Mpango wa wazungu ni kuua kabisa taasisi ndoa

 
Nimeona mtoa mada kaongelea midoli ngono, lesbianism, gays, ndoa za mikataba na ndoa za wanyama. Hoja yako ijikite kwenye vyote sio kakitu kamoja tu
 
Ndoa na mahusiano yame gubikwa na wingu kubwa la
1. Usawa wa kijinsia
2. Uharakati katika mapenzi
3. Uoga wa maisha
4. Kuingia katika ktk ndoa / mahusiano pasipo kuwa na maana yako ya mapenzi kichwan, mtu amekariri maana za mapenzi za wengine km mapenz pesa, mapenz hakunaga, mapenz yana mwisho, mapenzi hayana fomula nk (wapo wapo tu ni mabomu ya muda)
5. Watu hawana elimu ya mahusiano na hawataki kujifunza.
6. Watu wanaendekeza sana uasherati na wanafanya sifa ya maisha .( prestige).
7. Uigaji wa mambo ya kisasa katika ndoa na mahusiano.
8. Biashara
Yaani tajiri haangushi na maskini haokoti ni kizaizai, wote wana hali moja.
 
Nimekuelewa Sana Mkuu. Na ndio maana nimerudi nyuma kabisa.
Kama ulivyosema ndoa ni baraka ya Mungu. Ambayo imeshatushinda ndio maana imekuwa rahisi aina nyingine ya ndoa kuibuka na kukubalika na binadamu.
Mambo ya ndoa huanzia rohoni na yako kiroho zaidi. Ukiendesha ndoa kwa namna ya kimwili jua ndoa yako isha teleza na kumwagika.


Gal 5:16-26 SUV

Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.
 
Uharakati katika mapenzi
Wazungu na mambo yao ya women empowering. (Wanawake kuwezeshwa kiuchumi ni jambo bora sana, ila kadiri unavyokuwa kiuchumi ndivyo unavyotakiwa kuwa mnyenyekevu kwa mumeo)
 
Acha tu mzee mwenzangu.

Yaani navyoyachukiaga hayo mazungu,nikiyaonaga huwa nawaangalia kwa jicho baya sana.
 
Mzungu asisingiziwe, watu wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawajui kwanini wanaingia kwenye ndoa.

Wanapuyanga tu huko ndoani Kwa ujinga ujinga mwingi.
Utaambiwa tafuta hela , wakat huo huo mke wa Billgate alimwacha mke wake , nafkr ndoa inahtaji mpendane tuu , upendo huwa unameza kasoro nyingi Sana na ni nguzo ya uvumilivu .... Money can not buy this , mkioana Kwa kuangalia material thing , hamchukui round, ni ngumu kuvuka miaka 15 mkiwa pamoja
 
Mnawasingizia sana wazungu ndiyo maana kila siku tunaparanganyika sababu hatujifunzi kutokana na makosa yetu.
Ni wapi nimewasingizia wazungu? Je sex dolls hazijaletwa na wazungu? Vipi kuhusu ndoa za mkataba hazijaanzia kwao? Ndoa na wanyama je? Ushoga?
 
Umeandika ukweli Mkuu,tatizo ni kwamba tumeshikwa masikio ila hatutaki kukubali....UTANDAWAZI utatuua
Elimu ya jando ilikuwa bora mara 100 kuliko ya sasa. Ili reflect maisha yetu halisi na namna ya kuyamudu.

Elimu ya Afrka ilitueleza rasilimali ni nyingi kutuwezesha kututosheleza sote. Elimu ya mzungu ikatuambia rasilimali ni chache na adimu (scarcity of natural resources)

Matokeo yake akili zetu zimekuwa tegemezi. Tuna dhahabu tele tunaenda kuomba msaada wa kondom.

Matokeo yake tunapewa msaada wa condom na KY Jelly bure ila kwa masharti kwamba tuheshimu haki za mashoga na KY zigawiwe bure
 
Hii ni maono Yao tu ila hajaleta lolote wao wanafikisha mawazo Yao tu Kwa jamii. Tokea Hawa walikuwa wanapeana utamu .


Hakuna jipya chini ya jua
 
Msitishane maisha ni wewe unavyotaka yawe..utandawazi unavuruga sana concetration mambo ni mengi mpk tunaelemewa...as hakuna kipya chini ya jua...fata kile unachokiamini usitetereke fundisha na kizazi chako njia ziwapaswazo na hawata ziacha...na Mungu atawabariki hawatakengeuka...
 
Ila ndoa pia si walileta wao? Labda wameamua kubadilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…