MITAZAMO YA MAKUNDI (8) NANE YA WATU WANAOMUUNGA MKONO MBOWE NA SABABU ZAO.
Na; Garatwa Francis
Wakati umma unaomuunga mkono Tundu Lissu ukiwaza zaidi juu ya kumpata Tundu Lissu awe M/Kiti wa CHADEMA ili Chama kiweze kuinuka tena na kutoka kwenye mifuko ya CCM na Dola yao walikokificha kwa manufaa yao. Wengine wanawaza zaidi kuhusu tumbo zao na wengine wanawaza kuhusu vyeo vya madaraka wapewe na Mbowe kama walivyozoea. Hii hapa mitazamo na fikra za watu wanaomuunga mkono Mbowe. Mitazamo hii nimeigawa katika makundi (8) manane maana hawafanani mitazamo yao kutoka kundi moja kwenda lingine.
1. Wapo wanaovizia Ubunge wa Viti Maalum wakiamini kwamba; Mbowe ndiye ALFA na OMEGA kwa Mwanamke yeyote yule kuweza kupata Ubunge wa Viti Maalum ndani ya CHADEMA. Hawa huwezi kuwaambia chochote kuhusu Mbowe wakakuelewa maana vipaumbele vyao vyote kwenye chama hiki kuanzia kipaumbele cha kwanza mpaka cha mwisho ni Ubunge wa Viti Maalum tu. Hawa hawataki kujionyesha wako upande upi hata kama hawamtaki Mbowe; wanahisi kama kuna JINI MAKATA linaweza kuwanyima Ubunge wa Viti Maalum kama wakionekana kumuunga mkono Tundu Lissu.
2. Wapo wanaopata MIGAO ya hizo fedha chafu zinazosambazwa na Mama kupitia kwa Kibanda, Balile, Wenje na Abdul. Hawa nao huwaambii kitu. Mfano mzuri sana ni huyo Boni Yai.
3. Covid 19 wanapambana usiku na mchana Mbowe ashinde ili warudi tena kuvuna mafao kwenye SACCOS ya mjomba wao. (Mfano; Mdee, Bulaya, Matiko n.k)
4. Baadhi ya Maafisa na Wakurugenzi wa Makao Makuu ya Chama wanapambana ili Mbowe arudi waendelee kukikamua chama pale Makao Makuu kwa sababu akitoka mirija yote itazibwa na Lissu na fedha zitashuka kwenda kwenye wilaya na majimbo kusaidia shughuli za ujenzi wa chama.
5. Hao CCM wao wanaamini kwamba, Mbowe akiendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA; wanaendelea kunufaika na uporaji wa chaguzi kwa sababu huyu Mbowe wa sasa ni kibogoyo asiye na meno tena ya kung'ata. CCM wanamtetea kwa maneno kwamba; CHADEMA mchagueni tena Mbowe ana hekima na busara 😂
6. Serikali ya CCM nao wanaamini Mbowe akiendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wataipata nafuu ya kupumua hasa kwenye presha ya masuala mazito kama Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi; lakini pia hoja nzito za kuibua mambo ya hovyo wanayoyafanya kwenye serikali yao.
7. Wapo ambao ni wahuni na walevi wanaopenda starehe za Bar (Mfano; Ntobi Emmanuel na Henry Kilewo na Martin Maranja). Kwa hiyo, wao Chama sio kipaumbele ila zile starehe ambazo Mbowe amewazoesha na kuwafanya wabweteke wakidhani maisha washayamaliza.
8. Wapo wanaolipa fadhira kwa Mbowe kwa sababu za kuwasaidia kushinda chaguzi za maeneo yao kutokana na matumizi ya fedha chafu kutoka CCM alizokuwa anazipigia kelele Makamu M/Kiti wa Chama Tundu Lissu kila kuitwapo leo.
Garatwa Francis,
Sauti ya wasio na Sauti.
Dar es Salaam, Tanzania.
29 Desemba, 2024.