Mpanda: Aliyeporwa udiwani amwaga machozi mbele ya Mbowe

mawazo aliuawa tarehe ngapi na Magufuli aliapishwa kuwa rais tarehe ngapi?

Yani ukatili uliotokea enzi za JK siyo wake ila uliotokea enzi za Magufuli ni wake!

Hapa kuna mawili:
1. Unasumbuliwa na udini
2. Una utindio wa ubongo
 
Baki na ujinga wako mkuu!

Ccm hii inawapenda sana! Baada ya kuondoka Magufuli mtashinda kwa kishindo
 
mawazo aliuawa tarehe ngapi na Magufuli aliapishwa kuwa rais tarehe ngapi?

Yani ukatili uliotokea enzi za JK siyo wake ila uliotokea enzi za Magufuli ni wake!

Hapa kuna mawili:
1. Unasumbuliwa na udini
2. Una utindio wa ubongo
Wala sio udini ila hakuna Rais alitukanwa kama JK, kama angekua katili basi kina Dr Slaa wangeuwawa zamani sana au kupewa kesi za uhujumu uchumi.

Huwezi linganisha ukiukwaji haki za binadamu enzi za JK na ukatili wa JPM.

Havifanani kabisa hata asiye mdini anajua hilo
 
Baki na ujinga wako mkuu!

Ccm hii inawapenda sana! Baada ya kuondoka Magufuli mtashinda kwa kishindo
CCM haitupendi ila Mama Samia anajitahidi walau kuwa na utu kuliko mtangulizi wake.

Mama Samia mwenyewe amekiri kuwa wahafidhina kama nyie mnampinga kisa amegoma kuwafanyia ukatili wapinzani.
 
Mbona ipo wazi Samia is better than JPM kwenye demokrasia. Ukweli usemwe jamani, hivi enzi za JPM BAWACHA wangeweza kuandamana Hadi ofisi za bunge?
WaTanzania hawashibi "Demokrasia"!

Ninakushangaa sana mkuu 'zitto junior' kufumbwa macho na akili kiasi hiki.
WaTanzania wametoka kwenye tanuru la moto chini ya Magufuli, na sasa wamo ndani ya chungu wanapikika sawa sawa, halafu watu wenye upeo kiasi chako wanashangilia?
Maovu pekee ni huko kuuliwa kwa risasi na kuwekwa jela alikokufanya Magufuli, lakini nchi kuporwa mali na uozo chungu nzima hiyo inakuwa ni heri?
Serikali isiyokuwa na mipango ya kusimamia chochote kifanyike kwa ufanisi na sisi wenyewe, lakini inaona ni bora zaidi tukakodi watu waje hapa kuvuna, bila hata ya sisi kujibidisha kivyovyote kuhakikisha wavunaji watavuna kilicho haki yao nasi kubaki na haki yetu; hali hiyo ndiyo inayokusisimua wewe?

TICTS kakaa pale zaidi ya miaka 20, hatukujifunza chochote katika muda wote huo, sasa tunatafuta tena wengine waje, sisi tukiwepowepo tu!

Wizi sasa ndiyo imekuwa sifa kuu inayoheshimiwa hata na vijana wetu wadogo mashuleni? Hili ni taifa la namna gani hili?

Mkuu 'zitto junior', natambua sasa kwamba tumo kwenye nyakati za ku'score points' katika majadiliano yetu humu JF. Tumetoka kwenye zile nyakati za majadiliano ya ukweli wa tunayoyaamini sisi wenyewe kuwa ni sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…