Mpanda: Aliyeporwa udiwani amwaga machozi mbele ya Mbowe

Mpanda: Aliyeporwa udiwani amwaga machozi mbele ya Mbowe

Ukatili haukuwepo enzi za JK kwa extent ya JPM Hilo lipo wazi.

Mauaji kwenye kampeni yalitokea enzi Mwigulu ndio naibu Katibu mkuu ila tokea ahamishwe walau matukio ya mauaji yaliisha.

Mwangosi ni ukatili wa Polisi Wala sio order za JK na uonevu wa Polisi ulikuwepo tokea uhuru mpaka Leo hii ndio maana Samia amesema watalifumua jeshi.

Tunapomlaumu Rais sio sababu anatoa order ila attitude yake (Nakosa neno zuri la kiswahili) ndio unafanyiwa kazi na wasaidizi wake.

Mfano Rais akiwa mkali, basi mpaka ma-DC wanaigiza ukali ukali. Samia ameonekana mtu wa kufanya kazi bila kufoka foka na ndio tabia hiyo hiyo wameirithi wasaidizi wake huko chini.

So JPM alipoonyesha attitude ya chuki juu ya upinzani ikasababisha na hao wa chini wa copy Ili waendane na utashi wake. Mind you wote waliosulubu wapinzani walipandishwa vyeo je unategemea nani angeacha kufanya ukatili?

NB: Mawazo aliuwawa awamu ya JPM

Cc Kalamu
mawazo aliuawa tarehe ngapi na Magufuli aliapishwa kuwa rais tarehe ngapi?

Yani ukatili uliotokea enzi za JK siyo wake ila uliotokea enzi za Magufuli ni wake!

Hapa kuna mawili:
1. Unasumbuliwa na udini
2. Una utindio wa ubongo
 
Baada ya malalamiko mbona Mwigulu aliondolewa kwenye chama na tukiwa wakweli matukio ya tindikali, mauaji, kuchomana visu yakapotea kabisa Hadi JPM aliposhinda ndio tukashuhudia kifo cha kamanda Mawazo.

Ila kwa JPM ndio alikua anawapandisha vyeo mfano Mahera, Muro, Mnyeti, Makonda n.k yaani ukiwakandamiza tu wapinzani ndio unapata favor ya Rais.

Ndio maana nasema matukio ya wapinzani kuuwawa au kuteswa yanaendana sana na attitude and perceptions za Rais aliyepo madarakani.
Baki na ujinga wako mkuu!

Ccm hii inawapenda sana! Baada ya kuondoka Magufuli mtashinda kwa kishindo
 
mawazo aliuawa tarehe ngapi na Magufuli aliapishwa kuwa rais tarehe ngapi?

Yani ukatili uliotokea enzi za JK siyo wake ila uliotokea enzi za Magufuli ni wake!

Hapa kuna mawili:
1. Unasumbuliwa na udini
2. Una utindio wa ubongo
Wala sio udini ila hakuna Rais alitukanwa kama JK, kama angekua katili basi kina Dr Slaa wangeuwawa zamani sana au kupewa kesi za uhujumu uchumi.

Huwezi linganisha ukiukwaji haki za binadamu enzi za JK na ukatili wa JPM.

Havifanani kabisa hata asiye mdini anajua hilo
 
Baki na ujinga wako mkuu!

Ccm hii inawapenda sana! Baada ya kuondoka Magufuli mtashinda kwa kishindo
CCM haitupendi ila Mama Samia anajitahidi walau kuwa na utu kuliko mtangulizi wake.

Mama Samia mwenyewe amekiri kuwa wahafidhina kama nyie mnampinga kisa amegoma kuwafanyia ukatili wapinzani.
 
Mbona ipo wazi Samia is better than JPM kwenye demokrasia. Ukweli usemwe jamani, hivi enzi za JPM BAWACHA wangeweza kuandamana Hadi ofisi za bunge?
WaTanzania hawashibi "Demokrasia"!

Ninakushangaa sana mkuu 'zitto junior' kufumbwa macho na akili kiasi hiki.
WaTanzania wametoka kwenye tanuru la moto chini ya Magufuli, na sasa wamo ndani ya chungu wanapikika sawa sawa, halafu watu wenye upeo kiasi chako wanashangilia?
Maovu pekee ni huko kuuliwa kwa risasi na kuwekwa jela alikokufanya Magufuli, lakini nchi kuporwa mali na uozo chungu nzima hiyo inakuwa ni heri?
Serikali isiyokuwa na mipango ya kusimamia chochote kifanyike kwa ufanisi na sisi wenyewe, lakini inaona ni bora zaidi tukakodi watu waje hapa kuvuna, bila hata ya sisi kujibidisha kivyovyote kuhakikisha wavunaji watavuna kilicho haki yao nasi kubaki na haki yetu; hali hiyo ndiyo inayokusisimua wewe?

TICTS kakaa pale zaidi ya miaka 20, hatukujifunza chochote katika muda wote huo, sasa tunatafuta tena wengine waje, sisi tukiwepowepo tu!

Wizi sasa ndiyo imekuwa sifa kuu inayoheshimiwa hata na vijana wetu wadogo mashuleni? Hili ni taifa la namna gani hili?

Mkuu 'zitto junior', natambua sasa kwamba tumo kwenye nyakati za ku'score points' katika majadiliano yetu humu JF. Tumetoka kwenye zile nyakati za majadiliano ya ukweli wa tunayoyaamini sisi wenyewe kuwa ni sahihi.
 
Back
Top Bottom