Kumbe hufahamu kilichotokea?
Wakati majimbo yote ya uchaguzi wanakaribia kumaliza kuwatangaza waliowateya kuwa wabunge, Kabudi alienda kumweleza JPM kuwa Serikali itakosa pesa zaidi ya trilioni 1 toka Jumuia ya Madola kila mwaka, ya kusaidia bajeti ya Serikali kwa sababu sharti la ile pesa ni lazima uwe na kambi rasmi ya upinzani bungeni, na kamati 2 za Bunge, LAC, PAC ziongozwe na wapinzani. Na kwamba ili kuwe na kambi rasmi ya upinzani bungeni ni lazima chama cha upinzani kinachounda kambi rasmi ya upinzani kiwe kimefikisha asilimia 14 ya wabunge, asilimia ambayo haiwezi kufikiwa na wabunge pekee wa viti maalum ambao CHADEMA ingepata.
JPM akaamrisha kuwa majimbo yote yaliyobakia wapewe CHADEMA. Bahati mbaya mpaka muda huo lilikuwa limebakia jimbo moja tu la huyo dada, akatangazwa mbunge. JPM akatoa maelekezo kuwa kwa vile lazima CHADEMA wataenda mahakamani, mahakama itengue matokeo ya uchaguzi kwenye baadhi ya majimbo ili 14% ipatikane. Bahati mbaya kwake, hakuna mgombea wa CHADEMA aliyeenda mahakamani kupinga matokeo kama alivyotarajia. Baada ya hapo ndipo zile mbinu za kuwapeleka bungeni akina Mdee zikaanza. Kilichotarajiwa ni baadhi ya walioteuliwa ubunge kulazimishwa kujiuzulu baada ya kupewa nafasi kwenye Serikali, hasa ubalozi ili uchaguzi urudiwe kwenye majimbo watakayoyaacha, wapinzani wapitishwe, hata kama watakuwa ni wapinzani bandia, ilimradi tu 14% ipatikane.
Lilifanikiwa moja tu la akina Mdee, mengine hayakufikiwa kwa kuwa siku zake za kuishi Duniani, kwa hesabu ya Muumbaji wetu, zilikuwa zimekwisha. Pesa ya bure ya Jumuiya ya Madola tukaikosa mpaka leo. Tukawa tumekosa pesa ya msaada ya Jumuiya ya Madola na ya MCC. Ndiyo maana kwa sasa hakuna namna, ni lazima tukope kwa bidii kuziba mapengo.