip ubadhirifu wa mambo yenyewe. Molemo wewe uko humo CDM muda mrefu, je haya yasemwayo ni kweli ? Ni kweli kwamba michango ya fedha huenda kwenye a/c ya mtu binafsi?
 
Tapeli ni sifa sio tusi! Ila habari mnaipata wezi wakubwa nyinyi. Weka sera za Mbowe hapa badala ya brah brah
Inaonekana upeo wako ni hafifu sana.Mtu yeyote mwenye hoja hawezi kutukana mtu wala kumvunjia heshima.Mara nyingi matusi ya aina hii yanamyima kura mgombea unayempigania
 
Hopeless kweli nakueleza alichosema mjumbe wa kamati kuu unaniletea habari za kumwamini mtu mmoja

Lisu ana sababu gani ya kudanganya jambo kama hilo na angedanganya si lingekuwa limekanushwa na hao wengine unaowasema wewe

Hii media yako ni ya kitu gani?? naona huku unaitwa nini media

Ndio kwa akili hizi unategemea hiyo media yako iwe credible?

Nchi ina matapeli hii
Huwezi kushurutisha media yangu kukuamini Huo ni upuuzi na udikteta uliovuka viwango

Molemo media haiwezi kuendeshwa kwa porojo na propaganda ndiyo maana tumepata ukweli kutoka kwa Katibu Mkuu John Mnyika
 
Anaaminika na nani? unaona jinsi ambavyo reasoning yako ilivyo? Mimi kumwamini Lissu ni upuuzi ila wewe kumwamini Mnyika ni sahihi sio?

Hamna media hapa nisamehe kusema ni uchafu tu
 
wanasema kwamba kuna fedha za michango zinaingia kwenye account za mtu binafsi, hii ni kweli au ni matango? kama ni kweli ndip ubadhirifu wa mambo yenyewe. Molemo wewe uko humo CDM muda mrefu, je haya yasemwayo ni kweli ? Ni kweli kwamba michango ya fedha huenda kwenye a/c ya mtu binafsi?
Kwa utafiti wangu siyo kweli ila ni propaganda tu za uchaguzi

Kama kuna mwenye ushahidi wa kweli auweke hadharani na kutaja jina la huyo kiongozi ambaye michango inaingia kwa sababu kwenye hizi simu miamala ya kifedha siyo siri
 
Back
Top Bottom