Mpanda: Aliyeporwa udiwani amwaga machozi mbele ya Mbowe

JPM, Wabunge na Madiwani wote walikuwa wagombea, inakuwaje umshambulie JPM na kumuacha Mkutugenzi wa Uchaguzi?
Hakuna mkurugenzi anaweza fanya hayo bila Baraka kutoka juu kwamba awatese wapinzani. Hivi kwa Mama Samia umeona kiongozi yoyote anatumia style ya ziara ya kushtukiza alafu anatumbua tumbua tu?

Hakuna, why? Sababu wanaona aliyepo kwenye kiti Hana hizo tabia so na wao wanaogopa kuwa "wakali wakali".

So hao wakurugenzi utawaonea tu ila wanafanya kazi kwa order za Rais. JPM ndio anabeba lawama za uchaguzi ule, hakukua na haja ya kupora wakati angeweza kuiba za kwake za Urais akaachia wananchi waamue wabunge wake.
 
Uongozi ni mzigo, unasaidiwa kubebewa mzigo unalia machozi, kweli? Au aliwekeza kwa ajili maisha yake binafsi kwenye kutafuta udiwani?
Hapana analia sababu ya madhila aliyopata baada ya uchaguzi. Yaani kawekwa ndani, campaign manager kaporwa kiwanja, diwani mwenzake kafungwa miaka 4 alafu unategemea asiumie.
 
Bado najiuliza yule Aida alishinda kwenye mazingira gani?

Ni kwamba alisahaulika kwenye ile mipango ya awamu ya tano kama bahati tu, au waliamua kumtumia kama kigezo cha ule uchaguzi ulikuwa huru na haki?!
Kumbe hufahamu kilichotokea?

Wakati majimbo yote ya uchaguzi wanakaribia kumaliza kuwatangaza waliowateya kuwa wabunge, Kabudi alienda kumweleza JPM kuwa Serikali itakosa pesa zaidi ya trilioni 1 toka Jumuia ya Madola kila mwaka, ya kusaidia bajeti ya Serikali kwa sababu sharti la ile pesa ni lazima uwe na kambi rasmi ya upinzani bungeni, na kamati 2 za Bunge, LAC, PAC ziongozwe na wapinzani. Na kwamba ili kuwe na kambi rasmi ya upinzani bungeni ni lazima chama cha upinzani kinachounda kambi rasmi ya upinzani kiwe kimefikisha asilimia 14 ya wabunge, asilimia ambayo haiwezi kufikiwa na wabunge pekee wa viti maalum ambao CHADEMA ingepata.

JPM akaamrisha kuwa majimbo yote yaliyobakia wapewe CHADEMA. Bahati mbaya mpaka muda huo lilikuwa limebakia jimbo moja tu la huyo dada, akatangazwa mbunge. JPM akatoa maelekezo kuwa kwa vile lazima CHADEMA wataenda mahakamani, mahakama itengue matokeo ya uchaguzi kwenye baadhi ya majimbo ili 14% ipatikane. Bahati mbaya kwake, hakuna mgombea wa CHADEMA aliyeenda mahakamani kupinga matokeo kama alivyotarajia. Baada ya hapo ndipo zile mbinu za kuwapeleka bungeni akina Mdee zikaanza. Kilichotarajiwa ni baadhi ya walioteuliwa ubunge kulazimishwa kujiuzulu baada ya kupewa nafasi kwenye Serikali, hasa ubalozi ili uchaguzi urudiwe kwenye majimbo watakayoyaacha, wapinzani wapitishwe, hata kama watakuwa ni wapinzani bandia, ilimradi tu 14% ipatikane.

Lilifanikiwa moja tu la akina Mdee, mengine hayakufikiwa kwa kuwa siku zake za kuishi Duniani, kwa hesabu ya Muumbaji wetu, zilikuwa zimekwisha. Pesa ya bure ya Jumuiya ya Madola tukaikosa mpaka leo. Tukawa tumekosa pesa ya msaada ya Jumuiya ya Madola na ya MCC. Ndiyo maana kwa sasa hakuna namna, ni lazima tukope kwa bidii kuziba mapengo.
 
Mkuu nimeshaeleza kwamba subordinates wanafanya kazi kulingana na attitude ya kiongozi aliyepo juu. Mfano JPM alipokua anafoka foka basi na DC, DAS n.k walikua nao wanafoka foka na kutumbua wanavyojisikia.

So JPM anaweza asihusike Moja kwa Moja ila kitendo Cha yeye kuweka attitude ya kutotaka wapinzani hapo lazima wakurugenzi waibe na wapore uchaguzi.

Mfano Akiwa kule Busega na Bunda aliwatishia kuwa wasipomchagua au wakimpa wabunge na madiwani wa upinzani basi wasije kulilia Barabara na Mradi wa Maji!! Sasa kwa attitude hiyo na msimamo Kuna mkurugenzi atakubali akose pesa za miradi kisa upinzani?

Mama Samia kaonyesha kuwa anapenda demokrasia na upinzani ndio maana hata Polisi husikii wanakamata magazeti, wanaharakati, wachochezi n.k. Polisi ni wale wale, mahakama ni zile zile ila wote Wanafuata attitude ya Rais anayekuepo madarakani.
 
Aisee walifanya miscalculation kubwa sana, imagine Chadema ilikua na kura zaidi ya million 3 za wagombea ubunge ila eti wameshinda Jimbo Moja!! Kuna vitu vilikua vya ajabu sana ila 2020 ilivuka mipaka ndio maana wakaona enough is enough!!!
 
chachema ni wanafiki sana kazi yao ni kupanda mbegu za ukuda hii 255 ni ushuzi
 
Hakuna mtu anayeweza kupinga ujasiri wa Magufuli. Hata Lisu aliwahi kulitamka hilo.

Fikiria mtu anakata na kufuta 75% ya majina ya wagombea wa ubunge wa chama chake waliopitishwa na wajumbe, na kuwapacika watu wake aliowataka!! Mtu ambaye anatoa amri kuwa wakurugenzi wa Halmashauri wasiwatangaze wapinzani kuwa wabunge hata kama watakuwa wamechaguliwa na wananchi, na anafanya hayo yote bila ya hofu ya wanachama wa chama chake, bila hofu ya mamilioni ya watanzania wapiga kura, unadhani huo ni ujasiri wa kiwango gani?

Ujasiri ule wa Magufuli, tena katika kutenda uovu, siyo rahisi mtu wa kawaida kuwa nao. Kwenye ujasiri, Magufuli angepata 100% kwa sababu tu hakuna asilimia nyingine zaidi ya hiyo. Tatizo lake kubwa, ujasiri wake kwa sehemu kubwa ulikuwa kwenye mambo mabaya. Ujasiri wake ungekuwa kwenye mambo mazuri pekee, ungekuwa na faida kubwa.
 
Kwamba ina maana walikurupuka kufanya jambo bila kufahamu madhara yake?

Dah!.
 
Kumbe ndio maana kuna baadhi ya wabunge Chadema wanapinga uwepo wa Aida bungeni, wanamuona nae ni sehemu ya ile mipango ovu ya wakati ule.

Lakini bado inawezekana huyu dada alishinda kihalali, binafsi ningependa kuifahamu nguvu ya uungwaji mkono aliyokuwa nayo wakati wa kampeni, nione kama itashabihiana na ushindi wake.

Wakati mwingine naona kusema hakushinda kihalali ni kama ku underestimate nguvu ya Chadema, hasa maeneo ya mijini ambako inafahamika vyema, hivyo ajali iliyotokea ikamfanya atangazwe mshindi tofauti na wenzie walioshinda kihalali lakini wakaporwa ushindi wao, isionekane kosa lake Aida.
 
Kwamba ina maana walikurupuka kufanya jambo bila kufahamu madhara yake?

Dah!.
Yeah hawakumshauri vizuri, Sasa wamegundua madhara yake ikiwa too late ikabidi tu waokoteze. Kule zenji Kuna mbunge wa CCM alijiuzulu alafu uchaguzi ukafanyika akashinda ACT!! yote hiyo ilikua ni kujaziliza jaziliza Ili namba zibalance kwa wafadhili.
 
Museveni kumsifia Dikteta mwenzake kuna ajabu gani ?

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Hao wamefanyiwa hivyo na ccm ipi wakati Magufuli hayupo?
 
Katili kuliko yule alierusha bomu na kuua watu watano pale soweto arusha kwenye mkutano wa machadema?
 
kwa hiyo analia kwa kuwa alikosa mshahara na posho za udiwani. Ajiajili tu kwenye kilimo mbona huko ardhi nzuri.
 
Sijawahi kupata maelezo ya kuweza kuaminiwa kuhusu jambo hili hadi leo zaidi ya hii taarifa uliyoweka hapa.

Kuna maswali ndani yake, lakini bado ni habari inayojisimamia yenyewe kikamilifu.
 
Sina lolote ninaloweza kumkingia kifua Magufuli, isipokuwa katika mambo machache aliyoyasimamia na kwa bahati mbaya nayo kwa kiasi kikubwa kayasimamia vibaya kwa sababu ya udhaifu wa tabia yake.

Hapa tunazungumzia viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini na kwenye chama. Ndiyo, ni kweli hawa viongozi iliwalazimu kufanya mambo ambayo yasingekuwa kinyume cha aliyotaka mkuu wao; lakini hadi kuumiza watu, kama huyo aliyewekwa ndani ya jela kwa miaka?
Binaadam yeyote anao utashi, ambao hawezi kuukiuka kwa shurti tu kutoka kwa mtu mwingine yeyote.
Wengi wa viongozi hao walioshiriki kufanya maovu, wengi wao walitegemea utashi wao wenyewe.
 
Wisdom 👏
 
Asante sana Bams.

Narudia tena, na alaaniwe huko aliko!

Aliiharibu nchi yetu, aliharibu maisha, uchumi, biashara na kila kitu chema au cha haki.
Ni wajibu wetu sisi wapenda haki kusimama imara na kuchukua nafasi zetu ili maovu yale yasikae yarudiwe kamwe Tanzania
 
"Kazi zote ni za Rais, sisi tunamsadia tu..." Spika Tulia.

Unatambua vizuri madaraka ya Rais kwa Katiba ya sasa ni ya kifalme, ya "kimungu".
Rais ni kila kitu. Husikii hata fedha za umma au miradi ya umma husemwa ni ya Rais?

Kwa hiyo hakuna jambo lolote ovu au baya ambalo hayati Magufuli hakuhusika nalo (iwe directly au indirectly).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…