Mpangaji agoma kuhama baada ya mkataba kuisha. Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?

Mpangaji agoma kuhama baada ya mkataba kuisha. Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?

Kinachozingatiwa ni makubaliano yenu katika mkataba wenu. / ndiyo maana inapofika miezi mitatu kabla mkataba kwisha unatakiwa utume barua ya kumuuliza endapo ataendelea na mkataba au la!, (notice should be within the contracts)
Kuna wapangaji wafumbufu atavunja mkataba na la kufanya Huna zaidi labda uende mahakamani wamtoe kwa nguvu.

Bila ivyo huwezi kumtoa mpangaji msumbufu kirahisi rahisi Mr. Sisi tulikutana na mpangaji msumbufu Sanaa mpaka akawa anatangaza nyumba Ile ni yake kauziwa na mzee mtu Kama huyo anaweza kufoji documents mkaanza kusumbuana nae
 
Mtu kukaa miaka miwili mpaka mitatu bila kulipa kodi labda kama ni ya serikali la sivyo ni biashara kichaaa na wewe siyo mfanyabiashara waache wakae bure kabisaa.
Mimi ukipanga kwa mzee wangu utapata raha yule mzee hajui kudai pesa atachukulia wewe ni KIJANA wake. Utalipa kile unacho jisikia Ila kudai kufuatilia kukudai sahau. Watu wanasamehewa hata Kodi ya mwaka mzima.

Mpaka muda huu na type hapa Kuna watu wanakaa Bure kwenye nyumba za mzee wangu.
 
Kwq uelewa wangu mpangaji kama kodi imeisha inatakiwa umpe nosti ya miezi 3 ambayo atakaa free baada ya hapo ndio anatakiwa aondoke hio deposit ya pesa ambayo mnawekeana kama Iko kwenye mkataba na yeye alikubali kuwa na jambo kama Hilo na akasaini huo mkataba basi haki Iko kwako
Yaani mpangaji huna kodi ya kulipa,alafu bado nikupe notisi ya miezi 3 ukae bure!? Yaani wwe huogopi vya burebure!!??
 
Mimi ukipanga kwa mzee wangu utapata raha yule mzee hajui kudai pesa atachukulia wewe ni KIJANA wake. Utalipa kile unacho jisikia Ila kudai kufuatilia kukudai sahau. Watu wanasamehewa hata Kodi ya mwaka mzima.

Mpaka muda huu na type hapa Kuna watu wanakaa Bure kwenye nyumba za mzee wangu.
Ndiyo maana nikasema ni wavamizi lakini ujamaa na utanzania wetu unawachukulia kama ndugu zako.
 
Kuna nyumba moja Kali Sana ipo mkoa x

Tulimpangisha mzee mmoja kada wa CCM taifa yule mzee alilipa Kodi ya mwaka mmoja.

Baada ya mwaka JPM akaingia madarakani..mambo ya vyuma kukaza yaka cotton fire mambo ya kubana matumizi ya chama yaka chukua nafasi..

Yule mzee tulimvumilia ndani ya mwaka mmoja bila kulipa Kodi mzee wangu ni mtu mwema mwenye kujua utu..

Mpaka napo andika hapa muda huu uzee wangu Kuna nyumba ZAKE watu wanakaa buree sababu moja ukiwa KIJANA mzuri unatunza nyumba vizuri utakaa buree mpaka uamie Kwako.

Mpangaji kaanza kutangaza kwa umma kua mzee kamuuzia nyumba...mzee akamtaka jamaa ahame nyumba jamaa ni mbishi Sana hakuhama.

Ndipo nilipo kuja kugundua kua kumuhamisha mpangaji msumbufu ni very tough phenomena

Tulimtoa kwa nguvu ya mahakama maana tulimpa notice zikaisha yule jamaa ni msumbufu mno
Yeye kwanini alikua hataki kuhama au alijua nyie mpo mbali na mkoa anaoishi
 
Yeye kwanini alikua hataki kuhama au alijua nyie mpo mbali na mkoa anaoishi
Yaan tupo sio mbali nikama 5km..
Mkuu,
Hujawai kuona watoto watukutu shuleni hawakosekanagi ni kama wapangaji pia wapo wapangaji very stubborn.
Mtu mpaka anatangazia umma kua nyumba kainunua.

Msumbufu balaa kutoa pesa halipi kuhama hataki...Ila tulimuhamisha kwa nguvu ya mahakama.
 
Sasa mambo ya security deposit ya nini kwenye upangishaji wa chumba?

Kuna watu mnapenda complications sana aise yaani ujiaji usio na tija.

Watu tunapangisha wapangaji wanakaa hata miaka miwili hawajalipa kodi na bado mtu unamvumilia wala huna vijisababu kama vya kwako.

Kuna ndugu yangu yeye wapangaji wake wanakaa hata miaka mitatu hawajalipa kodi na wala huwezi kumkuta anaenda kwa wapangaji mara kwa mara.

Anaweza kukaa hata mwaka hajakanyaga kwa wapangaji maana hakai nyumba moja na wapangaji.
Ninyi ndiyo wale kazi yao Ni kufirisi biashara ya mtu. Kila biashara inayoanzishwa inakuwa na malengo yake. Sasa wewe unapangishwa Nyumba/Chumba alafu unakaa miaka 2 au 3 bila kulipa Kodi, huko ni kuvuruga malengo ya mtu. AU HUWA MNAMLOGA MWENYE NYUMBA ILI ASAHAU KUDAI KODI ZAKE ?
 
Unajua hapa dar Kuna watu Wana nyumba Ila Hana mtu wa kukaa??

Kwaio mfano Mimi mzee wangu nyumba ZAKE sio kua ndio anazitegemea kujikimu na kuendesha Maisha laaa.

Ana michongo yake mingine so akipata mtu mzuri wa kukaa..unamtunzia nyumba yake Mbona utakaa bureeee kabisa
 
Kuna mmoja miaka miwili hajalipa kodi katolewa kwa nguvu,nyumba imefungwa wakajua atahama analala kibarazan na watoto watatu wadogo na mkewe wanasema hawaondoki mpaka wapate haki yao 😂😂😂 na soon nyumba inavunjwa
 
Yaani mpangaji huna kodi ya kulipa,alafu bado nikupe notisi ya miezi 3 ukae bure!? Yaani wwe huogopi vya burebure!!??
Ndio na ni sheria lazima umpe mda wa huo miezi 3 free hata umpeleke wap na ukute huyo mpangaji anajua hicho kipengele lazima ukubali
 
Ndio na ni sheria lazima umpe mda wa huo miezi 3 free hata umpeleke wap na ukute huyo mpangaji anajua hicho kipengele lazima ukubali
Hakuna sheria hiyo ya kukaa kwenye nyumba ya watu bure,hata NHC huwezi ishii bure,lazima hiyo miezi ya notisi uilipie,na sheria inasema mpangaji kodi yako ikiisha na huna nyingine wwe unahesabika ni mvamizi!!
 
Adhabu yotehiyo ya nini.

Kuna mzee kopindi cha magu. Aliwaambia wapangaji wanangu hali ni ngumu...kila mmoja wenu azingatie mkataba. Ila kama unatatizo niambie usikae kimya.

Kuna binti alimwambia kama huna ukipata utanipa alikaa bure kwa muda na baasae akampa yule mzee kama milioni kama asante.

Wenye nyumba tuishi kwa upendo.wapangaji wanashukran sana wakitendewa ubinadamu
Unacheza na wapangaji. Wengi wao ni wasumbufu hakuna mfano. Kati ya wapangaji 100 mwenye shukrani ni mmoja au hakuna kabisa.
 
Ndio na ni sheria lazima umpe mda wa huo miezi 3 free hata umpeleke wap na ukute huyo mpangaji anajua hicho kipengele lazima ukubali
Kiongozi naomba unitajie hiyo sheria inayosema mpangaji apewe notisi ya miezi mitatu na akae bure kwa kipindi chote hicho nipate kuisoma vizuri.
 
Wana BODI naomba ushauri. Wapangaji wangu wote naingia nao mkataba wa miezi sita. Ambao ni renewable .

Katika mkataba kuna kipengele cha security deposit Sawa na kodi ya mwezi ambayo hutumika kutengeneza nyumba mkataba ukiisha.

Mpangaji wangu mmoja single mother mkataba wake ulikwisha mwezi January mwaka huu lakini amegoma kuhama akidai arudishiwe deposit yake ndio ahame kabla nyumba haijakaguliwa ; lakini amekwisha kaa hiyo nyumba mwaka mmoja na nusu na nyumba inahitajika matengenezo.

Amegoma kuondoka na sasa amefunga nyumba na kuacha vitu vyake ndani na kutoweka na funguo!

Ameisha kaa zaidi ya mwezi bila kulipa kodi na hata bill ya maji hajalipa! Nimekwenda serikali ya mtaa kutoa taarifa nao hawana msaada.

Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?
Siku kodi yake ilipoisha ulitakiwa kuweka makufuri makubwa kama sita hivi bila huruma
 
Polisi na mjumbe huwa wanakuja tu kishabiki wanajua hawawezi kukosa hela ya maji ila mwisho wa siku kesi ikienda mbele zaidi wanajitoa unabaki peke yako hiyo wala sio dawa.
Hapo mtego wake uko hivi mkienda kuvunja huyo mwanamke ataenda mahakamani kushitaki kwamba amevunjiwa nyumba na imesababisha upotevu wa milioni 20 kwa hivyo atataka alipwe milioni 20 kisha aondoke na vitu vyake.
Baada ya hapo polisi na mjumbe wakiitwa mahakamani watasema sisi tulikuwa mashahidi tu lakini hatuhusiki na chochote kwa hiyo mwenye nyumba ndio anajua kiundani ugomvi wake na mpangaji basi hapo wanakuwa washajitoa unabaki peke yako.
Hivi mahakamani mpangaji akishataja tu kwamba kaibiwa fedha milioni kadhaa ule usemi wa "..... prove beyond reasonable doubt" uyeyuka kabisa akilini mwa mahakimu na hivyo hawatajiangaisha ku-prove kwamba kweli mpangaji alikuwa kaacha fedha kiasi hicho ndani ya nyumba au pia ku-prove kwamba mwenye nyumba kweli aliichukua fedha hizo kwa mpangaji?
 
Ndoo maana wajanja wanawekeza kwenye bonds na utt amis ili kuepuka kero ndogondogo kama hizi.
Nilikuwa na wazo la kujenga nyumba za kupangisha, nilivyoona usumbufu wa wapangaji nikaachana nalo. Nawekeza zangu UTT etc.
 
Kama NAKUONA unavyoinbaa mwemyewee

Ur yaweah yaweah ur yaweah
Ur yaweah Alfa n omega

Komaa mpaka kieleweeke
 
Hivi mahakamani mpangaji akishataja tu kwamba kaibiwa fedha milioni kadhaa ule usemi wa "..... prove beyond reasonable doubt" uyeyuka kabisa akilini mwa mahakimu na hivyo hawatajiangaisha ku-prove kwamba kweli mpangaji alikuwa kaacha fedha kiasi hicho ndani ya nyumba au pia ku-prove kwamba mwenye nyumba kweli aliichukua fedha hizo kwa mpangaji?
Kibongobongo ni ngumu kupata ushahidi visible wa scenario kama hii kwa nchi za wenzetu nadhani wana technology zao za kuweza kuprove kwenye kila tukio,so hapo mtahukumiwa au kufungana kwa kutumia logical facts.
Ila mimi sio mtaalamu wa sheria natumia uzoefu wangu binafsi ndugu kama kuna wanasheria humu watakuja kutuelezea zaidi kiundani inavyokuwa.
 
Hivi mahakamani mpangaji akishataja tu kwamba kaibiwa fedha milioni kadhaa ule usemi wa "..... prove beyond reasonable doubt" uyeyuka kabisa akilini mwa mahakimu na hivyo hawatajiangaisha ku-prove kwamba kweli mpangaji alikuwa kaacha fedha kiasi hicho ndani ya nyumba au pia ku-prove kwamba mwenye nyumba kweli aliichukua fedha hizo kwa mpangaji?
Kitu kingine cha kuongezea hapo kwenye jibu la swali lako,kwa mfano mpangaji aking'ang'ania kwamba ana uhakika kweli aliacha milioni 20 ndani ya nyumba yake hakimu au wakili wa mwenye nyumba anaweza akamuuliza swali mpangaji swali hili hapa ili kujiridhisha zaidi.
"Je unaweza ukatuthibitishia kwamba kweli ulikuwa unamiliki kiasi hicho cha pesa?"
Mpangaji:Ndio,niliuza shamba langu kijijini kwetu mwezi uliopita kisha fedha nikazihifadhi ndani.
Sasa kama amekukamia hizo documents za kuonyesha kweli aliuza shamba ni rahisi tu kuzipata na wanunuzi feki watapatikana ili akunyooshe.
 
Back
Top Bottom