Mpanda: Aliyeporwa udiwani amwaga machozi mbele ya Mbowe

Mpanda: Aliyeporwa udiwani amwaga machozi mbele ya Mbowe

"Kazi zote ni za Rais, sisi tunamsadia tu..." Spika Tulia.

Unatambua vizuri madaraka ya Rais kwa Katiba ya sasa ni ya kifalme, ya "kimungu".
Rais ni kila kitu. Husikii hata fedha za umma au miradi ya umma husemwa ni ya Rais?

Kwa hiyo hakuna jambo lolote ovu au baya ambalo hayati Magufuli hakuhusika nalo (iwe directly au indirectly).
Mimi hayo siyaamini, kwa hiyo usinihusishe nayo.
Ninazo akili timamu na siku zote sitaazima akili toka kwa binaadam mwingine yeyote.

Sasa ukiniuliza nitafanya nini na hizi akili zangu, moja ni kuwa sitakubaliana nawe, na kama unanilazimisha nikubaliane nawe, nitakataa kwa njia yoyote itakayoniwezesha kukataa.
That's my bottom line.
 
"Kazi zote ni za Rais, sisi tunamsadia tu..." Spika Tulia.

Unatambua vizuri madaraka ya Rais kwa Katiba ya sasa ni ya kifalme, ya "kimungu".
Rais ni kila kitu. Husikii hata fedha za umma au miradi ya umma husemwa ni ya Rais?

Kwa hiyo hakuna jambo lolote ovu au baya ambalo hayati Magufuli hakuhusika nalo (iwe directly au indirectly).
Upo sahihi kabisa
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Hao wamefanyiwa hivyo na ccm ipi wakati Magufuli hayupo?
CCM ya Samia inawanyoosha sukuma gang. So hakuna aliye salama ni muhimu wote tudai katiba mpya Ili hata akiingia Mwenyekiti mpya wa CCM asiwashughulikie eti kisa tu mnamkosoa.

Najua kufikia 2025 tutaongea lugha Moja maana hakuna sukuma gang atapewa fomu ya uongozi.
 
Katili kuliko yule alierusha bomu na kuua watu watano pale soweto arusha kwenye mkutano wa machadema?
Hiyo ilikua kazi ya Mwigulu tokea aondolewe CCM kuingia serikalini hatukuona Tena mauaji kwenye kampeni
 
kwa hiyo analia kwa kuwa alikosa mshahara na posho za udiwani. Ajiajili tu kwenye kilimo mbona huko ardhi nzuri.
Hapana analia sababu ya unyanyasaji kama wenzie kupora viwanja, kufungwa jela miaka 4 n.k..Udiwani hauna pesa kiasi mtu alie, yeye ameumia sababu ya udhalilishaji aliopitia kisa Yuko CHADEMA.
 
Wengi wa viongozi hao walioshiriki kufanya maovu, wengi wao walitegemea utashi wao wenyewe.
Mbona huo utashi hatuoni kwa Sasa? Mfano Lissu mbona anaongea kuliko hata wakati wa JPM ila hajapewa kesi ya uchochezi? Ni hivi wote hao walikua wanafanyia kazi attitude ya JPM.

Angalia hata majaji wameachia wanachadema zaidi ya 460 ila ni mahakama hizo hizo ziliwafunga kipindi Cha JPM.

So hakuna utashi binafsi ndio maana kina Kabudi, Polepole na Bashiru wote walikua wajumbe wa Tume ya Warioba ila ilibidi wakane utashi wao wa kudai katiba Ili walinde vibarua vyao
 
Hiyo ilikua kazi ya Mwigulu tokea aondolewe CCM kuingia serikalini hatukuona Tena mauaji kwenye kampeni
Sasa hao waliofungwa kwanini umlaumu Magufuli?
Hata Mwangosi ilikuwa kazi ya Mwigulu?
Ulimboka ilikuwa kazi ya mwigulu?
Mawazo ilikuwa kazi ya mwigulu?

Kumbe mwigulu alikuwa rais!
 
We jamaa unampenda Samia hadi unakuwa kipofu!

Hapo juu umesema bomu lililouwa watu 5 kwenye mkutano wa chadema ilikuwa kazi ya Mwigulu wala siyo Jk aliekuwa rais wakati huo, hapa tena unamlaumu Magufuli moja kwa moja kwamba vile vitendo vilitokea kulingana na tune ya Rais aliyepo madarakani.

Hapa inawezekana wewe ni muislamu unatetea wavaa kobazi wenzio
 
CCM ya Samia inawanyoosha sukuma gang. So hakuna aliye salama ni muhimu wote tudai katiba mpya Ili hata akiingia Mwenyekiti mpya wa CCM asiwashughulikie eti kisa tu mnamkosoa.

Najua kufikia 2025 tutaongea lugha Moja maana hakuna sukuma gang atapewa fomu ya uongozi.
Nitajie sukuma gang alienyooshwa na kanyooshwaje?
 
Hiyo ilikua kazi ya Mwigulu tokea aondolewe CCM kuingia serikalini hatukuona Tena mauaji kwenye kampeni
Hii inanikumbusha yale yaliyowatokea CHADEMA kule Arusha walipolipukiwa na bomu, akina Mbowe wakaponea chupu chupu, lakini yule mdada (Oooh, hata jina hakumbukwi tena hata huko CHADEMA kwenyewe?)
 
We jamaa unampenda Samia hadi unakuwa kipofu!

Hapo juu umesema bomu lililouwa watu 5 kwenye mkutano wa chadema ilikuwa kazi ya Mwigulu wala siyo Jk aliekuwa rais wakati huo, hapa tena unamlaumu Magufuli moja kwa moja kwamba vile vitendo vilitokea kulingana na tune ya Rais aliyepo madarakani.

Hapa inawezekana wewe ni muislamu unatetea wavaa kobazi wenzio
Niajabu kidogo, lakini ninakubaliana na wewe, siku hizi mkuu 'zitto junior' kabadilika sana; na wasiwasi wangu ni huo huo juu ya Mbowe pia.
 
Mbona huo utashi hatuoni kwa Sasa? Mfano Lissu mbona anaongea kuliko hata wakati wa JPM ila hajapewa kesi ya uchochezi? Ni hivi wote hao walikua wanafanyia kazi attitude ya JPM.

Angalia hata majaji wameachia wanachadema zaidi ya 460 ila ni mahakama hizo hizo ziliwafunga kipindi Cha JPM.

So hakuna utashi binafsi ndio maana kina Kabudi, Polepole na Bashiru wote walikua wajumbe wa Tume ya Warioba ila ilibidi wakane utashi wao wa kudai katiba Ili walinde vibarua vyao
Fair enough.
Sina uwezo wa kueleza ninachokilenga hapa kuhusu "utashi" wa kiongozi katika ngazi yoyote ile anayoitumikia; kwa sababu katika jamii viongozi wa namna hiyo wanakuwa ni wachache sana, na inakuwa mbaya zaidi inapotokea kuwa kwenye mfumo wa utawala wa aina ya tulio nao.

Hata hivyo, umenipa 'assignment' hapa nisiyoweza kuikwepa, kwa sababu najua ulichoandika hapa siyo sahihi, lakini sina jibu maalum la kukupa uelewe ninachokilenga hasa ni nini.

Kiongozi huko wilayani anamfunga mpinzani kwa vile tu kumfurahisha mkuu wake na kuweka utashi wake pembeni? Halafu tunahamishia lawama kwa mkuu wake kwa vile ndiye anayelengwa kufurahishwa? Halafu tunakuja hapa na kusema mtu huyo ni kiongozi?
Sina uwezo wa kujibu hoja yako kwa sasa hivi mkuu 'zitto junior'.

Tuendelee na mengine.
 
Mkuu nimeshaeleza kwamba subordinates wanafanya kazi kulingana na attitude ya kiongozi aliyepo juu. Mfano JPM alipokua anafoka foka basi na DC, DAS n.k walikua nao wanafoka foka na kutumbua wanavyojisikia.

So JPM anaweza asihusike Moja kwa Moja ila kitendo Cha yeye kuweka attitude ya kutotaka wapinzani hapo lazima wakurugenzi waibe na wapore uchaguzi.

Mfano Akiwa kule Busega na Bunda aliwatishia kuwa wasipomchagua au wakimpa wabunge na madiwani wa upinzani basi wasije kulilia Barabara na Mradi wa Maji!! Sasa kwa attitude hiyo na msimamo Kuna mkurugenzi atakubali akose pesa za miradi kisa upinzani?

Mama Samia kaonyesha kuwa anapenda demokrasia na upinzani ndio maana hata Polisi husikii wanakamata magazeti, wanaharakati, wachochezi n.k. Polisi ni wale wale, mahakama ni zile zile ila wote Wanafuata attitude ya Rais anayekuepo madarakani.
Wee weee ishia hapo hapo mama nani kaonesha nini? Unaijua CCM kwa uchu wa madaraka wewe?Wanapora ushindi hadi wa wanawake.
Hawapo tayari kutoka kwa hiari yao hukumskia Pole pole anasema unaijua Vi eiti wewe pia pole pole anasema CCM kuna wahuni.
 
Niajabu kidogo, lakini ninakubaliana na wewe, siku hizi mkuu 'zitto junior' kabadilika sana; na wasiwasi wangu ni huo huo juu ya Mbowe pia.
Mbona ipo wazi Samia is better than JPM kwenye demokrasia. Ukweli usemwe jamani, hivi enzi za JPM BAWACHA wangeweza kuandamana Hadi ofisi za bunge?
 
Sasa hao waliofungwa kwanini umlaumu Magufuli?
Hata Mwangosi ilikuwa kazi ya Mwigulu?
Ulimboka ilikuwa kazi ya mwigulu?
Mawazo ilikuwa kazi ya mwigulu?

Kumbe mwigulu alikuwa rais!
Ukatili haukuwepo enzi za JK kwa extent ya JPM Hilo lipo wazi.

Mauaji kwenye kampeni yalitokea enzi Mwigulu ndio naibu Katibu mkuu ila tokea ahamishwe walau matukio ya mauaji yaliisha.

Mwangosi ni ukatili wa Polisi Wala sio order za JK na uonevu wa Polisi ulikuwepo tokea uhuru mpaka Leo hii ndio maana Samia amesema watalifumua jeshi.

Tunapomlaumu Rais sio sababu anatoa order ila attitude yake (Nakosa neno zuri la kiswahili) ndio unafanyiwa kazi na wasaidizi wake.

Mfano Rais akiwa mkali, basi mpaka ma-DC wanaigiza ukali ukali. Samia ameonekana mtu wa kufanya kazi bila kufoka foka na ndio tabia hiyo hiyo wameirithi wasaidizi wake huko chini.

So JPM alipoonyesha attitude ya chuki juu ya upinzani ikasababisha na hao wa chini wa copy Ili waendane na utashi wake. Mind you wote waliosulubu wapinzani walipandishwa vyeo je unategemea nani angeacha kufanya ukatili?

NB: Mawazo aliuwawa awamu ya JPM

Cc Kalamu
 
Katika ziara ya Chadema (Operation +255) huko mpanda, Kuna tukio limeniacha na majonzi sana. Mgombea udiwani wa Chadema 2020, mwanamama shupavu alimwaga chozi akikumbuka ukatili wa JPM.

Mgombea huyu aliwekewa pingamizi so hakufanya kampeni muda mrefu, kama haitoshi aliposhinda udiwani (Fomu za matokeo anazo) hakutangazwa mshindi kama ilivyokua katika kata zote Tanzania.

Kilichoniuma zaidi, aliyekuwa campaign manager wake aliporwa kiwanja na Serikali ya Kijiji kisa tu alimsupport mama huyu. Kama hiyo haitoshi aliekuwa diwani wa kata ya Isengule 2015 alifungwa gerezani kwa zaidi ya miaka 4 kisa kuwa mpinzani!!

Aisee kama nchi tulipita kipindi kigumu sana, mtu ushampora kata Sasa si yameshaisha Bado tu hutosheki unaenda kubeba shamba na diwani mstaafu akatupwa jela. WaTanzania tushirikiane kudai katiba mpya na tume huru Ili hizi tabia za kishetani zisijirudie Tena.

Video hapa chini

Source: Mwananchi Digital
Chadema mmekosa ajenda kabisa au sijui mmelambishwa asali siasa zenu ni kulia lia na kumlaumu Magufuli mkitafuta huruma ya wananchi na Mama Samia
 
We jamaa unampenda Samia hadi unakuwa kipofu!

Hapo juu umesema bomu lililouwa watu 5 kwenye mkutano wa chadema ilikuwa kazi ya Mwigulu wala siyo Jk aliekuwa rais wakati huo, hapa tena unamlaumu Magufuli moja kwa moja kwamba vile vitendo vilitokea kulingana na tune ya Rais aliyepo madarakani.

Hapa inawezekana wewe ni muislamu unatetea wavaa kobazi wenzio
Baada ya malalamiko mbona Mwigulu aliondolewa kwenye chama na tukiwa wakweli matukio ya tindikali, mauaji, kuchomana visu yakapotea kabisa Hadi JPM aliposhinda ndio tukashuhudia kifo cha kamanda Mawazo.

Ila kwa JPM ndio alikua anawapandisha vyeo mfano Mahera, Muro, Mnyeti, Makonda n.k yaani ukiwakandamiza tu wapinzani ndio unapata favor ya Rais.

Ndio maana nasema matukio ya wapinzani kuuwawa au kuteswa yanaendana sana na attitude and perceptions za Rais aliyepo madarakani.
 
Chadema mmekosa ajenda kabisa au sijui mmelambishwa asali siasa zenu ni kulia lia na kumlaumu Magufuli mkitafuta huruma ya wananchi na Mama Samia
Poleni sana Sukuma gang tukutane kwenye sanduku la kura 2025 ndio mtakapo elewa kama tulikuwa tunalialia au tunajenga chama.
 
Back
Top Bottom