Mpangaji agoma kuhama baada ya mkataba kuisha. Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?

Jamaa punguani kweli huyo
 
Rudisha fedha ya watu haraka. Security deposit ndio upuuzi gani
 
Umempata mpangaji boya mm ningepita na shingo yako huwa sipendag unyonyaji
Hulazimishwi kupanga nyumba isiyo kuwa size yako!! Tafuta chumba kwa mtogole endesha maisha yako!
 
Upo wap mkuu nije nipange upo wap Mimi mpangaji mtiifu sicheleweshi Kodi natunza nyumba vizuri..naomba kuwasilisha.
 
Mbinu ya uhakika ni kumpa security deposit yake atumie kuhamisha vitu vyake.
Inawezekana amepata changamoto ya hela kwa sasa, msaidie unapoweza.
 
Nenda mahakamani si umejitungia sheria mwenyewe? Huyo mwamba anajua sheria atakuaibisha. Eti security deposit, umeiweka kwa mujibu wa sheria ya nchi gani. Ulimpatia notice ya miezi 3? Kujenga nyumba isiwe kibali cha kunyanyasa watu, muwe na utu hv vitu vyote ni vya kuacha hp duniani. Ongea vizuri na binadamu mwenzako uelewe tatizo lake
 
Wabongo wamezoea kulipa kodi ya miezi sita!! Wale wa kulipa kodi ya mwaka mmoja ni wachache sana.
Mi napenda kulipwa kila mwezi.

Sijawahi kuona utamu wafedha ya kodi ya mkupuo wa mwaka mzima.

Hela haikaliki, ukishakulipwa mkupuo wa mwaka mzima, unaiingiza kwenye expenditure kisha inakata kwa muda huo huo, unaanza kusubiria miezi 12 tena!

Isee, hadi unasahau kama huwa unalipwa kodi ya pango.
 
Acha mihemko, amefanya uharibifu gani. Km rangi ni ww unaipiga upya. Huyo bwana naye hazimo nyumba nyingi hivyo kwanini akubali vitu vya ajabu
 
Notsi ya miezi mitatu haipo siku hizi
 
Kuna nyumba moja Kali Sana ipo mkoa x

Tulimpangisha mzee mmoja kada wa CCM taifa yule mzee alilipa Kodi ya mwaka mmoja.

Baada ya mwaka JPM akaingia madarakani..mambo ya vyuma kukaza yaka cotton fire mambo ya kubana matumizi ya chama yaka chukua nafasi..

Yule mzee tulimvumilia ndani ya mwaka mmoja bila kulipa Kodi mzee wangu ni mtu mwema mwenye kujua utu..

Mpaka napo andika hapa muda huu uzee wangu Kuna nyumba ZAKE watu wanakaa buree sababu moja ukiwa KIJANA mzuri unatunza nyumba vizuri utakaa buree mpaka uamie Kwako.

Mpangaji kaanza kutangaza kwa umma kua mzee kamuuzia nyumba...mzee akamtaka jamaa ahame nyumba jamaa ni mbishi Sana hakuhama.

Ndipo nilipo kuja kugundua kua kumuhamisha mpangaji msumbufu ni very tough phenomena

Tulimtoa kwa nguvu ya mahakama maana tulimpa notice zikaisha yule jamaa ni msumbufu mno
 
Tanzania yetu wapangaji wengi ni wavamizi, sema ujamaa unafanya tuone kama ni wapangaji kwani asilimia kubwa hawafuati mikataba.
 
Notsi ya miezi mitatu haipo siku hizi
Utamfanya Nini mpangaji msumbufu?? Mvunjie mlango toa vitu nje then utakutana na kesi utakayo jutia maana atakwambia kapotelewa na Vito vyake vya thamani then ndio utaijua JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA..KAZI IENDELEE
 
Utamfanya Nini mpangaji msumbufu?? Mvunjie mlango toa vitu nje then utakutana na kesi utakayo jutia maana atakwambia kapotelewa na Vito vyake vya thamani then ndio utaijua JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA..KAZI IENDELEE
Kinachozingatiwa ni makubaliano yenu katika mkataba wenu. / ndiyo maana inapofika miezi mitatu kabla mkataba kwisha unatakiwa utume barua ya kumuuliza endapo ataendelea na mkataba au la!, (notice should be within the contracts)
 
Sasa mambo ya security deposit ya nini kwenye upangishaji wa chumba?

Kuna watu mnapenda complications sana aise yaani ujiaji usio na tija.

Watu tunapangisha wapangaji wanakaa hata miaka miwili hawajalipa kodi na bado mtu unamvumilia wala huna vijisababu kama vya kwako.

Kuna ndugu yangu yeye wapangaji wake wanakaa hata miaka mitatu hawajalipa kodi na wala huwezi kumkuta anaenda kwa wapangaji mara kwa mara.

Anaweza kukaa hata mwaka hajakanyaga kwa wapangaji maana hakai nyumba moja na wapangaji.
 
Mtu kukaa miaka miwili mpaka mitatu bila kulipa kodi labda kama ni ya serikali la sivyo ni biashara kichaaa na wewe siyo mfanyabiashara waache wakae bure kabisaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…