Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

wanasema kwamba kuna fedha za michango zinaingia kwenye account za mtu binafsi, hii ni kweli au ni matango? kama ni kweli ndip ubadhirifu wa mambo yenyewe. Molemo wewe uko humo CDM muda mrefu, je haya yasemwayo ni kweli ? Ni kweli kwamba michango ya fedha huenda kwenye a/c ya mtu binafsi?
Kwa utafiti wangu siyo kweli ila ni propaganda tu za uchaguzi

Kama kuna mwenye ushahidi wa kweli auweke hadharani na kutaja jina la huyo kiongozi ambaye michango inaingia kwa sababu kwenye hizi simu miamala ya kifedha siyo
Anaaminika na nani? unaona jinsi ambavyo reasoning yako ilivyo? Mimi kumwamini Lissu ni upuuzi ila wewe kumwamini Mnyika ni sahihi sio?

Hamna media hapa nisamehe kusema ni uchafu tu
Uko desparate sana ndugu, nakushauri tu tafuta kura kwa mgombea unayemtaka, usitukane mpinzani wako wala asiyeunga mkono mgombea wako

Kushutumu na kutoa propaganda za uongo utafiti umeonyesha hausaidii sana wagombea kupata kura

Kura ni ushawishi lakini wa ukweli.Matusi , shutuma na kujimilikisha ukweli siyo sababu ya kupata kura.Kila mtu ana mtazamo tofauti.Na kuwa na mtazamo tofauti siyo ugomvi kwa mwanademokrasia bali kwa madikteta waliokubuhu
 
Ni vizuri sasa kwa vile umesema una mgombea wako ukamshauri ajikite kushawishi wajumbe wa mkutano mkuu wampe ridhaa.Kushinda uchaguzi ni ushawishi wa hoja na sera.Bila kufafanua vizuri sera zako unaweza usieleweke vyema.
Nani kakuambia kuwa sera ndio lazima ziamue mshindi?
 
Nani kakuambia kuwa sera ndio lazima ziamue mshindi?
Kwa mpiga kura anayejitambua anasikiliza sera na ukweli wa mtu anachozungumza, hatacukimtizama usoni unasema huyu kweli anamaanisha na siyo propaganda za uchaguzi
 
Kwa mpiga kura anayejitambua anasikiliza sera na ukweli wa mtu anachozungumza, hatacukimtizama usoni unasema huyu kweli anamaanisha na siyo propaganda za uchaguzi
Kuna hao wapiga kura wanaojitambua? Kwenye rushwa kujitambua ni porojo isiyo na mashiko.
 
Kwanini unapanga uhalifu wa kutoa rushwa? Kiongozi halali wa Chadema hatapatikana kwa kutoa rushwa bali kwa sera nzuri za mgombea.Nimushauri kama ulipanga hivyo uachane kabisa na mpango huo haramu
Kwamba unaamini bado hatujui uhalisia wa chaguzi zinazoendeshwa na viongozi wanaotaka kutoka madarakani wakiwa na miaka 68?
 
Kwamba unaamini bado hatujui uhalisia wa chaguzi zinazoendeshwa na viongozi wanaotaka kutoka madarakani wakiwa na miaka 68?
No evidence no right to speak.Huwezi kutuhumu tu bila ushahidi wowote ukaeleweka.Leo hii kuna watu wanatuhumu watu wa Lissu wananunua wajumbe na pia kuna wanaotuhumu upande wa Mbowe.Sasa je tutakurupuka tu kumtusi huyu au yule anatoa rushwa bila ushahidi? Tuache porojo za mtaani tysubiri wajumbe waamue nasi tuheshimu mawazo yao
 
Wapi umeona watu wakituhumu watu wa Lisu kuhonga? Lisu ana hela gani ha kuhonga? Au hapa ndio unadhani utanipoteza maboya boss? Naona ni kama umeishiwa na hoja za utetezi wa huyo king'ang'anizi wa madaraka. Wajumbe gani waamue, waamue watakacho lakini tunachokitaka tunakijua.
 
Nyie ndo mmemshauri vibaya mwamba kusudi adhalilike mfurahi...yaani mbowe leo hii ni wa kusubiri mbeleko za wajumbe kushinda uenyekiti...kweli?!.
Kwasabb ni dhahiri haungwi mkono na wanachama wengi wa kawaida (wasio na haki kikatiba kupiga kura).
 
Unapokuwa umeshajipambanua wewe unamuunga mkono nani siku zote mtu unajitia upofu kwamba mtu wako ni malaika na ndiye mkweli kuliko watu wote duniani.

Hiyo ndiyo shida ya kuunga mkono kundi fulani huwezi kuona makosa kwa hilo kundi na badala yake utajaribu kutumia kila njia kupaka matope na kuchafua upande wa pili ili waonekane hawafai.

Ushauri ninaoweza kukupa ni kufuatilia sera za wagombea na kujiondoa kwenye kundi hatari linalojulikana kama wapambe

Ukishaingia kwenye kundi la upambe huwezi kuona mapungufu ya kundi lako

Na ndipo sasa mgombea unayemtaka akishindwa utaanza kusingizia kila aina ya uongo kujifariji
 
Wajumbe wanaopiga kura wanapatikana kwa kupigiwa kura na wanachama kwa hiyo mgombea atakayeshinda atakuwa chaguo la wanachama wote
 
Ilikuwa kama utani na ilianza tetesi kwamba Tundu Lissu ameamua kupambana na Mwenyekiti wake ili kumpata kiongozi mpya atakayekiongoza chama hicho kwa miaka mitano ijayo

Sasa ni rasmi mafahali hawa wawili wameingia ulingoni ili kuamua ugomvi wao kupitia sanduku la kura.

Freeman Mbowe amekiongoza chama hicho kwa mafanikio makubwa mpaka zasa kiasi kwamba hata washindani wake wanakosa hoja ya msingi sana ya kushindana naye badala yake zimebaki tu propaganda za hapa na pale.

Freeman Mbowe mwanasiasa mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa mpaka sasa anaungwa mkono na wenyeviti 9 wa Kanda kati ya 10 waliopo huku pia akiungwa mkono na wenyeviti wa mikoa 24 kati ya 30 iliyopo

Freeman Mbowe amekuwa mwanasiasa na kiongozi mtulivu zaidi, anayesikiliza, anayeshaurika na ambaye hana maneno mengi sana bali vitendo kwa wingi.

Freeman Mbowe ni kiongozi anayesimamia na kuliamini jambo lililopitishwa na vikao hata kama baadhi ya watu watalipinga na mfano mzuri ni maridhiano kati ya chama chake na serikali ya CCM.

Tundu Lissu msanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu kwa muda mrefu ametangaza kugombea uenyekiti Chadema miezi mitatu tu tangu kutangaza kugombea Makamo Mwenyekiti wa chama hicho.Hajaweka wazi kwanini ghafla amebadili uamuzi wake

Tundu Lissu mwanasheria aliyebobea ni kiongozi ambaye ana misimamo mikali na ambaye haamini katika maridhiano.

Baadhi ya wapinzani wa Tundu Lissu wanamuona kama ni mtu anayeungwa mkono zaidi na makundi yaliyo nje ya Chadema hasa wanaharakati na watanzania waishio nje ya nchi.

Kingine ambacho wapinzani wa Tundu Lissu wanamwandama nacho ni tabia yake ya kupenda sana kuzungumza sana na vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii kama vile Club House, Spaces, Digital channels nk ambapo imedaiwa amekuwa akizungumza wakati mwingine mambo ya ndani ya chama.

Yote kwa yote msema kweli ni tarehe 21/1/2025 ambapo Mkutano Mkuu utachagua Mwenyekiti mpya kati ya miamba hii miwili ya siasa za Chadema na Tanzania kwa ujumla.

Sisi wa Molemo Media Tutawabarisha mambo mbalimbali kuhusu wagombea hawa kuelekea Januari 21 inayosubiriwa kwa hamu na Watanzania kwa ujumla.
Umeandika nini hiki mkuu au lengo lako ni kutangaza tu kuwa una miliki media?
 
Unapokuwa umeshajipambanua wewe unamuunga mkono nani siku zote mtu unajitia upofu kwamba mtu wako ni malaika na ndiye mkweli kuliko watu wote duniani.

Hiyo ndiyo shida ya kuunga mkono kundi fulani huwezi kuona makosa kwa hilo kundi na badala yake utajaribu kutumia kila njia kupaka matope na kuchafua upande wa pili ili waonekane hawafai.

Ushauri ninaoweza kukupa ni kufuatilia sera za wagombea na kujiondoa kwenye kundi hatari linalojulikana kama wapambe

Ukishaingia kwenye kundi la upambe huwezi kuona mapungufu ya kundi lako

Na ndipo sasa mgombea unayemtaka akishindwa utaanza kusingizia kila aina ya uongo kujifariji
Nasisitiza tena, si lazima hizo unazoita sera ndio zitoe mshindi, rushwa ina nafasi kubwa kwenye chaguzi hizi.
 
Hoja mojawapo ni kuwa Mbowe kafikia mwisho wa kukalia kiti hicho, na hili ni takwa la wakati. Mgombea wangu kashasema akipata hiyo nafasi atafanya nini. Ifahamike kuambiwa ukweli si kuchafuliwa.
... hayo ni maoni yako! Demokrasia inakutaka kuheshimu maoni ya wengine pia!
BOKSI LA KURA!
 
Jifunze kwa Uncle Pascal Mayalla anavyoandika maandiko yake.
Mkuu Manya,@manyanza, asante sana,hilo jamaa ni moja viongozi wakubwa tuu pale kwao,lakini ni lijitu lijinga ajabu!,stalisahau, limenichafulia CV yangu ya jf nikapigwa ban yangu ya kwanza na ya mwisho humu jf,kuna mtu analijua,akalitaja humu kuwa hili jamaa ni nani pale ufipa, akalutaja jina na cheo chake, mimi nika reply hiyo post,kwa kusema siamini ofisa mkubwa hivyo anaweza kuposti utumbo humu,lijamaa likaniripoti kwa mode kuwa ni mimi ndio nimelitaja jina lake na cheo chake hivyo kufanya kosa la name calling, nikala ban!。Nilikasirika ssna na siku hiyo ndio ingekuwa mwisho wangu jf,nikamwambia mode aliyemtaja jina sio mimi, mimi nime reply tuu, ndipo nikafunguliwa。
P
 
mmepewa hela kuja kumpamba na kumtetea Mbowe na kumsema vibaya Lissu hivi mna akili timamu?
weka ushahidi wa hicho hapo, short of this wewe ndiye mjinga kudakia mambo ya mitandaoni ukayaamini bila ushahidi
 
Back
Top Bottom