Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

Molemo Media inakushauri kutumia njia mbalimbali kushawishi wajumbe wa mkutano mkuu kumpigia kura mgombea unayempenda.

Pia ni vizuri wagombea wetu wakajikita kutoa sera nzuri ili kushawushi wapiga kura na kuachana na mtindo wa kuchafuana na kutuhumiana bila hoja za msingi
Hoja mojawapo ni kuwa Mbowe kafikia mwisho wa kukalia kiti hicho, na hili ni takwa la wakati. Mgombea wangu kashasema akipata hiyo nafasi atafanya nini. Ifahamike kuambiwa ukweli si kuchafuliwa.
 
Ilikuwa kama utani na ilianza tetesi kwamba Tundu Lissu ameamua kupambana na Mwenyekiti wake ili kumpata kiongozi mpya atakayekiongoza chama hicho kwa miaka mitano ijayo

Sasa ni rasmi mafahali hawa wawili wameingia ulingoni ili kuamua ugomvi wao kupitia sanduku la kura.

Freeman Mbowe amekiongoza chama hicho kwa mafanikio makubwa mpaka zasa kiasi kwamba hata washindani wake wanakosa hoja ya msingi sana ya kushindana naye badala yake zimebaki tu propaganda za hapa na pale.

Freeman Mbowe mwanasiasa mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa mpaka sasa anaungwa mkono na wenyeviti 9 wa Kanda kati ya 10 waliopo huku pia akiungwa mkono na wenyeviti wa mikoa 24 kati ya 30 iliyopo

Freeman Mbowe amekuwa mwanasiasa na kiongozi mtulivu zaidi, anayesikiliza, anayeshaurika na ambaye hana maneno mengi sana bali vitendo kwa wingi.

Freeman Mbowe ni kiongozi anayesimamia na kuliamini jambo lililopitishwa na vikao hata kama baadhi ya watu watalipinga na mfano mzuri ni maridhiano kati ya chama chake na serikali ya CCM.

Tundu Lissu msanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu kwa muda mrefu ametangaza kugombea uenyekiti Chadema miezi mitatu tu tangu kutangaza kugombea Makamo Mwenyekiti wa chama hicho.Hajaweka wazi kwanini ghafla amebadili uamuzi wake

Tundu Lissu mwanasheria aliyebobea ni kiongozi ambaye ana misimamo mikali na ambaye haamini katika maridhiano.

Baadhi ya wapinzani wa Tundu Lissu wanamuona kama ni mtu anayeungwa mkono zaidi na makundi yaliyo nje ya Chadema hasa wanaharakati na watanzania waishio nje ya nchi.

Kingine ambacho wapinzani wa Tundu Lissu wanamwandama nacho ni tabia yake ya kupenda sana kuzungumza sana na vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii kama vile Club House, Spaces, Digital channels nk ambapo imedaiwa amekuwa akizungumza wakati mwingine mambo ya ndani ya chama.

Yote kwa yote msema kweli ni tarehe 21/1/2025 ambapo Mkutano Mkuu utachagua Mwenyekiti mpya kati ya miamba hii miwili ya siasa za Chadema na Tanzania kwa ujumla.

Sisi wa Molemo Media Tutawabarisha mambo mbalimbali kuhusu wagombea hawa kuelekea Januari 21 inayosubiriwa kwa hamu na Watanzania kwa ujumla.
Wajumbe wafanye wafanyavyo wanachadema wanamtaka tundu lissu, wakikosea watakuwa wamekizika chama rasmi.
 
Chadema ni chama cha kidemokrasia sanduku la kura ndiyo linaamua.Wala hakuna haja yamalumbano.Wanaopiga kura ni wajumbe wa mkutano mkuu waache waamue juu ya hatma ya chama chao

Kudhani kwamba mmojawapo akishinda Chadema itakufa ni kujidanganya kwa kiwango kikubwa chama hiki kilishavuka level hiyo
..sawa mkuu, endeleeni kushupaza shingo, chadema isikilize maoni ya umma, chama kinaweza endelea kubaki kwa msajili kikafa huku mtaani
 
🚮🚮🚮🚮
Nilikuwa nakuheshimu enzi zile wakati una ripoti habari zako lakini kwa andiko lako la Leo nimekushusha thamani yote.

Umeegemea upande mmoja kwa kusifia na upande mwingine umeusiriba tope. Hivi Unaweza ukasimama mtaani na kuanza kumsifia FAM na kumtukana TAL?
Aisee Meku Nimekushusha sana thamani
Wapi Molemo Media imetukana mgombea? Unaweza kuripoti kwa Moderators wakaondoa hayo matusi?
 
Wajumbe wafanye wafanyavyo wanachadema wanamtaka tundu lissu, wakikosea watakuwa wamekizika chama rasmi.
Wajumbe hawatachagua mgombea kwa kushurutishwa wala kwa matusi bali kwa hekima na busara wakitizama chama chao kwa miaka 5 ijayo.

Ni vyema sasa wagombea wakajikita kutangaza sera zao bila kukashifu upande wowote
 
..sawa mkuu, endeleeni kushupaza shingo, chadema isikilize maoni ya umma, chama kinaweza endelea kubaki kwa msajili kikafa huku mtaani
Wala Chadema haiwezi kufa kwa sababu chama ni cha wanachama na siyo viongozi.Yeyote atakayechaguliwa ataungwa mkono na wananchi kwani ndivyo demokrasia inavyotutaka kuwa
 
Hoja mojawapo ni kuwa Mbowe kafikia mwisho wa kukalia kiti hicho, na hili ni takwa la wakati. Mgombea wangu kashasema akipata hiyo nafasi atafanya nini. Ifahamike kuambiwa ukweli si kuchafuliwa.
Ni vizuri sasa kwa vile umesema una mgombea wako ukamshauri ajikite kushawishi wajumbe wa mkutano mkuu wampe ridhaa.Kushinda uchaguzi ni ushawishi wa hoja na sera.Bila kufafanua vizuri sera zako unaweza usieleweke vyema.
 
Tunasubiria kwa hamu,hakika CDM imekuwa gumzo kila mahali.
Ni kweli kabisa imekuwa gumzo, nchi nzima imejikita kuzungumzia uchaguzi wa Chaddma hasa kwa ushawishi wa wagombea wake

Molemo media itajitahidi kufanya mahojiano na wagombea wote
 
Unaweza kuonyesha hata mstari mmoja tumeandika kwenye taarifa hii halina ukweli?
Sana. Mtu yeyote mwenye uhuru wa akili ataona kasoro kubwa kwenye andiko hilo. Ila kwa kuwa wewe tayari umejifunga pingu upande huo, kamwe huwezi ona tofauti na hayo unayo yafikiri wewe.
 
Unaweza kuweka haba utafiti wako usiotia shaka kwamba yatatokea uliyoyaandika.Kwa sasa Chadema kimekuwa kikubwa kuliko personalities.Aondoke Freeman au Tundu chama hiki hakiwezi kufa kiko mioyoni mwa watu
LOooh!
Mkuu 'Molemo, ni bora ulijipumzisha kuingia humu JF; kwa sababu inaelekea huko uliko sasa kunakuonyesha utofauti na dunia ya sasa ilivyo huku.
CHADEMA ina hali mbaya sana wakati huu. Ipo ukingoni kabisa. Ikikosea tu kidogo kumbakisha Mbowe; kazi itakuwa imekwisha.
 
Sana. Mtu yeyote mwenye uhuru wa akili ataona kasoro kubwa kwenye andiko hilo. Ila kwa kuwa wewe tayari umejifunga pingu upande huo, kamwe huwezi ona tofauti na hayo unayo yafikiri wewe.
Msomaji wetu tumesema onyesha jambo lolote ambalo si la kweli tuliloliandika

Molemo media tutaendelea kutoa habari kwa uhuru bila kuhofia yeyote kwa sababu tunaamini huo ndiyo ukweli
 
LOooh!
Mkuu 'Molemo, ni bora ulijipumzisha kuingia humu JF; kwa sababu inaelekea huko uliko sasa kunakuonyesha utofauti na dunia ya sasa ilivyo huku.
CHADEMA ina hali mbaya sana wakati huu. Ipo ukingoni kabisa. Ikikosea tu kidogo kumbakisha Mbowe; kazi itakuwa imekwisha.
Tukukumbushe tu mwaka 2016 kuna kiongozi alitabiri Chadema itakufa kabla ya 2020

Naona na wewe unatabiri kama huyo kiongozi, tukuhakikishie tu wewe siyo Mungu kutaka kusema hivyo.

Chama hiki kimejengwa mioyoni mwa watu.Kudhani kitakufa unajidanganya sana.Binafsi nimetoka ziara Katavi ya wiki 3 kuna maelfu ya wanachadema wala hawana habari na vituko mnavyoandika mitandaoni.

Wanachama wa ukweli vijijini wala hawana habari ya upuuzi unaoitwa makundi
 
Mdahalo wa Chief Odemba ujibu haya:
Who, did, what , when and how? Hiyo iwe ni cross examination kwa wote- Mbowe na Lissu katika nyanja zote za contentious issues, vinginevyo itakuwa ni kupuyanga tu.
 
Mdahalo wa Chief Odemba ujibu haya:
Who, did, what , when and how? Hiyo iwe ni cross examination kwa wote- Mbowe na Lissu katika nyanja zote za contentious issues, vinginevyo itakuwa ni kupuyanga tu.
Kuna watu wenye busara na heshima katika jamii Molemo media ilizungumza nao na wakashauri mdahalo huo usifanyike

Sababu wanayotoa ni kwamba mdahalo huo uaweza kutumika kupakana matope na kusingiziana uongo usiomithilika.

Pia kuna hofu mdahalo huo unaweza kutumika kuanika siri za chama na kukitia doa chama hicho
 
.......

Freeman Mbowe mwanasiasa mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa mpaka sasa anaungwa mkono na wenyeviti 9 wa Kanda kati ya 10 waliopo huku pia akiungwa mkono na wenyeviti wa mikoa 24 kati ya 30 iliyopo.....
Kwa hiyo wapiga kura ni hao wenyeviti 10 wa kanda na wenyeviti 30 wa mikoa!!!???
 
Molemo Media inakushauri kutumia njia mbalimbali kushawishi wajumbe wa mkutano mkuu kumpigia kura mgombea unayempenda.
Njia mbalimbali kushawishi wajumbe wa mkutano mkuu kumpigia kura mgombea ni pamoja na kutoa rushwa na vitisho!!?

Mimi nasubiria clips za watu wanavyoshawishi wajumbe kwa rushwa zianze kutolewa ndio watu mtaumbuka.
 
Back
Top Bottom