Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

Sidhani kama ni kweli kwa sababu naona wajumbe wamegawanyika wapo wanaounga mkono upande huu na wapo wanaounga mkono upande wa pili.

Cha msingi wagombea wajikite kumwaga sera ili kubadili maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu
Ngoma nzito.
 
Ukilamba asali na akili inahama,nimekueleza wakati wa dr slaa ruzuku ilikuwa inashuka chini kuna sehemu andiko limesema dr alikuwa mwenyekiti,ujinga wako umependezeshwa na mikoba ya mbowe
Sitakujibu tena comment yoyote kwa sababu wewe ni mtukana matusi na kujibizana na wewe ni kujidhalilisha.Kwaheri
 
Mb

owe haitajiki kwa sasa huku majimboni hatupati hiyo ruzuku shughuli zote za chama sisi viongozi tunapitisha michango kwa wanachama.Mbowe atapata kura za kina boni yai na genge lake ila hatoboi
Lakini anaweza kuamua kufungua mkoba uliojaa maokoto.
Pili akizidiwa ataenda kwa mwenye nazo.
 
Amesh
Lakini anaweza kuamua kufungua mkoba uliojaa maokoto.
Pili akizidiwa ataenda kwa mwenye nazo.
Ameshaanza kuzisambaza kuna mdau kaweka thread hapa jamiiforums,yuko demu wa wenje na mwenzake anaitwa sauti wanazunguka kugawa pesa watu wamewarekodi zitaachiwa,pitia uzi hapa jf utauona.

Mimi nasubiri wanifuate na hizo pesa zao niwakimbize tunaendesha chama kwa shida sana huku majimboni
 
Lakini anaweza kuamua kufungua mkoba uliojaa maokoto.
Pili akizidiwa ataenda kwa mwenye nazo.
 
No evidence no right to speak.Huwezi kutuhumu tu bila ushahidi wowote ukaeleweka.Leo hii kuna watu wanatuhumu watu wa Lissu wananunua wajumbe na pia kuna wanaotuhumu upande wa Mbowe.Sasa je tutakurupuka tu kumtusi huyu au yule anatoa rushwa bila ushahidi? Tuache porojo za mtaani tysubiri wajumbe waamue nasi tuheshimu mawazo yao
Hata mimi nashangaa kumshutumu MTU bila ushaidi ,hawa wapenzi WA CHADEMA mitandaoni ni waajabu Sana wakiongozwa na kipenzi chao Lisu. Kwanza hawa sio wapiga Kura na hata kwenye uchaguzi sidhani kama wanapiga kwenye National election
 
Hata mimi nashangaa kumshutumu MTU bila ushaidi ,hawa wapenzi WA CHADEMA mitandaoni ni waajabu Sana wakiongozwa na kipenzi chao Lisu. Kwanza hawa sio wapiga Kura na hata kwenye uchaguzi sidhani kama wanapiga kwenye National election
Ndiyo maana tumewashauri badala ya kutukana wajikite kueneza sera za mgombea wanayempenda ili kuruhusu wajumbe wa mkutano mkuu kufanya maamuzi mazuri
 
Mawazo yake ameyatoa kidemokrasia.yaheshimiwe na siyo ujinga.
Mara nyingi mtu akijikita kwenye kutukana na kukashifu bila hoja anapuuzwa sana na hata mgombea wake anakuwa hana nguvu kwa wapiga kura
 
KWA NINI MBOWE HATAKI KUACHIA UENYEKITI WA CHADEMA

Mbowe ni Mwanachama pekee asiye na hasara ndani ya CHADEMA na mnufaika Mkuu japo wengi hawaoni kwa macho ya kawaida na anatumia mbinu zifuatazo;

1. Pesa yake yoyote ile anayoitumia ndani ya CHAMA inaandikwa kama mkopo na CHAMA kikipata fedha kwa njia ama ya Ruzuku, Chadema Digital ama Join the Chain analipwa kama mfadhiri wa chama.

Kama Mbowe yeye kila pesa yake anayoitumia ndani ya CHADEMA analipwa kama deni na anaitwa mfadhiri wa chama; sisi wengine anaotuita wabangaizaji ni nani anatulipa hizo chenji zetu za jero jero ambazo tunaamua kushinda ama kulala njaa ili tuki-support chama?

Hakika haya ni mambo ya aibu sana yasiyovumilika kwa kila mpenda mabadiliko wa nchi hii.

2. Mbowe ndiye Mwanachama pekee wa CHADEMA ama wa upinzani kwa sasa anayeweza kuipinga Serikali ya CCM hadharani; na ASITEKWE wala kuumizwa mwili wake hata kwa rungu ama jiwe na dola hii ya CCM ama huyu Mbowe hajawahi kupata athari yoyote ile kutokana na kukaa kwake gerezani kwa sababu; Mbowe akipelekwa gerezani inakuwa fursa ya kuweka sawa mipango yao na watu wa dola na mipango ikishakaa sawa anatolewa na anaambiwa aandike hasara zake zote alipwe na serikali na kweli analipwa.

Kama ni uongo, Mbowe atoke hadharani akatae kama hajalipwa Mabillioni ya Shilingi na Serikali ya CCM kama fidia ya hasara za kisiasa. Haya yote ni yanatokea hivi kwa sababu; Mbowe ni; mwenzao tangu enzi japo tulipoteza muda wetu mwingi sana kumuamini pasipo kujua.

Tazama Tundu Lissu anavyohangaika kudai hata hayo madai yake ya halali aliyotibiwa kama Mbunge baada ya kumuumiza vibaya sana kwa risasi za moto.

Kwamba, wapo tayari kumhonga Lissu Mabillioni ya Shilingi kupitia kwa Wenje na Abdul, lakini hawako tayari kumlipa gharama zake za matibabu ambazo ni halali yake kwa mujibu wa sheria za nchi.

3. Mbowe ni Mwanachama pekee ndani ya CHADEMA ambaye hajawahi kuishi nje ya nchi kama MKIMBIZI kutokana na usalama wake kuwa hatarini wala familia yake haijawahi kupata msukosuko kama ambavyo tunaona kwa wapinzani wa kweli walio committed kutaka CCM iondoke madarakani kama akina Godbless Lema na huyu Tundu Lissu.

Unahisi ni kwa nini Mbowe na familia yake hawajawahi kupata msukosuko serious wa kuwalazimu kuikimbia nchi ili hali na yeye anaikisoa serikali? Jibu liko Behind the Scene. Tuendelee kunywa mchuzi, nyama ziko chini.

Garatwa Francis,
Sauti ya wasio na Sauti.
29 Desemba, 2024.
 
MITAZAMO YA MAKUNDI (8) NANE YA WATU WANAOMUUNGA MKONO MBOWE NA SABABU ZAO.

Na; Garatwa Francis

Wakati umma unaomuunga mkono Tundu Lissu ukiwaza zaidi juu ya kumpata Tundu Lissu awe M/Kiti wa CHADEMA ili Chama kiweze kuinuka tena na kutoka kwenye mifuko ya CCM na Dola yao walikokificha kwa manufaa yao. Wengine wanawaza zaidi kuhusu tumbo zao na wengine wanawaza kuhusu vyeo vya madaraka wapewe na Mbowe kama walivyozoea. Hii hapa mitazamo na fikra za watu wanaomuunga mkono Mbowe. Mitazamo hii nimeigawa katika makundi (8) manane maana hawafanani mitazamo yao kutoka kundi moja kwenda lingine.

1. Wapo wanaovizia Ubunge wa Viti Maalum wakiamini kwamba; Mbowe ndiye ALFA na OMEGA kwa Mwanamke yeyote yule kuweza kupata Ubunge wa Viti Maalum ndani ya CHADEMA. Hawa huwezi kuwaambia chochote kuhusu Mbowe wakakuelewa maana vipaumbele vyao vyote kwenye chama hiki kuanzia kipaumbele cha kwanza mpaka cha mwisho ni Ubunge wa Viti Maalum tu. Hawa hawataki kujionyesha wako upande upi hata kama hawamtaki Mbowe; wanahisi kama kuna JINI MAKATA linaweza kuwanyima Ubunge wa Viti Maalum kama wakionekana kumuunga mkono Tundu Lissu.

2. Wapo wanaopata MIGAO ya hizo fedha chafu zinazosambazwa na Mama kupitia kwa Kibanda, Balile, Wenje na Abdul. Hawa nao huwaambii kitu. Mfano mzuri sana ni huyo Boni Yai.

3. Covid 19 wanapambana usiku na mchana Mbowe ashinde ili warudi tena kuvuna mafao kwenye SACCOS ya mjomba wao. (Mfano; Mdee, Bulaya, Matiko n.k)

4. Baadhi ya Maafisa na Wakurugenzi wa Makao Makuu ya Chama wanapambana ili Mbowe arudi waendelee kukikamua chama pale Makao Makuu kwa sababu akitoka mirija yote itazibwa na Lissu na fedha zitashuka kwenda kwenye wilaya na majimbo kusaidia shughuli za ujenzi wa chama.

5. Hao CCM wao wanaamini kwamba, Mbowe akiendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA; wanaendelea kunufaika na uporaji wa chaguzi kwa sababu huyu Mbowe wa sasa ni kibogoyo asiye na meno tena ya kung'ata. CCM wanamtetea kwa maneno kwamba; CHADEMA mchagueni tena Mbowe ana hekima na busara 😂

6. Serikali ya CCM nao wanaamini Mbowe akiendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wataipata nafuu ya kupumua hasa kwenye presha ya masuala mazito kama Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi; lakini pia hoja nzito za kuibua mambo ya hovyo wanayoyafanya kwenye serikali yao.

7. Wapo ambao ni wahuni na walevi wanaopenda starehe za Bar (Mfano; Ntobi Emmanuel na Henry Kilewo na Martin Maranja). Kwa hiyo, wao Chama sio kipaumbele ila zile starehe ambazo Mbowe amewazoesha na kuwafanya wabweteke wakidhani maisha washayamaliza.

8. Wapo wanaolipa fadhira kwa Mbowe kwa sababu za kuwasaidia kushinda chaguzi za maeneo yao kutokana na matumizi ya fedha chafu kutoka CCM alizokuwa anazipigia kelele Makamu M/Kiti wa Chama Tundu Lissu kila kuitwapo leo.

Garatwa Francis,
Sauti ya wasio na Sauti.
Dar es Salaam, Tanzania.
29 Desemba, 2024.
 
Kwako wewe ni ujinga lakini kwa wanademokrasia siyo ujinga.
Kuna wanademokrasia hapo au wapigaji tu?
Chama lazima kirudi kwa wanachama ili kukiokoa na kifo ambacho sasa kipo dhahiri. Huku site chama kimepoa na hakiaminiki tena. Ukweli huu mchungu kuna watu hataki kuusikia,kwao matumbo yao ni bora kuliko chama hiki.
 
Back
Top Bottom