Mpanda: Aliyeporwa udiwani amwaga machozi mbele ya Mbowe

Badili Heading la sivyo tutatofasri amelilia kuwa diwani, jambo ambalo lina maswali mengi sana.
Ionekane tu analia kwa dhuluma zilifanyika na uporaji wa mali.
Nitakuwa wa mwisho kuamini. Siiamini ccm na upinzani uliopo, waliungana na ccm kupora pesa za escrow kwa kumfanya mhusika toka ccm kuwa safi na awe rais wetu
 
Ndiyo lile jizi la kura la kihutu linateseka huko kuzimu. Ushenzi aliofanya hata shetani mwenyewe anashangaa
 
Mkuu 'zitto jr', huu ni mwandiko wako kweli?

Pamoja na kuweka hiyo "sosi" ya taarifa yenyewe, lakini kiuhalisia huu mwandiko siyo ule uliozoeleka. Labda tuseme ulikuwa na haraka na jambo fulani lililokuwa akilini mwako.

Sote tunajua uenda wazimu aliokuwa nao Magufuli; lakini taarifa hii hapa ni kama umemuunganisha tu nayo; au pengine kuna taarifa ambazo hukuziweka humu zinazoonyesha kwamba alitoa maagizo hayo yatekelezwe kuhusu hawa waTanzania waliokandamizwa?

Ni lazima sasa tuwe wakweli, haya mambo hakuyafanya yote Magufuli, pamoja na kwamba yeye ndiye aliyekuwa kinara. Leo hii tunao 'disciples' wake ambao sasa ni kama tunawapa heshima ya kiumalaika.
 
Asante sana kwa hii mistari michache.
Kwa upande wangu, wote walioshiriki kwa njia yoyote katika kuwakandamiza waTanzania wenzao kwa sababu yoyote ile; hata iwe ni ya kumfurahisha mkubwa wao, hawa wote siyo viongozi ninaowapa heshima hata kidogo; hata kama sasa hivi wanajinyesha kuwa na sura tofauti na ile ya wakati ule.
 
Utawala wa awamu ya 5 umepita. Cha kujiuliza ni je, tunafanya nini sasa ili kuziba kabisa mianya ya kuruhusu wasiofaa kuwa viongozi hawapati nafasi.
Njia pekee ni kuwaruhusu waTanzania watumie haki yao ya kumchagua yeyote wanayeona anafaa kwa maslahi yao; hata kama wakichagua kichaa mwingine, mradi wawe na uhuru wa kufanya hivyo, na ufahamu wa hatma ya nchi yao na wao wenyewe.
 
Bado najiuliza yule Aida alishinda kwenye mazingira gani?

Ni kwamba alisahaulika kwenye ile mipango ya awamu ya tano kama bahati tu, au waliamua kumtumia kama kigezo cha ule uchaguzi ulikuwa huru na haki?!
 
Baada ya Rais Yoweri Mseveni kumsifia JPM kwa ujasiri na maamuzi ya haraka mbele ya macho ya dunia, naona sasa mnatafuta pa kupitia.

JPM, Wabunge na Madiwani wote walikuwa wagombea, inakuwaje umshambulie JPM na kumuacha Mkutugenzi wa Uchaguzi?

Baada ya Prof wa Malawi, sasa ni Yoweri Mseveni na kesho tunasubiri mwingine wa Kimataifa
 
Hakika
 
Uongozi ni mzigo, unasaidiwa kubebewa mzigo unalia machozi, kweli? Au aliwekeza kwa ajili maisha yake binafsi kwenye kutafuta udiwani?
Inashangaza sana. Wamekutua mzigo badala ya kushukuru wewe unalia. Ha ha ha haa
 
Bado najiuliza yule Aida alishinda kwenye mazingira gani?

Ni kwamba alisahaulika kwenye ile mipango ya awamu ya tano kama bahati tu, au waliamua kumtumia kama kigezo cha ule uchaguzi ulikuwa huru na haki?!
Huyo ndiye aliyeshinda. Wengine wote walipigwa kihalali
 
Sinema hizi za Kitapeli


Udiwani ni wa kumaaga machozi[emoji1787]
Wewe ndiyo huelewi kabisa. Soma tena mada, labda utaelewa.

Hapa siyo suala la udiwani, ujumbe au ubunge, bali ni suala la dhuluma. Mtu anadhulumiwa haki yake ya kuchaguliwa, halafu anadhulumiwa mashamba yake, anawekwa jela, kwa sababu tu aligombea udiwani au alijulikana kuwa anamwunga mkono mgombea aliyechaguliwa na wananchi.

Mtawala kama huyo ina maana hata angewafahamu waliompa kura mgombea ambaye yeye hakumtaka angeweza kuwatesa kama alivyowafanyia wale alioweza kuwatambua.

Mungu atusaidie, alisaidie Taifa la Tanzania, tusipate tena utawala dhulumati wa kiwango hicho tena.
 
The departed was a real Beast, let him get barbecued in eternal fire.
 
Bado najiuliza yule Aida alishinda kwenye mazingira gani?

Ni kwamba alisahaulika kwenye ile mipango ya awamu ya tano kama bahati tu, au waliamua kumtumia kama kigezo cha ule uchaguzi ulikuwa huru na haki?!
Aida hakushinda, hata yeye anajua Hilo maana mawakala wake walitolewa nje maeneo mengi. Ila kwa kuwa alitangazwa mwishoni mwishoni ikabidi waachilie hata Jimbo Moja Ili hata mtu akisema ameibiwa watamuuliza " Mbona Aida kashinda". Hata kule Mtwara, Jimbo la Hawa Ghasia alizawadiwa mama wa CUF Ili kubalance kuwa hakukuwa na wizi.
 
Baada ya Rais Yoweri Mseveni kumsifia JPM kwa ujasiri na maamuzi ya haraka mbele ya macho ya dunia, naona sasa mnatafuta pa kupitia.

Baada ya Prof wa Malawi, sasa ni Yoweri Mseveni na kesho tunasubiri mwingine wa Kimataifa
Afrika Kila mtu akifariki anageuka mzuri, hata Nkuruzinza anasifiwa Kila siku ilihali alikua zero tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…